Mwigulu, "CHADEMA" Wanaohujumu Zao la Pamba Hawa Hapa!

English Learner

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
355
355
Despite my limited time, to keep the records clear and straight this can't pass uncommented.

Wahujumu wa zao la pamba ni wabunge na wanasiasa wenye maslahi kwenye zao hili. Wabunge hawa wanatoka chama tawala na upinzani. Miongoni mwa wabunge hao ni John Cheyo, Shibuda, na Chenge. Wamo pia Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya zinazolima zao hili. Kwa ufupi wahujumu wa Pamba wamo ndani ya Serikali ya CCM na wapo pia kwenye vyama vya upinzani. Ni Wapagani, Wakristu kwa Waislamu. Hivyo hoja ya kuangusha zigo hili kwa Wapinzani tu hususani CHADEMA ni mfu.

Viongozi hawa wahujumu wanahusika katika kununua na wengine wanamiliki ginneries. Ili kuwanyonya vema wakulima wamejitanua kwenye hii sekta wakianzia kwenye usambazaji wa pembeze kwa njia ya kukopesha na mkopo hurejeshwa na mkulima kama makato wakati wa mavuno. Riba ya mikopo ya pembejeo ni aghali mno na ndiyo chanzo kikubwa cha super profit kwa dealers kwenye sekta hii. Faida ya mikopo ya pembejeo ni kubwa hata kuliko mauzo ya pamba yenyewe!

Tatizo linakuja vipi?
Serikali imepata ufadhili kuendesha Tanzania Cotton Development Programme (TCDP) inayokuza na kuendeleza zao hili. Hii programme ina promote kilimo cha mkataba na imeanzisha utaratibu unaotoa pembejeo kwa mikopo nafuu kabisa. TCDP iko chini ta Tanzania Cotton Board (TCB) ikishirikiana kwa karibu na Wizara ya Viwanda na Biashara na CoET-UDSM. Ni mradi mpana unaoboresha cotton value chain kuanzia usambazaji wa pembejeo, masoko, mpaka value addition. Interventions zinazofanyika kwenye TCDP zinawaua kabisa middle men na baadae yawezekana kukawa hakuna fursa tena ya hao intermediaries. Hapa ndipo ugomvi na fitna zinapoanzia. Kwa ufupi ni ugomvi wa kimaslahi kati ya wenye majukwaa ya kufanya maamuzi ambao wana maslahi ndani ya ugomvi wanaouanzisha dhidi ya watendaji wasio na jukwaa, wanaotekeleza makujumu yao katika kumkwamua Mkulima na kukuza pato la Taifa.

Mizengwe ya kutengeneza imekuwa mingi sana kwenye hii sekta. Yote hiyo inachochewa na akina Cheyo na genge lake. Bunge lililopita hawa wabunge haswa wa Shinyanga walimkomalia Waziri wa Kilimo mpaka ikabidi kulidanganya Bunge kwamba amemsimamisha kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba. Muda huo Waziri anatamka hayo nilikuwa na huyu M/Kiti Mwanza Deluxe Hotel tunasubiri kuingia mkutanoni. Mzee akuweza kuendelea na mkutano. Ilibidi aondoke na kesho yake alipomuomba Katibu wa Wizara ampe barua ya kusimamishwa kazi akaambiwa haipo na akamsihi atulie, aendelee kuitumikia nchi yake kwa moyo na uadilifu.

Kina Cheyo wameenda mbali zaidi na kuchonga uongozi wa vyama vya msingi na chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Pamba. Wanawatumia viongozi hawa kuanzisha fujo na kutoa matamko ya kupinga kilimo cha mkataba chini ya TCDP ili waweze kuendelea kuchuma super profit ya wao kukopesha wenyewe. Wametengeneza cartel na wanaitumia kuhujumu Bodi ya Pamba na kuwatesa wakulima; yote hayo ili kuichonganisha TCDP na Wakulima.

Zao la pamba katika nchi hii haliwezi kuinuka kama vyombo vya kutunga sera vinageuka majukwaa ya kuwaaminisha watu uongo ili kuhalalisha unyonyaji. Kila bunge linapokaa fuatilia hoja za Cheyo hasa kwenye Kilimo utauona wazi wazi ugomvi huu.

Nimesikiliza bunge, na kwa aliyesikiliza pia atakua amesikia.
Ni kwamba CHADEMA mbali na kuzuia wananchi kufanya shughuli za kimaendeleo katika majimbo wanayoyaongoza wao,kuna taarifa kwamba CHADEMA imepenyeza watu serikali ili kuhujumu nchi. Taarifa zinasema kwamba kuna barua imekamatwa iliyokua ianaenda kwa mkurugenzi wa pamba taifa ili ashushe bei ya pamba na hii ingewasaidia CHADEMA kuchukua nchi.

