ukwelinauwazi
Member
- Nov 24, 2014
- 71
- 91
Shamba la Kitulo la Ufugaji wa Ng'ombe aina ya Mitamba lilianzishwa mwaka 1963 na Mwl.Nyerere kama eneo la kuzalisha maziwa ya kusambaza nchi nzima,Ng'ombe aina ya Mitamba wanaopatikana kwenye shamba hilo waliingizwa nchini kutokea Marekani na nchi za Ulaya Mashariki ambazo hali yake ya hewa inaendana na ile ya kitulo ambayo kuna wakati ni 0 centgrade,na hali ya juu zaidi inaweza kuwa 19 Centgrade.
Kuanzia miaka hiyo ,Shamba la kitulo ambalo linauwezo wa kulisha ng'ombe elfu nne (4000),Shamba hilo kwa sasa lina ng"ombe mia saba tu(700).
Mbali zaidi,nyenzo za kutunzia ndama na kukamua maziwa haziridhishi na ukuziaji wa nyasi zilizopandwa kwaajili ya malisho haulidhishi.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya kusikiliza na kuona changamoto zinazolikabili shamba la kitulo kwa ufugaji wa ng'ombe,Ameahidi kuhakikisha analiboresha na kusaidia upatikanaji wa ng'ombe wa kutosha,huduma za kutosha ili eneo la kitulo liwe ni shamba darasa hata kwa mashamba mengine ndani na nje ya nchi yetu.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.