Mwigulu hii Tsh 70 katika Makusanyo ya Tsh 48,489,225,670 imetoka wapi wakati Siku hizi hakuna Sarafu ya Tsh 20?



Jamani hebu acheni kumsema vibaya mleta mada. Si kila mtu katika safari ya elimu alijifunza vema.

Okay, ndugu mleta uzi ni hivi. Hapa unachokizungumzia kinapatikana katika topic ya currency au money physical representation. Yaani namna kitu kinawekwa kwenye hali ya kushikika.

Pesa ni kitu chenye thamani ya kufikirika na si halisi kama vile wewe na mimi. Yaani thamani yake ni ya muda fulani tu na hivyo hata uwepo wake au uumbaji wake hutegemea uhitaji wake katika nyakati fulani tu.

Kwa mfano kuna sarafu ambazo miaka hiyo zilikuwako ila kwa sasa hazina maana wala thamani sababu muda wake wa kuhitajika umeshakwisha.

Sasa nikirejea kukujibu ni kwamba pesa ili iwe presented physically ni lazima kuwe na uhitaji wake katika mzunguko. Gharama za transactions ndizo zinaamua pesa ipi na ipi itakuwa katika mzunguko.

Tazama sasa hivi kuna mfumuko wa bei wa kiwango cha kati ambao unafanya sarafu chini ya tsh. 500 ziwe ni mzigo tu katika uchumi sababu bidhaa na huduma at minimum most of them huanzia bei ya tsh 500. Ndio maana hata ukipanda daladala ya route fupi ya shillingi 450 unajikuta haudai chenji yako ya shillingi 50 kwasababu unajua haina impact katika budget zako.

So inakuwa ngumu sana kwa serikali kuingia gharama kutengeneza kitu ambacho hakihitajiki kwenye mzunguko.

Hiyo tsh 20 ina thamani katika digital form ila sio katika physical form.
Samcezar uko sawa kwa maelezo yako ILA hilo la kuwaachia makonda hizo sh.50, 50 sikubaliani na wewe kwani ni pesa nzuri na ina faida yake ndiyo maana iko PHYSICALLY kwenye mzunguko wa fedha! Sh.50 mbili ni sh.100 na tatu ni sh.150 n.k!
 
Dah...yaani tozo tunaminywa billion 48 kwa mwezi....halafu mama na wapambe wanatumbua Billion 60 kwa wiki mbili pale hoteli ya Pierre ....kweli? ...so sad 🤭
 
Back
Top Bottom