Mwigulu Ijumaa ijayo atavuma tena, ushauri wa kupunguza kodi ya 1% ya mishahara ya watumishi wanyonge unamkosanisha Rais na Watanzania

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Ijumaa hii mishahara mipya itatoka. Lile punguzo la kodi ya PAYE ambalo Dr. Mwigulu alimshauri mama kwa watumishi wenye mishahara midogo kwa hesabu za haraka ni punguzo la Shilingi 2,750/- (Shlingi elfu mbili, mia saba na hamsini tu). Kwa maana hiyo kila mtumishi wa Serikali na Sekta binafsi ata pokea nyongeza ya mshahara ya shilingi 2,750/- tu. Hii ni kwa mwezi, tofautisha na miamala ya kwenye simu ambayo hufanyika kwa kila siku na ni mara nyingi.

Kwa tafsiri ya haraka, nyongeza ya mshahara ya kila mfanyakazi wa Tanzania ni sawa na transaction moja ya kutuma au kutoa shilingi elfu ishirini kwenye mtandao wa simu.

Hiyo statement ya kuwa Serikali itaachia mihela haitakuja itokee kamwe. Dr. Mwigulu anafikir bado yupo zile Enzi za kusema mbovumbovu bungeni kama ilivyokuwa wakati wa JPM. Kwa sasa Bungeni hamna upinzani - kilichobaki upinzani utakuwa miongoni mwetu sisi wenyewe.

Rais Samia hawa watu hukutakiwa kwenda nao - yaani waropokajiropokaji wa awamu ya tano walitakuwa waishie kwenye awamu hiyo hiyo.

Mama ukiendelea kuwalea lea hawa watakurudia wewe mwenyewe - kwa sasa hamna upinzani mseme kuwa mtawasingizia hao ndiyo wakwamishaji wa mambo. Tumebaki sisi wenyewe CCM na lazima tupigane na kusigana wenyewe. DADEKI!
 
Hahaha! Miamala mmoja wa sh elfu 20 unakata nyongeza ya mwezi mzima ya mtumishi wa unmma!!!? Daah! Hii serikali ni katili kweli kweli!
 
Ijumaa hii mishahara mipya itatoka. Lile punguzo la kodi ya PAYE ambalo Dr. Mwigulu alimshauri mama kwa watumishi wenye mishahara midogo kwa hesabu za haraka ni punguzo la Shilingi 2,750/- (Shlingi elfu mbili, mia saba na hamsini tu). Kwa maana hiyo kila mtumishi wa Serikali na Sekta binafsi ata pokea nyongeza ya mshahara ya shilingi 2,750/- tu. Hii ni kwa mwezi, tofautisha na miamala ya kwenye simu ambayo hufanyika kwa kila siku na ni mara nyingi.

Kwa tafsiri ya haraka, nyongeza ya mshahara ya kila mfanyakazi wa Tanzania ni sawa na transaction moja ya kutuma au kutoa shilingi elfu ishirini kwenye mtandao wa simu.

Hiyo statement ya kuwa Serikali itaachia mihela haitakuja itokee kamwe. Dr. Mwigulu anafikir bado yupo zile Enzi za kusema mbovumbovu bungeni kama ilivyokuwa wakati wa JPM. Kwa sasa Bungeni hamna upinzani - kilichobaki upinzani utakuwa miongoni mwetu sisi wenyewe.

Rais Samia hawa watu hukutakiwa kwenda nao - yaani waropokajiropokaji wa awamu ya tano walitakuwa waishie kwenye awamu hiyo hiyo.

Mama ukiendelea kuwalea lea hawa watakurudia wewe mwenyewe - kwa sasa hamna upinzani mseme kuwa mtawasingizia hao ndiyo wakwamishaji wa mambo. Tumebaki sisi wenyewe CCM na lazima tupigane na kusigana wenyewe. DADEKI!
Swala la kupunguza kodi na kuongeza salary halikuwa kipaombele mwaka huu bali kupandisha madaraja na kulipa malimbikizo pamoja na ajira mpya ndio vilikuwa kipaombele.

Hiyo itatusaidia hata kwenye makato ya ATM
 
Nchi imeshavurugika, yajayo mwezi wa nane yanatisha, mwezi wa nane tozo la lakini za simu, kodi ya majengo kupitia luku,ongezeko la mshahara 2750,haya maisha wanafaid wanasiasa tu hususan wa CCM. Wabunge kupitia uchavuzi 2020,umepeleka mapunguani kuwa wabunge, haiwezekan wamepitisha mambo ya ajabu mno
 
Nchi imeshavurugika, yajayo mwezi wa nane yanatisha, mwezi wa nane tozo la laini za simu, kodi ya majengo kupitia luku,ongezeko la mshahara 2750,haya maisha wanafaid wanasiasa tu hususan wa CCM. Wabunge kupitia uchavuzi 2020,umepeleka mapunguani kuwa wabunge, haiwezekan wamepitisha mambo ya ajabu mno
 
Kwa hiyo nyongeza ya mshahara 2,750/- tozo na kodi ya kutuma mwamala mmoja wa elf 50 ni shilingi 7,250/-, duh! kweli huyu ni mchumi daraja la kwanza.
 
Kumbe ni hivyo?SIO KWELI!JAMAA YANGU MMOJA WA KUAMINIKA KANIAMBIA NIANDAE POCHI KUBWA NA WALINZI ETI MAMA ANAMWAGA MIHELA MWEZI HUU!!HEBU MTULIE!!!
 
Mimi naomba kuuliza je mapato anayolipwa mfanyakazi nje ya mshahara kama vile gratuity je yanakatwa KODI? Kama ndio asilimia ngapi?
 
1% sio kiasi hicho kiongozi, Kama CWT wananikata 2% ni 18,200 nadhani hiyo unategemea na basic yako
 
Back
Top Bottom