Mwigulu, Mnyika, Zitto, Mdee na Silinde waweza leta sura mpya sakata la Escrow leo Bungeni

Hii skendo jamani ki hoja na facts kwa kweli imewakalia ovyo ma CCM, lakini CCM wanachojivunia ni uingi wao pale bungeni..watoa hoja wa ccm ilikuwa ni mipasho bila supporting evidences, lugha za mitaani na lugha za khanga mtupu..Naunga hoja ya mchangiaji mmoja ktk uzi mmoja kuwa upinzani wanapotoa hoja nzito na facts, Komba,Lusinde,Maji marefu na wengine hawakufahamu kutokana na uelewa wao mdogo..Naunga mkono..Lusinde alipokuwa anatoa viroja jana, Maccm wote walikuwa wameamka ndio kusema wanaelewa na wanafurahia matusi na lugha za mitaani…

kwa upande mwingine hii kitu itawakalia vibaya zaidi ma CCM kama serikali ya ccm itajiudhuru..wanaogopa kuwa watawapa upinzani cha kuwaeleza wananchi kuwa wezi wa mali ya Umma ni ccm na hapo ndipo watakosa kura zaidi…Tukumbuke kuwa wabunge wengi wa CCM hawatachaguliwa tena kama vipindi vilivyopita..
Hapa wanajalibu kushika kila tawi na majani lakini wanaanguka tu
Kama Mtanzania,Kilichotokea jana kimeniaibisha sana kwa kuwa na wawakilishi kama hawa wa CCM.

NASHAURI NJIA MOJAWAPO YA KUWATOA HAWA MAGAMBA NI KUSHAWISHI FAMILIA YAKO, MAJIRANI,MARAFIKI NA MTU YEYOTE AENDE KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA..HIYO NDIO KARATA YETU SISI TUSIO BUNGENI DODOMA
 
Mwigulu aliishabeba ushujaa kwa namna magazeti yalivyomuandika kuhusu hiyo hoja na ata wengine tukaanza kuweka imani kwake ata kwa 2015.

Sasa ni nafasi yake kuonyesha kama anastahili kweli hiyo imani iliyoanza kumea.
 
Orodha ya wachangiaji wa Asubuhi ya leo

1.MWIGULU NCHEMBA
2.ESTHER BULAYA
3.ZITO KABWE
4.J.MNYIKA
5.LEMA
6.LEMBELI
7.DR KINGWANGALA
8.J.MPINA
9.D.FILIKUNJOMBE
10.KANGI LUGOLA
11.SILINDE
12.MDEE
13.NASARI
15.MACHALI
16.MBATIA

Zitto ndio mtoa hoja atachangia VP sasa ama badala yake atamshkia keissy wa nkasi? Sijaelewa
 
Acha hizo,ukiondoa maeneo machache sana presentation ya lusinde ilikuwa ya kieango cha juu sana

Kiwango kipi mkuu...?
Kutojua Ethics za Utawala ni kiwango cha juu?

Kutojua jinsi ya kuongea ukiwa na watu wa Imani tofauti ni kiwango cha juu?

Kwangu nilishindwa kabisa kumtofautisha na Akina mama waliokua wanagombana na mamaangu a way back, hasa ile mipasho na maneno mengi ya kanga...and he still entitled to be called " Mheshimiwa"!!!
Never!
 
Hiyo listi inafanya wale wapambe wa pinda wahangaike na noti mapema kabisa asubuhi hii wahakikishe wanajaribu kupenyeza kwa hao waheshimiwa ili waikatae ripoti ya bunge lao! Sina imani sana na mwigulu katika kutetea raslimali za nchi hasa haya mabilioni yaliyochotwa pale B.o.T Kwa amri ya baba riz pale magogoni!
 
VIchwa vya leo vya kutoa hoja viko makini sana na wanauwezo wa kujenga hoja na kuitetea safi wabunge wa namna hii sio tunakuwa na wabunge maslahi kama kina Lukuvi na wenzake.
 
Kumbe matusi na kukashifu imani za watu ni facts? mh ninawasi wasi na namna tunavyoweza kuwaunga watu mkono kwa hoja zao. Bila matusi inawezekana ukajenga hoja na ikakubarika tu
 
Mwigulu aliishabeba ushujaa kwa namna magazeti yalivyomuandika kuhusu hiyo hoja na ata wengine tukaanza kuweka imani kwake ata kwa 2015.

Sasa ni nafasi yake kuonyesha kama anastahili kweli hiyo imani iliyoanza kumea.

