Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,001
- 9,866
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kutodai kumbukumbu za miaka mingi iliyopita huwa ni kero kwa wafanyabiashara
Amesema kawaida wafanyabiashara wakishamalizana na serikali hawana utaratibu wa kutunza kumbukumbu bali huwekeza nguvu nyingi katika kukuza biashara. Hivyo si sahihi kuomba kumbukumbu za miaka hiyo
Aidha, watanzania hawana kawaida ya kutunza kumbukumbu, suala hilo ndio limewaingiza wengi kwenye hatia ya kudaiwa kodi kubwa. Ametolea mfano kwa kuwaambia waandishi kama kuna yeyote kati yao mwenye ‘salary slip’ ya 2005
Amewataka wazingatie weledi katika kukusanya kodi kama alivyoagiza Rais Samia katika hotuba yake alipokuwa amewaapisha mawaziri na manaibu waziri Ikulu Dodoma