Mwigulu Lameck Nchemba: Uchambuzi wa wagombea Urais CCM

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,665
4,797
Historia yake

Mwigulu Lameck Nchemba alizaliwa Januari 7, 1975 mkoani Singida, hivyo alifikisha miaka 40 Januari 7, mwaka huu. Kwa sasa yeye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) upande wa Tanzania Bara na ni Naibu Waziri wa Fedha.

Mwigulu alianza masomo yake katika Shule ya Msingi Makunda wilayani Iramba, Singida mwaka 1987 na kuhitimu mwaka 1993. Alijiunga na Shule ya Sekondari Ilboru kwa masomo ya kidato cha I – IV mwaka 1987 – 1993 kisha akafaulu na kuanza kidato cha V na VI Mazengo Sekondari, Dodoma.

Baada ya kukamilisha masomo yake ya kidato cha sita, Mwigulu alichaguliwa kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisomea masuala ya Uchumi. Alihitimu Shahada ya Kwanza ya Uchumi mwaka 2004 na kupata daraja la kwanza, akaunganisha kusomea Shahada ya Uzamili ya Uchumi ambayo aliikamilisha mwaka 2006.

Baada ya kukamilisha masomo yake, Mwigulu alijiunga na utumishi wa umma katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kitengo cha sera za uchumi, akiwa mchumi daraja la I na wakati huohuo akiendelea na harakati za siasa ndani ya CCM.

Nyota yake kisiasa ilianza kung’ara mwaka 2001 alipochaguliwa kuwa mjumbe wa vijana wa Wilaya ya Iramba, mwaka 2008 akawa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) na mwaka huohuo, akachaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu kupitia Umoja wa Vijana (UVCCM). Mwigulu ameoa na ana watoto.

Mbio za ubunge

Mwigulu anatoka katika familia ya kawaida ya wazazi wasio na uwezo sana. Yeye mwenyewe anasema kama isingelikuwa “sera ya kutoa mikopo kwa wanafunzi,” basi asingelisoma. Pamoja na umasikini wa familia yake, yeye alikuwa na ndoto kubwa, alihitaji kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo alilozaliwa ili atumie elimu na uzoefu wake kuwasaidia wananchi.

Mwaka 2010, Mwigulu aliacha kazi nzuri pale BoT akajitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuusaka ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi. Alitumia vizuri udhaifu wa Mbunge wa Iramba Magharibi wakati huo, Juma Hassan Kilimba, akaomba ridhaa kwa chama chake na kufikia hatua ya kura za maoni ambako alimshinda Kilimba kwa kura chache na kufanikiwa kuteuliwa na CCM kuwania nafasi hiyo.

Katika uchaguzi wa jumla, nguvu ya Mwigulu iliamsha uimara wa CCM akapata asilimia 87.6 dhidi ya asilimia 9.4 za vyama vyote vya upinzani, akawa Mbunge wa Jimbo la Iramba.

Mwigulu aliendelea na safari yake ya utumishi kwa wana Iramba Magharibi na ilipofika Aprili 2011, Katibu Mkuu wa CCM wa wakati huo, Yussuf Makamba na sekretarieti nzima walipojiuzulu ili kutekeleza ile dhana ya “kujivua gamba,” chama hicho kilimteua Mwigulu kushikilia wadhifa wa Katibu wa Uchumi na Fedha chini ya Katibu Mkuu mpya, Wilson Mkama.

Katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa CCM Novemba 2012, Mkama alipumzishwa katika majukumu yake na CCM ilijiunda upya, sekretarieti ikiwekwa chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Mwigulu alipanda kisiasa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara.

Nyota ya Mwigulu ilipaa zaidi, Januari 2014 kijana huyo aliongezewa mzigo mzito zaidi wa moja ya wizara nyeti katika nchi, Wizara ya Fedha.

Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika wakati ambao Serikali ilikuwa inakabiliwa na matatizo lukuki ya kiuchumi na mbaya zaidi, alipewa wadhifa huo ili kufanya kazi chini ya waziri mwenye uzoefu mdogo, Saada Mkuya.

Umaarufu wake kisiasa ulizidi kukua kwa sababu ya kufanya kazi katika Wizara ya Fedha.

