Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,432
- 7,055
Dkt. Mwigulu Nchemba, amejibu hoja ya Zitto Kabwe: Tangu lini Rais anaheshimu Bunge? Kosa la Lugola ni kufanya dili kwa kumzunguka Rais, hoja ya Bunge ni kisingizio tu
Ameandika:
Bwana zitto, jifunze kutafakari kabla hujaandika. Rais ameongelea "Mradi wa hovyo" na anasema mradi huu hauko kwenye bajeti, wala haukupitishwa kwenye baraza la mawaziri na bunge.
Sasa vinginevyo na unavyovisema, miradi kama Airport, SGR, e-passport, ununuzi wa ndege na mingine ni miradi iliyopo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, imepitiwa na Baraza la Mawaziri, ipo kwenye Bajeti na imepitishwa bungeni.
Acha kupotosha watu, mikataba huwa haisainiwi bungeni, wala hakuna siku bunge litajadili mkataba wa mradi labda maazimio na taarifa ya mkataba.
Kwa mikopo, kila mwaka serikali inaleta mapendekezo ya kukopa kwenye bajeti kuu na tunapitisha., sasa mantiki ya unachokisema iko wapi? Kama kawaida yako unapotosha kwa makusudi, kisiasa na kirafiki.
Nani asiyejua ulikuwa kamati moja na kangi na wengine uliwatumia sana kwa maslahi binafsi? Watanzania wanakumbuka urafiki wenu ule na kwa maslahi yenu binafsi.