Mwigulu asisitiza mshikamano ndani ya CCM

BONGE BONGE

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
3,721
2,106
Akiongea kwa upole na sauti ya unyenyekevu mkubwa na wananchi wa Ndago na vijiji vya jirani kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi-CCM (Bara), Mh. Mwigulu Nchemba (Mb) pamoja na mambo mengine alitumia muda wake alipopanda jukwaani kusisitiza mshikamano ndani ya Chama cha Mapinduzi-CCM.

Wakati Nchemba akisisitiza mshikamano Mbunge wa Jimbo la Mtera na rafiki yake mkubwa Mh. Livingstone Lusinde (aka Msumari wa Moto) aliyeambatana na Mh. Mwigulu aliwataka wananchi wa Iramba kutoipoteza lulu yao (Nchemba) kwa sababu ni zawadi kutoka kwa Mungu, wakati Mwigulu amejikita kutoa misaada kwenye mashule na taasisi mbalimbali, alikemea watu wanaobeza juhudi hizo ili hali wao wanawajengea wananchi vilabu vya pombe.

Source, mimi mwenyewe
 
Wanasias wetu wao ni maajabu tu! Badala kukomaa na serikali yao itekeleze ilani na kuwakomboa wananchi wao wamekazana na mishikamano ndani yao!!!
 
Wanasias wetu wao ni maajabu tu! Badala kukomaa na serikali yao itekeleze ilani na kuwakomboa wananchi wao wamekazana na mishikamano ndani yao!!!

Wewe unaishi dunia gani? Ilani imekamilika kwa zaidi ya asilimia 65 katika miaka miwili.
 
Wanasias wetu wao ni maajabu tu! Badala kukomaa na serikali yao itekeleze ilani na kuwakomboa wananchi wao wamekazana na mishikamano ndani yao!!!
............kaka kumbuka CCM ndicho chama kilichoshika Dola na kinaisimamia serikali katika kutekeleza majumuku ya kila siku kupitia ilani yake, ccm ikiyumba, serikali itayumba pia (kwa lugha rahisi haitakuwa imara)
 
............kaka kumbuka CCM cdicho chama kilichoshika Dola na kinaisimamia serikali katika kutekeleza majumuku ya kila siku kupitia ilani yake, ccm ikiyumba, serikali itayumba pia (kwa lugha rahisi haitakuwa imara)

Natumaini ripoti ya World Bank umeiona mkuu! Haya mambo ya kushangilia kujenga bara bara tukaita serikali inafanya kazi inabidi yaishe. Maana tunalipa kodi in return of huduma za jamii kuboreshwa! Kwa hiyo wananchi tu-deserve kupata barabara bora na afya bora!!

Serikali inapaswa kuhangauka issues, like kutengeneza mazingira ya uchumi imara, kazi kwa wananchi, mfumo mzuri wa afya, kusomesha wananchi wake, to name few!!

Sasa hizo kazi huwa zinafanywa saa ngapi kaka?
 
Wewe unaishi dunia gani? Ilani imekamilika kwa zaidi ya asilimia 65 katika miaka miwili.

kaka ilani imekamilka vip? wakati maisha yanazidi kuwa magumu kila siku kuanzia bei ya vyakula, petrol shida au kwa sababu nyie mnapata mafuta bure mnaona imekamilika so kaangalie wananchi wa vijijini kama imekamilika then uongee....ushabiki mbaya sana kaka....:A S-baby:
 
hakuna jipya. inasikitisha sana. yaani unazunguka nchi nzima unazungumzia mshikamano leo? tanzania inamatatizo yanayohitaji viongozi wenye utashi wa kuyatatua na si kuomba mshikamano kwani bado hauwasaidii wananchi hata kidogo. hebu viongozi wetu mnaopewa dhamana ya uongozi jaribuni kujifunza dhana kamili ya uongozi kwa maana pana zaidi na kuwaongoza watz katika haki, kweli, sheria bila upendeleo na ushirikishi wa pamoja kwa uwazi katika kupanga, kusimamia, kutekeleza na kupitia upya mara kwa mara miradi ya maendeleo ya jamii husika. iwe ni ya elimu, afya, uchukuzi, maji na uzalishaji mali kwa kutumia rasilimali tulizonazo kwa faida ya watz. tuache siasa za zamani.
 
Wewe unaishi dunia gani? Ilani imekamilika kwa zaidi ya asilimia 65 katika miaka miwili.

CCM acheni kujitekenya then mnacheka wenyewe, so acheni kupoteza muda kujidanganya eti 65% ilani yenu imetimizwa kwani huo ni uongo na kujirisha upepo koz huku mtaani maisha magumu.
 
Akiongea kwa upole na sauti ya unyenyekevu mkubwa na wananchi wa Ndago na vijiji vya jirani kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi-CCM (Bara), Mh. Mwigulu Nchemba (Mb) pamoja na mambo mengine alitumia muda wake alipopanda jukwaani kusisitiza mshikamano ndani ya Chama cha Mapinduzi-CCM; Wakati Nchemba akisisitiza mshikamano Mbunge wa Jimbo la Mtera na rafiki yake mkubwa Mh. Livingstone Lusinde (aka Msumari wa Moto) aliyeambatana na Mh. Mwigulu aliwataka wananchi wa Iramba kutoipoteza lulu yao (Nchemba) kwa sababu ni zawadi kutoka kwa Mungu, wakati Mwigulu amejikita kutoa misaada kwenye mashule na taasisi mbalimbali, alikemea watu wanaobeza juhudi hizo ili hali wao wanawajengea wananchi vilabu vya pombe.

Source, mimi mwenyewe

Tunachohitaji kutoka kwa viongozi ni Maendeleo na sio fadhila za vimsaada ambavyo tunajua ni tone tu la Pesa na rasilimali wanazotufisadi!
 
Wewe unaishi dunia gani? Ilani imekamilika kwa zaidi ya asilimia 65 katika miaka miwili.
Ilani ipi hiyo mkuu?

Maisha bora hakuna, mfumuko wa bei unatisha, umaskini unakithiri na mkwele kashasema hajui hata chanzo chake, Ajira ni bomu linangoja kulipuka, Rushwa imetapakaa mpaka ndani ya uongozi wa juu wa CCM.....
 
ipo siku ccm watasema wanampango wa kumwita yesu,na wafuasi wake wakakubali kabisa,huyo bwana hayana mvuto kabisa,tuulizeni sisi tunaye soma hapa dodoma kwa mambo anayofanya,eti aongea kwa unyenyekevu ndago,aliposababisha mauaji ndago,sitamsahau huyo kwa mambo ayafanyayo hapa dodoma,anguko lake ni 2015.
 
Wewe unaishi dunia gani? Ilani imekamilika kwa zaidi ya asilimia 65 katika miaka miwili.
Na hizi ahadi za JK?

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Mtu wa Shamba huyu hana ahadi kwa Kilimnajaro na Iringa, na mikoa mingine mingi tuu.
Pamoja na kutoa luluki la haadi bado kakosa kwa baadhi ya mikoa muhimu.
Mbaya ahadi zote zilikuwa out of desperation baada ya kubaki yeye, Kinana mama na mtoto.
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom