Mwigulu atolewe Uwaziri, apokee kijiti cha Polepole kuwa Katibu Mwenezi

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Akiwa kama Waziri wa fedha ana majukumu mazito ya kumsaidia Rais kukuza uchumi wetu na kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja. Ni wazi uchumi wetu umedorora na unahitaji juhudi kubwa sana huku mambo mengi yakitukabili, kuna wastaafu, watumishi wanataraji nyongeza mishahara, miradi mikubwa inahitaji pesa, bado pesa za maendeleo n.k lakini Mh anaonekana anapenda 'headlines' kwa kurumbana na kubishana na wanasiasa kuliko jukumu zito alilopewa. Mabishano na vijembe waachie wakina Kibajaji, Msukuma na wengine wasio na majukumu makubwa.

Tunategema ukisimama uongee masuala ya mapato, kutanua wigo wa walipa kodi, uzungumzie mafao ya wastaafu na mambo mengine ya msingi na sio kusimama na kutokea 'fenti fodi' unamjibu Mbowe.

Nadhani Mama atagundua moja ya watu ameshakosea kuwa naye ni wewe, na atakuwa ameona nafasi ya Uenezi wa Chama ndio inakufaa zaidi kuliko Uwaziri wa Fedha na Mipango
 
Huyo Rais wa mawe hafit popote! Nashangaa kwanini wanampa wizara nyeti na kubwa kama wizara ya fedha! Mama anapaswa kutazama upya Hii nafasi
 
Mh. Mwigulu, acha Siasa chafu..jikite kwenye TRA NA UCHUMI

ukishindwa kuongeza wigo wa Kodi, utatymbuliwa. Huyu Rais hataki kusifiwa sifiwa.

Mwigulu, utaulizwa umeongeza walipa Kodi wangapi wapya

Je, utaulizwa Kampuni ngapi zimekuja
 
Mh. Mwigulu, acha Siasa chafu..jikite kwenye TRA NA UCHUMI

ukishindwa kuongeza wigo wa Kodi, utatymbuliwa. Huyu Rais hataki kusifiwa sifiwa.

Mwigulu, utaulizwa umeongeza walipa Kodi wangapi wapya

Je, utaulizwa Kampuni ngapi zimekuja
Anadhani Mama na yeye anapenda mapambio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom