Mwigulu awapa bodaboda siku 30 kila mmoja awe na kofia ngumu 2

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
229
485
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 30 kwa wamiliki na madereva wa bodaboda nchini kote kuhakikisha wanakuwa na kofi a ngumu (helmet) mbili ili kuwezesha dereva na abiria kupunguza madhara ajali inapotokea.

Amesema baada ya siku hizo kuisha, dereva yeyote wa bodaboda au abiria atakayekaidi agizo hilo atakamatwa na kutozwa faini. Waziri Nchemba aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa kikao cha utoaji elimu kwa waendesha bodaboda, ambao wamelalamikiwa kutojua sheria ya usalama wa barabarani na wengine kuendesha bila kuwa na elimu yoyote ya udereva.

Nchemba alisema kuwa siku 30 zinatosha kwa wamiliki wa bodaboda na madereva wake kwa nchi nzima, kujiandaa kuhakikisha wanakuwa na kofia ngumu mbili ambazo watavaa moja abiria na nyingine dereva ili kupunguza madhara ya ajali kwani vijana wengi wanapoteza maisha na kuathiri nguvu kazi.

Alisema abiria atakayekaidi kuvaa kofia ngumu, ashushwe na dereva aliyetii aachwe aendelee na safari, kwa vile wapo abiria hasa wanawake wamekuwa na tabia ya kukataa kuvaa kofia hizo kwa madai kuwa wataharibu nywele zao, walizozitengeneza kwa gharama kubwa saluni. Waziri huyo alisema kuwa vituo vya polisi, vingi vimekuwa na bodaboda na baiskeli nyingi zilizokamatwa.

Kwamba hatua hiyo haina faida yoyote kwa jeshi la polisi, kwa vile wanakuwa hawajatimiza lengo na hivyo dawa ni kutoa elimu ya kutosha juu ya usalama wa barabarani ili waweze kupunguza ajali zisizo za lazima.

Alilitaka Jeshi la Polisi nchini kote kukaa na madereva hao wa bodaboda na kuwapa elimu, akisema katika mwaka wa 2016/2017 zaidi ya vifo 3,000 vilitokea katika ajali zaidi ya 7,000, nyingi zikiwa zinatokana na uzembe wa madereva bodaboda kwa kuendesha mwendokasi huku wakiwa wamelewa na ukaaji mbaya wa abiria .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack alisema baadhi ya madereva hawajui sheria za usalama barabarani na ndio maana wamekuwa wakiruhusu abiria wao kukaa vibaya na kuhatarisha maisha yao.

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele alisema misuguano mingi ya madereva wa bodaboda na baadhi ya askari polisi ni kwa askari hao kutumia nguvu kubwa wanapotaka kuwakamata badala ya kutoa elimu.
 
Kwenye matukio muhimu kama IMMA Advocates kushambuliwa huwa jamaa anazama chini ya meza. Sijui nini kimemkumba huyu Mchumi grade one?Hiyo Wizara bora apewe Sirro tu.
 
Back
Top Bottom