Usimuamini Mwana CCM yeyote unaweza ukakuta Mwigulu Nchemba akawasafisha maofisa wa TRA na RITA na Wote waliokwapua Pesa.
 
Last edited by a moderator:
Mwigulu aliishabeba ushujaa kwa namna magazeti yalivyomuandika kuhusu hiyo hoja na ata wengine tukaanza kuweka imani kwake ata kwa 2015.

Sasa ni nafasi yake kuonyesha kama anastahili kweli hiyo imani iliyoanza kumea.

Sidhani kama Mwigulu atakuwa na jipya tofauti na Magamba waliomtangulia! !!!!
 
....kuna hoja ambazo hakika watu wa serikali kupitia utetezi wa muhongo(mtu muongo)wamejitahidi sana kuupotosha umma ili kuficha ukweli na uzito wa wizi huu....na wale wabunge wengine wa ccm(aina za kina lusinde)wametoa mipasho badala ya hoja kuficha uovu huu...hata kufikia kutaka kuonyesha kuwa eti kazi ya kamati ya PAC ni ya wapinzani....huku wakisahau kuwa kazi hii ya PAC pia imewahusisha wenzao huko ccm....Hii inasikitisha sana na inaonyesha jinsi watu walivyojipanga kuwatetea wezi kwa namna yoyote ili kulinda maslahi yao.....


My take mpaka sasa..

1. Ni kawaida ya wezi kukana kuiba hata kama wameshikwa ready handed...its just natural kwao kukana kuiba....hili halishangazi...

2.Muhongo na wanaowatetea wezi wamejitahidi eti kuaminisha uma kuwa serikali ina kinga dhidi ya madai baada ya kubariki wizi huu,....hii si kweli kwani tayari SCBHK wamewaapa siku 30 tanesco kuwa pesa ya escrow irudi....kwani wamegundua kuwa wameruhusu pesa zitolewe kwa third party(PAP)ambao hawakuwepo kwenye makubaliano ya awali....bila hivyo SCBHK watashtak tanesco.....Haya tayari yanatupeleka kwenye madai...maana tayari PAP si wamiliki halali wa IPTL...na kinga yao kwa serikali inakua redundant....Ama tanesco si taasisi ya serikali??kwamba madai kwa tanesco hayaihusu serikali????....ama mikataba ya tanesco haiihusu serikali ya TZ????mbona waziri anajiweka mbali hata na maamuzi ya mahakama ya usuluhishi yaliyohusu tanesco kana kwamba hayana uhusiano na serikali ya TZ???...ama mkopo wa SCBHK kwa IPTL..eti ulifanyika huko nje na hivyo hauihusu serikali ya TZ???kwani IPTL walikua wanafanya kazi na nani hapa TZ wakati mkopo unachukuliwa??si tanesco?...sasa serikali inajiwekaje mbali wakati tanesco ni taasisi yake???...nani atalipa haya madeni??? mambo Muhongo amejitahidi sana kupindisha.....


3. Waziri Muhongo anawaaminisha uma kuwa Nimrod Mkono ametafuna pesa ndefu sana y umma..Tujiulize..nani alimpa kazi Mkono kama sio hao hao tanesco (serikali)??kwanza Mkono ni mtu wao huko ccm....sasa tujiulize...MKono kafanya kazi kalipwa mabilioni na serikali kwa kazi aliyowafanyia kwa makubaliano yao....leo inakuwaje inakua nongwa kwao serikali???nani alimpa kazi Mkono???nani alaumiwe???....Mwisho...iweje Mkono alaumiwe kwa malipo kwa kazi aliyowafanyia wakati leo watu wamelipwa mabilioni ya escrow kwa kazi ambazo hawajafanya(rejeeni bank statement ya JR kule MKombozi)???...

4.Issue ya pesa ni za serikali ama la...Hivi hata kama hela si za serikali..nani ametoa justification kwamba ziibiwe??kwamba kwa vile si za serikali ndio ziibwe???..haya madai ya serikali ndio yanadhiirisha walivyopanga kuziiba hizi hela....kwamba liwalo na liwe vile si za kwetu???..huu ujinga ndio unaudhi na kwa msimamo huu wafadhili ndio kabisaa watazidi kushikilia pesa zao....maana mnazziba mkijua si jasho lenu....

5.Issue hii serikali na watetezi wake wanataka kuifanya iwe ni ya Zitto/Kafulila vs wabaya wao...lakini ifahamike kuwa wahisani wanajua sana sana kwamba wizi huu umefanyika na wahusika wanajulikana....na kwa maana hiyo hii issue ni zaidi ya serikali wanavyofikiria....Tutafakari...
 
Back
Top Bottom