Mara nyingine amekuwa akisikika akitamka kauli ambazo zinawatia moyo Watanzania wengi kuhusu masuala ya uchumi wa nchi, hata kama kauli hizo hazitekelezeki na hana uwezo wa kuzitekeleza.

Baadhi ya watu wanamwona kama kijana mchapakazi lakini anayekwamishwa na miundombinu ya chama na Serikali yake.

Mbio za urais

Mwigulu aliingia kwenye rekodi ya watu wanaodhaniwa kuutaka urais mwaka 2013 aliponukuliwa na vyombo vya habari akidai kuwa “… wananchi ndiyo waamuzi wa mwisho. Endapo wataona nafaa kuwa rais, basi nitafanya hivyo kwa sababu nipo tayari kuwatumikia katika nafasi yoyote”.

Kauli hiyo ilichukuliwa kwa umakini mkubwa na wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa na hata ndani ya chama chake na ikaanza kufanyiwa utafiti ikilinganishwa na matendo yake kisiasa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Mwigulu alizidisha moto wake wa kujipanga kuwania urais ndani ya CCM mwaka 2014 alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha huku pia akishikilia kofia ya Unaibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara. Hali hiyo ilisababisha Kamati ya Maadili ya chama hicho kumweka katika kundi la wagombea urais waliopigwa marufuku na chama hicho kuendeleza harakati za wazi za nafasi hiyo kabla chama hakijategua “kitendawili”.

Pamoja na onyo hilo, Mwigulu alitumia kofia yake ya uongozi ndani ya CCM na kufanya ziara zilizoandaliwa kimkakati mwaka jana tena kwa kutumia “chopa”.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisitisha ziara za Mwigulu Januari mwaka huu na kumtaka atoe taarifa kwake (Kinana) ili kupata kibali kabla ya kufanya ziara yoyote ya chama.

Nguvu yake

Mwigulu si “king’ang’anizi” na anajifunza kutokana na makosa yake. Sifa hii ni muhimu sana. Siku za nyuma aliongoza wanaCCM na wabunge wa chama chake kushambulia na kutumia lugha chafu dhidi ya upinzani.

Mfano, aliwaita “magaidi,” “wanataka kuleta ushoga” na kwamba “bajeti ya kambi ya upinzani ni ya waongoza disko.” Lakini Mwigulu ninayemjadili hapa leo, ni mtu tofauti.

Hivi sasa anasimama na kujadili hoja na anatumia lugha ya staha, amekuwa kiongozi mwema kwa kuonyesha kuwa hawezi kurudia kule alikotoka. Hili ni jambo jema.

Katika Bunge Maalumu la Katiba, Mwigulu alitoa rai zipigwe hesabu kujua kama akidi ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa itatimia, vinginevyo Bunge liahirishwe kuokoa muda na fedha zinazopotea bure kwa posho.

Nguvu nyingine ya Mwigulu iko katika mitandao ya kijamii. Alipokuwa anashambulia vyama vya upinzani na watu wenye mtazamo kinzani kwa CCM, vijana wengi walimshambulia kwenye mitandao na alikuwa hapendwi. Yeye mwenyewe alilijua hilo na alipata kutamka; “najua nachukiwa sana na vijana kwa sababu ya kuitetea CCM”.

Leo ukitembelea akaunti za Mwigulu na marafiki zake, unakuta maoni chanya juu yake na siku hizi kila analofanya linabandikwa mtandaoni. Nguvu hii ya mitandao si ya kudharau kwa siasa za sasa na inamwongezea safari.

Jambo la tatu linalompa nguvu ni kuaminiwa ndani ya CCM. Wana CCM na hasa viongozi wa juu wa chama hicho wanamwamini.

Moja ya mambo ambayo niliambiwa na watu wake wa karibu ni uaminifu; kwamba hapendi maisha makubwa ya kifahari na huwa tayari kuishi kulingana na mazingira yaliyopo, ndiyo maana hadi hivi leo ameendelea kupanda ngazi na kufika hapa alipo.