Pia CHADEMA imeshutumiwa kwa kumnyang'anya mbunge wao SERASINI UWAZIRI KIVULI KWA kwa kosa la kuisifia serikali.
 
Hizi porojo za nini? BARUA si ilinaswa kabisa sasa wewe unachokingia kifua hapa ni nini?
 
Ukiona mtu anatengeneza hoja isiyo kuwa na mashiko ujue kaishiwa hoja na hana lingine la kufanya zaidi ya kutunga mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu,hakuna mwananchi wa kawaida ambaye anaweza kukubaliana na hoja ya Mwigulu na anaonekana ni mtu anayetapatapa na hajui hatma yake kisiasa.
 
Hizi porojo za nini? BARUA si ilinaswa kabisa sasa wewe unachokingia kifua hapa ni nini?

Why always Mwingulu is hyping and faking people and still those contending to have "three eyes" believe wholeheartedly? Instead of using empty words, can you post that letter?
Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale iwe polisi, mahakamani bungeni hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare
 
nathamani ningekuwa gaidi wa kweli kama osama, ningelipua bunge kudadeki kupinga ubepari wa ccm .:A S-fire1::A S-fire1::A S-fire1:
 
hivi nchemba alipelekwa bungeni kwenda kuisaidia serikali kujibu hoja mbona anaingilia majukumu yasiyo kuwa ya kwake
 
Wahujumu wa zao la pamba ni wabunge na wanasiasa wenye maslahi kwenye zao hili. Wabunge hawa wanatoka chama tawala na upinzani. Miongoni mwa wabunge hao ni John Cheyo, Shibuda, na Chenge. Wamo pia Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya zinazolima zao hili. Kwa ufupi wahujumu wa Pamba wamo ndani ya Serikali ya CCM na wapo pia kwenye vyama vya upinzani. Ni Wapagani, Wakristu kwa Waislamu. Hivyo hoja ya kuangusha zigo hili kwa Wapinzani tu hususani CHADEMA ni mfu.

Huyu kwenye red hata Mtoto aliezaliwa leo anajua kwamba sio Chadema.. Ila kwa kuwa Chadema ndo wanatawala nchi hii lazima walaumiwe..
 
Kweli CCM imekwisha kabisa na haina hoja yoyote, embu angalia historia ya uzushi wao;

1/Migomo ya wanavyuo imeanzishwa na CHADEMA.

2/Migomo ya Waalimu na madaktari ni mipango ya CHADEMA.

3/Daudi Mwangosi alitumwa na CHADEMA ajitoe muhanga kwa kujilipua bomu ili aue askari, baadaye hadithi ikabadilika na kuwa Mwangosi ameuwawa na wafuasi wa CHADEMA!!

4/Dr.Ulimboka alitumwa na CHADEMA na waliomtesa ni wafuasi wa CHADEMA.

5/Kubanda aliteswa na wafuasi wa CHADEMA.

6/Fujo na Maandamano ya wananchi wa Mtwara yalikuwa yakipangwa na CHADEMA.

7/Kufeli kwa wanafunzi wengi wa kidato cha nne ni mipango na mikakati ya CHADEMA!!

8/Kudorora kwa kilimo cha Pamba ni mikakati ya CHADEMA!!!
 
Hizi porojo za nini? BARUA si ilinaswa kabisa sasa wewe unachokingia kifua hapa ni nini?

hivi umesha maliza mitihani kijana?
hivi unaongelea barua imenaswa na unasema hipo wakati hakuna hiyo barua hapa, hivi ndivyo unavyo jibu maswali tena juujuu tu.
 
Mhujumu mwingine wa wakulima na kilimo cha pamba ni mbunge wa Nzega(ccm) Ndugu Hamisi Kigwangala ambaye aliwadhulumu wakulima wa pamba mamilioni ya fedha za stimulus package.

Sasa ikitokea mwendawazimu akasema kuwa Chadema ndiyo inahujumu zao la pamba wenye akili timamu tunang'amua mapema kuwa hizo ni sanaa tu baada ya serikali kushindwa kuwajibika kwa wakulima na kilimo nchini hasa wakulima wa pamba.
 
hivi nchemba alipelekwa bungeni kwenda kuisaidia serikali kujibu hoja mbona anaingilia majukumu yasiyo kuwa ya kwake

Kwani anajitambua? Mtumasiyejitambua hawezi kuwa na mipaka ya wajibu na uwajibikaji.
 
hawa cdm kwa ulafi wa madaraka wanaweza fanya hv, ili serikali ichukiwe but tushaanza kusoma mchezo wao. Kura zitaongea mbili kumi na tano na si wingi wa watu kwenye mikutano.
 
hivi nchemba alipelekwa bungeni kwenda kuisaidia serikali kujibu hoja mbona anaingilia majukumu yasiyo kuwa ya kwake

Ni na naibu katibu mkuu wa chama chetu cha zamani kwa hiyo ana majukumu mengi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom