Mwigulu kakamata wachina 72 wanaishi bila vibali

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza katika Mgodi wa Dhahabu wa Nyamahuna mkoani Geita na kukuta Wachina 72 kati ya 100 wakiishi na kufanya kazi bila vibali.

Akizungumza katika mgodi huo unaomilikiwa na Mtanzania, Andrew Obole, Mwigulu alisema alifika hapo kutokana na kuona taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya jamii.

Mwigulu alisema taarifa hizo zilimuonyesha Masanja Shokera akicharazwa bakora na raia wa mmoja wa China, Lee Swii, kwa madai ya kuiba mawe ya dhahabu Julai 6, mwaka huu.

“Nimefika kuthibitisha nilichokisikia kwamba kuna raia wa kigeni wanachapa watu hapa. Nimemuona mtuhumiwa wa udhalilishaji na kushangazwa na kukuta wafanyakazi wa China hapa wapatao 100 kwenye mgodi huo,” alisema.

Alisema taarifa alizonazo ambazo zipo uhamiaji zinaonyesha kuwa raia wa China waliopo mgodini hapo ni 28 ambao wana vibali halali vya kuishi nchini.

Waziri alisema kwa sababu hiyo, aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita kuwaweka chini ya ulinzi Wachina wengine 72, walinzi saba na Kaimu Meneja Uzalishaji, Richard Joachim.

“Wakati hawa wakiwa chini ya ulinzi naiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita kuchunguza uhalali wa raia hao wa China kuishi nchini bila ya kuwa na vibali.

Vilevile huyo anayeitwa Lee ambaye anatuhumiwa kumdhalilisha Mtanzania mwenzetu awekwe chini ya ulinzi na walinzi saba na kumpiga na kumjeruhi,”alisema.

Masanja Shokera ambaye anayedaiwa kudhalilishwa, , alisema siku hiyo alivamiwa na walinzi wa mgodi huo akituhumiwa kuiba mawe ya dhahabu.

Alisema walimpiga na kumfunga mikono na miguu na kuendelea kumwadhibu hali iliyosababisha apoteze fahamu.

“Walionipiga wote nawatambua, ni hawa walinzi wa Kimasai wote walinishambulia na huyu Mchina alikuja pia kunipiga wakati nimefungwa kamba… alianza huyu mkuu wa ulinzi, Sitta Dotto kuwaamrisha nikaguliwa kunipiga kichwani,” alisema.

Mkurugenzi wa mgodi huo, Andrew Obole alisema anachotambua Wachina waliopo kwake ni 28 na kwamba hao wengine alikuwa hawatambui.
 
kama hao wahamiaji haramu hawana vibali uchunguzi wa uhalali wa kuishi tz ni kupoteza muda...ingekuwa vyema Mh.Rais au waziri wa mambo ya ndani. watoe tamko la hawa wahamiaji haramu kuondoka wenyewe kwa hiari sio hadi wasubiri kufikishwa mahakamani.
 
Hivi huu umiliki wa migodi kwa watanzania ni halali kweli? au wamewekwa kama vivuli na hao wachina? ukienda hapo mgodini unakuta wachina ndio wana power kubwa kuliko mmiliki ambae ni mtanzania. Serikali iwafanyie uspy hawa wawekezaji wazawa kama kweli wanamiliki kihalali au wanatumika tu.
 
Sio wachina tu wapo baadhi ya raia wengine wa kigeni washenzi kweli kweli mfano WaGHANA na WaSOUTH Africa weupe huku huku shamba la bibi Kanda ya ziwa
 
Wapo wengi.
Njoo mererani wamejazana ,usisahau kua utapewa madini ya tanzanite ambayo yatakufanya usichukue hatua yoyote ile.
Wewe sio wa kwanza kunyamazishwa..wenzio wengi walishindwa.
Huku kupewa milioni mia tano ni kama kumsukuma mlevi
 
Huyo mwenye mgodi sijui ni Mtanzania wa wapi asie kuwa na utu wa ubinadamu naye atumbuliwe tu akanyee debe gerezani, atakuwa anajua udhalilishaji wote unaofanyika ndani ya mgodi wakesijifanye kuruka uongo Mh. Magufuli ukitoka Geita rudi dar kwenye magodauni mengi sana kunaishi wachina na wahindi wasio na vibali wanatoka ucku tu kutalii wanarudi kujifungia ndani kama kuku wakisha jua Kiswahili ndio wanatoka muda wote. Hii nchi ilishaonza baada ya kufanywa shamba la bibi, pitia upya sharia ya wafanyakazi wa kigeni kwa makampuni yote utakuta kazi zinazoweza kufanywa na wazawa wanaletwa wahindi kuzifanya, pita kariakoo wanauza mpaka karanga barabarani. Kabla hujaamia Dodoma pitia dar kuisafisha wamezidi kuwa wengi
 
Sio wachina tu wapo baadhi ya raia wengine wa kigeni washenzi kweli kweli mfano WaGHANA na WaSOUTH Africa weupe huku huku shamba la bibi Kanda ya ziwa


mkuu

kungekuwa na mfumo wa kisasa pale raia wa kigeni akiingia nchini anarekodiwa ktk compyuta na tarehe ya kuondoka... ili akiendelea kuwepo nchi ajulikane na huo mfumo, na taarifa na picha zao kutolewa kwenye vyombo vya habari kila baada ya muda fulani.

hiyo itasaidia kujua wahamiaji haramu.
na hilo ndio jukumu la uhamiaji.
 
mkuu

kungekuwa na mfumo wa kisasa pale raia wa kigeni akiingia nchini anarekodiwa ktk compyuta na tarehe ya kuondoka... ili akiendelea kuwepo nchi ajulikane na huo mfumo, na taarifa na picha zao kutolewa kwenye vyombo vya habari kila baada ya muda fulani.

hiyo itasaidia kujua wahamiaji haramu.
na hilo ndio jukuma la uhamiaji.

unadhani huo mfumo haupo? upo il uhamiaji wenyewe ndio unawapa dili unadhani watautumia kwa lolote
 
Back
Top Bottom