Kuna wakati tetesi zilienezwa kuwa nafasi aliyo nayo sasa ndani ya CCM ya Unaibu Katibu Mkuu Bara itakabidhiwa kwa John Nchimbi ili kumfanya awekeze nguvu kwenye Wizara ya Fedha.

Naona suala hilo halitatimia na Mwigulu ataendelea kuongoza chama hicho hadi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Tofauti na watu wengi wanavyomfikiria, kwa kumwona kwenye TV akipambana na wapinzani, wengi hawajui kuwa Mwigulu ni mpole, mchangamfu na anajichanganya sana na watu. Suala hili linamwongezea vigezo muhimu katika safari yake.

Mwigulu hakatai kupokea simu ya mtu hata kama haifahamu na haachi kujichanganya na vijana kila anapopata nafasi. Hili ni jambo kubwa ambalo limewashinda vijana wengi waliopewa nyadhifa kidogo tu ndani ya CCM.

Udhaifu wake

Udhaifu wake mkubwa ni mtu anayejifunza polepole mno; siyo darasani, bali katika siasa. Kwa kipindi chote tangu 2010 hadi 2013 aliendesha siasa za kimafia dhidi ya vyama vya upinzani na watu walioikosoa CCM.

Pamoja na kuwa amebadilika, amechelewa kiasi watu wengi walianza kumchukulia vibaya. Kwa sasa tunaweza kuendelea kumpima kwa sababu bado ana muda katika ofisi za umma na ikiwa ameondosha udhaifu huo tutamjua.

Udhaifu mwingine mkubwa kwake ni kuchukulia mambo kirahisi na kudhani kuwa yeye peke yake anaweza kuleta mabadiliko bila kuwashirikisha watu wengine.

Mfano mzuri ni pale Wizara ya Fedha inapofanya uamuzi fulani, Mwigulu hukimbilia kudai kuwa yeye ndiye amefanya uamuzi huo. Mwaka jana, alitangaza kuwa anapambana na “wafanyakazi hewa serikalini” na amefanikiwa kuwatokomeza kwenye malipo ya fedha za umma.

Juhudi za mapambano hayo zilifanywa na Wizara ya Fedha nzima lakini Mwigulu na marafiki zake wanataka jamii ielewe kuwa bila yeye jambo hilo lisingefanyika.

Unapokuwa unafanya uongozi na wenzako, tena uko chini ya mtu, lazima ujifunze kuwa kila linalofanyika linafanywa na timu nzima na kamwe si wewe peke yako. Kujichukulia “ujiko” huko ni moja ya udhaifu na unaweza kuwa na maana pana na “hasi” kiuongozi.

Nini kinaweza kumfanya apitishwe

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa Mwigulu anaungwa mkono nje ya CCM hivyo, ikiwa CCM inahitaji rais kijana si jambo la kupuuza.

Miaka michache iliyopita, alikuwa anachukiwa lakini amefanikiwa kubadilika kwa maneno na vitendo na kujiweka katika ngazi tofauti; sasa anaonekana kama kiongozi anayefikiri sawasawa, tena kwa kutumia akili zake.

Jambo la pili ni mtandao ndani ya chama. Mwigulu anaonekana kama kijana wa kipekee ndani ya CCM aliyejijenga na kuungwa mkono. Hii ni sababu kubwa inayoweza kumwongezea sifa za kupewa kijiti.

Jambo la tatu ni taaluma yake. Mwigulu ni msomi mzuri na aliyefuzu kwa alama za juu sana katika masomo yake ya chuo kikuu na hata sekondari. Amebobea katika masuala ya uchumi na tatizo la nchi yetu ni uchumi. CCM inaweza kumwona kama mtu muhimu katika eneo hilo.

Jambo la nne ni ujana. Sifa hii inamweka kwenye karai moja na wagombea wengine vijana na huenda isiwe na mashiko sana hadi pale itakapoonekana chama hicho kinahitaji mgombea urais kijana.

Jambo la mwisho linaloweza kumsaidia apitishwe ni kutokuishi katika makundi.

Mwigulu amekuwa kiongozi ndani ya CCM akiwa anajiweka mbali na makundi, hivyo, ikiwa CCM itahitaji mgombea asiye na makundi yenye nguvu kubwa, basi yeye pia ataingia kwenye orodha hiyo.

Nini kinaweza kumwangusha

Uzoefu ni suala zito linaloweza kumwangusha Mwigulu. Amekuwa mbunge kwa miaka mitano tu na amekuwa kiongozi wa CCM katika kipindi hicho tu na amekuwa serikalini kama Naibu Waziri kwa miaka miwili peke yake.

Huu ni uzoefu mdogo mno ukilinganisha na wakongwe lukuki waliokitumikia chama hicho kwa miongo kadhaa.

Pili, anaweza kuangushwa na maswali ya wanaomsaidia kifedha. Mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa akitumia chopa katika mikutano yake ambayo ilikuwa sehemu ya ziara binafsi.

Mwigulu anajulikana kuwa kijana wa kawaida asiye na fedha, utumiaji wa chopa kufanya ziara zenye gharama kubwa kama ilivyokuwa kinaweza kuwa kitendawili kitakachofanya ahukumiwe na vikao vya chama chake, kwamba waliokuwa wanamfadhili ni kina nani na wana malengo gani?

Ikumbukwe kuwa Mwigulu yuko kwenye kapu la wagombea walioanza kampeni mapema na kushtukiwa kabla ya kupewa karipio.

Ikiwa CCM itaweka msimamo kuwa waliocheza rafu wote wasifikiriwe, Mwigulu anaweza kuanguka kirahisi na bila kujitetea.

Dhana ya kumwandaa kwa ajili ya CCM ya miaka ijayo inaweza pia kumwangusha.

Wazee wa chama wanaweza kudai kuwa ni kijana mzuri lakini asubiri wakati zaidi upite. Moja kwa moja, sababu hii isiyo na maana yoyote kidemokrasia, inaweza kumpeleka nje ya ulingo.

Asipopitishwa (Mpango B)

Ikiwa Mwigulu hatapitishwa na CCM kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho, nadhani chaguo atakalobakia nalo ni kutumia ushawishi wake kumuunga mkono rais atakayependekezwa na chama chake.

Bila shaka, yeye atarudi kugombea ubunge jimboni kwake Iramba Magharibi na kupiga hesabu za kukwaa uwaziri kamili kwenye baraza la mawaziri litakalofuata, ikiwa CCM ndiyo itashinda uchaguzi.

Mwigulu anaonekana kuwa kijana mwenye bahati. Ukifuatilia historia yake utagundua kuwa ametoka kwenye familia ya kawaida na kwamba amefika hapo alipo kisiasa kwa juhudi kubwa alizowekeza.

Mtu wa namna hii anahitaji kuwa mtulivu kama anahitaji mafanikio ya kisiasa siku za mbele.

Hitimisho

Kwa sababu ameonyesha kuwa “anang’ara” kuliko vijana wengine wanaosaka urais ndani ya CCM, inawezekana kuwa nyota hiyo ikaendelea miaka inayokuja na siku moja “ikamtoa”.

Jambo la msingi atakalopaswa kufanya ni kutokuwa na purukushani zisizo na msingi na kutorudi katika maisha ya mashambulizi ambayo aliwahi kuyafanya kipindi cha nyuma, maisha ambayo, naamini, anapoyakumbuka anajiona alikuwa “hajakua”.

Nimemjadili Mwigulu mtu ninayemjua kwani ni mtu wangu wa karibu na mara nyingi huwa tunawasiliana.

Namfahamu vizuri na namwona kama kiongozi mzuri wa baadaye. Kwa sasa namwona kama mtu anayehitaji kujifunza na kufundishwa zaidi.

Kazi ya kwenda Ikulu ili kuongoza nchi inahitaji ukomavu mkubwa zaidi ya ule alionao Mwigulu, na hapa ile dhana ya “ujana” naiondoa kidogo.

Hata hivyo, Namtakia Mwigulu Nchemba safari salama katika hatua aliyofikia, kuona kama atayapata matarajio yake.
chanzo mwanchi
 
Mbona hajasema kuwa mwiguluneti ni kati ya majangili hatari afrika mashariki?
 
Watu wako bize na Zitto sahivi hawawezi kusoma notes hizi
 
Historia yake

Mwigulu Lameck Nchemba alizaliwa Januari 7, 1975 mkoani Singida, hivyo alifikisha miaka 40 Januari 7, mwaka huu. Kwa sasa yeye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) upande wa Tanzania Bara na ni Naibu Waziri wa Fedha.

Mwigulu alianza masomo yake katika Shule ya Msingi Makunda wilayani Iramba, Singida mwaka 1987 na kuhitimu mwaka 1993. Alijiunga na Shule ya Sekondari Ilboru kwa masomo ya kidato cha I – IV mwaka 1987 – 1993 kisha akafaulu na kuanza kidato cha V na VI Mazengo Sekondari, Dodoma.

Baada ya kukamilisha masomo yake ya kidato cha sita, Mwigulu alichaguliwa kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisomea masuala ya Uchumi. Alihitimu Shahada ya Kwanza ya Uchumi mwaka 2004 na kupata daraja la kwanza, akaunganisha kusomea Shahada ya Uzamili ya Uchumi ambayo aliikamilisha mwaka 2006.

Baada ya kukamilisha masomo yake, Mwigulu alijiunga na utumishi wa umma katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kitengo cha sera za uchumi, akiwa mchumi daraja la I na wakati huohuo akiendelea na harakati za siasa ndani ya CCM.

Nyota yake kisiasa ilianza kung'ara mwaka 2001 alipochaguliwa kuwa mjumbe wa vijana wa Wilaya ya Iramba, mwaka 2008 akawa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) na mwaka huohuo, akachaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu kupitia Umoja wa Vijana (UVCCM). Mwigulu ameoa na ana watoto.

Mbio za ubunge

Mwigulu anatoka katika familia ya kawaida ya wazazi wasio na uwezo sana. Yeye mwenyewe anasema kama isingelikuwa "sera ya kutoa mikopo kwa wanafunzi," basi asingelisoma. Pamoja na umasikini wa familia yake, yeye alikuwa na ndoto kubwa, alihitaji kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo alilozaliwa ili atumie elimu na uzoefu wake kuwasaidia wananchi.

Mwaka 2010, Mwigulu aliacha kazi nzuri pale BoT akajitosa kwenye kinyang'anyiro cha kuusaka ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi. Alitumia vizuri udhaifu wa Mbunge wa Iramba Magharibi wakati huo, Juma Hassan Kilimba, akaomba ridhaa kwa chama chake na kufikia hatua ya kura za maoni ambako alimshinda Kilimba kwa kura chache na kufanikiwa kuteuliwa na CCM kuwania nafasi hiyo.

Katika uchaguzi wa jumla, nguvu ya Mwigulu iliamsha uimara wa CCM akapata asilimia 87.6 dhidi ya asilimia 9.4 za vyama vyote vya upinzani, akawa Mbunge wa Jimbo la Iramba.

Mwigulu aliendelea na safari yake ya utumishi kwa wana Iramba Magharibi na ilipofika Aprili 2011, Katibu Mkuu wa CCM wa wakati huo, Yussuf Makamba na sekretarieti nzima walipojiuzulu ili kutekeleza ile dhana ya "kujivua gamba," chama hicho kilimteua Mwigulu kushikilia wadhifa wa Katibu wa Uchumi na Fedha chini ya Katibu Mkuu mpya, Wilson Mkama.

Katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa CCM Novemba 2012, Mkama alipumzishwa katika majukumu yake na CCM ilijiunda upya, sekretarieti ikiwekwa chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Mwigulu alipanda kisiasa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara.

Nyota ya Mwigulu ilipaa zaidi, Januari 2014 kijana huyo aliongezewa mzigo mzito zaidi wa moja ya wizara nyeti katika nchi, Wizara ya Fedha.

Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika wakati ambao Serikali ilikuwa inakabiliwa na matatizo lukuki ya kiuchumi na mbaya zaidi, alipewa wadhifa huo ili kufanya kazi chini ya waziri mwenye uzoefu mdogo, Saada Mkuya.

Umaarufu wake kisiasa ulizidi kukua kwa sababu ya kufanya kazi katika Wizara ya Fedha.

Mara nyingine amekuwa akisikika akitamka kauli ambazo zinawatia moyo Watanzania wengi kuhusu masuala ya uchumi wa nchi, hata kama kauli hizo hazitekelezeki na hana uwezo wa kuzitekeleza.

Baadhi ya watu wanamwona kama kijana mchapakazi lakini anayekwamishwa na miundombinu ya chama na Serikali yake.

Mbio za urais

Mwigulu aliingia kwenye rekodi ya watu wanaodhaniwa kuutaka urais mwaka 2013 aliponukuliwa na vyombo vya habari akidai kuwa "… wananchi ndiyo waamuzi wa mwisho. Endapo wataona nafaa kuwa rais, basi nitafanya hivyo kwa sababu nipo tayari kuwatumikia katika nafasi yoyote".

Kauli hiyo ilichukuliwa kwa umakini mkubwa na wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa na hata ndani ya chama chake na ikaanza kufanyiwa utafiti ikilinganishwa na matendo yake kisiasa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Mwigulu alizidisha moto wake wa kujipanga kuwania urais ndani ya CCM mwaka 2014 alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha huku pia akishikilia kofia ya Unaibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara. Hali hiyo ilisababisha Kamati ya Maadili ya chama hicho kumweka katika kundi la wagombea urais waliopigwa marufuku na chama hicho kuendeleza harakati za wazi za nafasi hiyo kabla chama hakijategua "kitendawili".

Pamoja na onyo hilo, Mwigulu alitumia kofia yake ya uongozi ndani ya CCM na kufanya ziara zilizoandaliwa kimkakati mwaka jana tena kwa kutumia "chopa".

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisitisha ziara za Mwigulu Januari mwaka huu na kumtaka atoe taarifa kwake (Kinana) ili kupata kibali kabla ya kufanya ziara yoyote ya chama.

Nguvu yake

Mwigulu si "king'ang'anizi" na anajifunza kutokana na makosa yake. Sifa hii ni muhimu sana. Siku za nyuma aliongoza wanaCCM na wabunge wa chama chake kushambulia na kutumia lugha chafu dhidi ya upinzani.

Mfano, aliwaita "magaidi," "wanataka kuleta ushoga" na kwamba "bajeti ya kambi ya upinzani ni ya waongoza disko." Lakini Mwigulu ninayemjadili hapa leo, ni mtu tofauti.

Hivi sasa anasimama na kujadili hoja na anatumia lugha ya staha, amekuwa kiongozi mwema kwa kuonyesha kuwa hawezi kurudia kule alikotoka. Hili ni jambo jema.

Katika Bunge Maalumu la Katiba, Mwigulu alitoa rai zipigwe hesabu kujua kama akidi ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa itatimia, vinginevyo Bunge liahirishwe kuokoa muda na fedha zinazopotea bure kwa posho.

Nguvu nyingine ya Mwigulu iko katika mitandao ya kijamii. Alipokuwa anashambulia vyama vya upinzani na watu wenye mtazamo kinzani kwa CCM, vijana wengi walimshambulia kwenye mitandao na alikuwa hapendwi. Yeye mwenyewe alilijua hilo na alipata kutamka; "najua nachukiwa sana na vijana kwa sababu ya kuitetea CCM".

Leo ukitembelea akaunti za Mwigulu na marafiki zake, unakuta maoni chanya juu yake na siku hizi kila analofanya linabandikwa mtandaoni. Nguvu hii ya mitandao si ya kudharau kwa siasa za sasa na inamwongezea safari.

Jambo la tatu linalompa nguvu ni kuaminiwa ndani ya CCM. Wana CCM na hasa viongozi wa juu wa chama hicho wanamwamini.

Moja ya mambo ambayo niliambiwa na watu wake wa karibu ni uaminifu; kwamba hapendi maisha makubwa ya kifahari na huwa tayari kuishi kulingana na mazingira yaliyopo, ndiyo maana hadi hivi leo ameendelea kupanda ngazi na kufika hapa alipo.

Kuna wakati tetesi zilienezwa kuwa nafasi aliyo nayo sasa ndani ya CCM ya Unaibu Katibu Mkuu Bara itakabidhiwa kwa John Nchimbi ili kumfanya awekeze nguvu kwenye Wizara ya Fedha.

Naona suala hilo halitatimia na Mwigulu ataendelea kuongoza chama hicho hadi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Tofauti na watu wengi wanavyomfikiria, kwa kumwona kwenye TV akipambana na wapinzani, wengi hawajui kuwa Mwigulu ni mpole, mchangamfu na anajichanganya sana na watu. Suala hili linamwongezea vigezo muhimu katika safari yake.

Mwigulu hakatai kupokea simu ya mtu hata kama haifahamu na haachi kujichanganya na vijana kila anapopata nafasi. Hili ni jambo kubwa ambalo limewashinda vijana wengi waliopewa nyadhifa kidogo tu ndani ya CCM.

Udhaifu wake

Udhaifu wake mkubwa ni mtu anayejifunza polepole mno; siyo darasani, bali katika siasa. Kwa kipindi chote tangu 2010 hadi 2013 aliendesha siasa za kimafia dhidi ya vyama vya upinzani na watu walioikosoa CCM.

Pamoja na kuwa amebadilika, amechelewa kiasi watu wengi walianza kumchukulia vibaya. Kwa sasa tunaweza kuendelea kumpima kwa sababu bado ana muda katika ofisi za umma na ikiwa ameondosha udhaifu huo tutamjua.

Udhaifu mwingine mkubwa kwake ni kuchukulia mambo kirahisi na kudhani kuwa yeye peke yake anaweza kuleta mabadiliko bila kuwashirikisha watu wengine.

Mfano mzuri ni pale Wizara ya Fedha inapofanya uamuzi fulani, Mwigulu hukimbilia kudai kuwa yeye ndiye amefanya uamuzi huo. Mwaka jana, alitangaza kuwa anapambana na "wafanyakazi hewa serikalini" na amefanikiwa kuwatokomeza kwenye malipo ya fedha za umma.

Juhudi za mapambano hayo zilifanywa na Wizara ya Fedha nzima lakini Mwigulu na marafiki zake wanataka jamii ielewe kuwa bila yeye jambo hilo lisingefanyika.

Unapokuwa unafanya uongozi na wenzako, tena uko chini ya mtu, lazima ujifunze kuwa kila linalofanyika linafanywa na timu nzima na kamwe si wewe peke yako. Kujichukulia "ujiko" huko ni moja ya udhaifu na unaweza kuwa na maana pana na "hasi" kiuongozi.

Nini kinaweza kumfanya apitishwe

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa Mwigulu anaungwa mkono nje ya CCM hivyo, ikiwa CCM inahitaji rais kijana si jambo la kupuuza.

Miaka michache iliyopita, alikuwa anachukiwa lakini amefanikiwa kubadilika kwa maneno na vitendo na kujiweka katika ngazi tofauti; sasa anaonekana kama kiongozi anayefikiri sawasawa, tena kwa kutumia akili zake.

Jambo la pili ni mtandao ndani ya chama. Mwigulu anaonekana kama kijana wa kipekee ndani ya CCM aliyejijenga na kuungwa mkono. Hii ni sababu kubwa inayoweza kumwongezea sifa za kupewa kijiti.

Jambo la tatu ni taaluma yake. Mwigulu ni msomi mzuri na aliyefuzu kwa alama za juu sana katika masomo yake ya chuo kikuu na hata sekondari. Amebobea katika masuala ya uchumi na tatizo la nchi yetu ni uchumi. CCM inaweza kumwona kama mtu muhimu katika eneo hilo.

Jambo la nne ni ujana. Sifa hii inamweka kwenye karai moja na wagombea wengine vijana na huenda isiwe na mashiko sana hadi pale itakapoonekana chama hicho kinahitaji mgombea urais kijana.

Jambo la mwisho linaloweza kumsaidia apitishwe ni kutokuishi katika makundi.

Mwigulu amekuwa kiongozi ndani ya CCM akiwa anajiweka mbali na makundi, hivyo, ikiwa CCM itahitaji mgombea asiye na makundi yenye nguvu kubwa, basi yeye pia ataingia kwenye orodha hiyo.

Nini kinaweza kumwangusha

Uzoefu ni suala zito linaloweza kumwangusha Mwigulu. Amekuwa mbunge kwa miaka mitano tu na amekuwa kiongozi wa CCM katika kipindi hicho tu na amekuwa serikalini kama Naibu Waziri kwa miaka miwili peke yake.

Huu ni uzoefu mdogo mno ukilinganisha na wakongwe lukuki waliokitumikia chama hicho kwa miongo kadhaa.

Pili, anaweza kuangushwa na maswali ya wanaomsaidia kifedha. Mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa akitumia chopa katika mikutano yake ambayo ilikuwa sehemu ya ziara binafsi.

Mwigulu anajulikana kuwa kijana wa kawaida asiye na fedha, utumiaji wa chopa kufanya ziara zenye gharama kubwa kama ilivyokuwa kinaweza kuwa kitendawili kitakachofanya ahukumiwe na vikao vya chama chake, kwamba waliokuwa wanamfadhili ni kina nani na wana malengo gani?

Ikumbukwe kuwa Mwigulu yuko kwenye kapu la wagombea walioanza kampeni mapema na kushtukiwa kabla ya kupewa karipio.

Ikiwa CCM itaweka msimamo kuwa waliocheza rafu wote wasifikiriwe, Mwigulu anaweza kuanguka kirahisi na bila kujitetea.

Dhana ya kumwandaa kwa ajili ya CCM ya miaka ijayo inaweza pia kumwangusha.

Wazee wa chama wanaweza kudai kuwa ni kijana mzuri lakini asubiri wakati zaidi upite. Moja kwa moja, sababu hii isiyo na maana yoyote kidemokrasia, inaweza kumpeleka nje ya ulingo.

Asipopitishwa (Mpango B)

Ikiwa Mwigulu hatapitishwa na CCM kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho, nadhani chaguo atakalobakia nalo ni kutumia ushawishi wake kumuunga mkono rais atakayependekezwa na chama chake.

Bila shaka, yeye atarudi kugombea ubunge jimboni kwake Iramba Magharibi na kupiga hesabu za kukwaa uwaziri kamili kwenye baraza la mawaziri litakalofuata, ikiwa CCM ndiyo itashinda uchaguzi.

Mwigulu anaonekana kuwa kijana mwenye bahati. Ukifuatilia historia yake utagundua kuwa ametoka kwenye familia ya kawaida na kwamba amefika hapo alipo kisiasa kwa juhudi kubwa alizowekeza.

Mtu wa namna hii anahitaji kuwa mtulivu kama anahitaji mafanikio ya kisiasa siku za mbele.

Hitimisho

Kwa sababu ameonyesha kuwa "anang'ara" kuliko vijana wengine wanaosaka urais ndani ya CCM, inawezekana kuwa nyota hiyo ikaendelea miaka inayokuja na siku moja "ikamtoa".

Jambo la msingi atakalopaswa kufanya ni kutokuwa na purukushani zisizo na msingi na kutorudi katika maisha ya mashambulizi ambayo aliwahi kuyafanya kipindi cha nyuma, maisha ambayo, naamini, anapoyakumbuka anajiona alikuwa "hajakua".

Nimemjadili Mwigulu mtu ninayemjua kwani ni mtu wangu wa karibu na mara nyingi huwa tunawasiliana.

Namfahamu vizuri na namwona kama kiongozi mzuri wa baadaye. Kwa sasa namwona kama mtu anayehitaji kujifunza na kufundishwa zaidi.

Kazi ya kwenda Ikulu ili kuongoza nchi inahitaji ukomavu mkubwa zaidi ya ule alionao Mwigulu, na hapa ile dhana ya "ujana" naiondoa kidogo.

Hata hivyo, Namtakia Mwigulu Nchemba safari salama katika hatua aliyofikia, kuona kama atayapata matarajio yake.
chanzo mwanchi

Naona jme umemoderate comment yangu hapo juu ukaweka unayoyaamini wewe, sasa nairudisha comment ukiharibu ndo nitakuharibia zaidi, ole wako. Hapo kwenye nyekundu "Naamini Mwigulu mwenyewe atakanusha kuwa si kweli, la sivyo tutamsaidia kukanusha hili!"
 
Back
Top Bottom