Mwigulu ashutumiwa kwa kuleta mkanganyiko Arumeru - Apendekeza Jina la 1 hadi 4 yakatwe

kama kweli ni wewe,tunakuribisha kwa mikono miwili.tunakuomba uwe mvumilivu kwa maswali utakayo ulizwa.usije ukaropoka vijimatusi mlivyozoea,ukalimwa ban kabla hatujakukimbiza kwa hoja makini.karibu
 
Karibu Jamvini kama ndo wewe..kwa kale kamchezo ka Igunga nadhani wanaJF wote wanatahadhali ya kutosha!
Tunaomba Arumeru endesheni siasa za kistaarabu,watu wamekusifu sana hapa jamvini kuwa una brain kali,sasa itumies kudisplay high intellectual maturity,Tanzania ni nyetu sote.
Acha kujipendekeza watu wepi....wamemsifu.
 
Mwigulu amependekeza vipi Sioi akatwe jamani? Utaratibu wa maamuzi ya chama unafanywa kwa vikao, na Mwigulu si mjumbe wa vikao vya huko Arusha na wala hana mandate ya kuamuru nani akatwe na nani asikatwe...tusubirini vikao vya juu viamue nani atatayetuwakilisha huko, sisi tutaenda kumnadi tu! Obviously, kuna watu wanamuogopa Mwigulu (Jembe la ukweli kutoka Iramba Magharibi) na kwa vyovyote vile akipewa jukumu hilo atawasumbua sana tu maana hana papara na anaweza mikiki mikiki ya siasa za sasa...

jembe la kuchukua wake za watu.what do you mean kigwangala,usituletee cheap politics hapa.tena ww usiseme kabisaa,juzi ulitaka kuwaiga wabunge wa upinzani kutetea wananchi.ukasemwa ukafyata kama vile haupo.hadi leo upo kimya.you are good for nothing kigwangala.
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.

Hongera kwa kuingia JF, karibu sana!!
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.

Lakini unatamani uwe wewe na ulivyo muhuni wazee wa huko watakumaliza kabisa wewe peleka hizo pesa uwahonge wake zao uone usifikiri kule ni Igunga mbona hujibu tuhuma za Igunga mkeo anajua?
 
Mwigulu amependekeza vipi Sioi akatwe jamani? Utaratibu wa maamuzi ya chama unafanywa kwa vikao, na Mwigulu si mjumbe wa vikao vya huko Arusha na wala hana mandate ya kuamuru nani akatwe na nani asikatwe...tusubirini vikao vya juu viamue nani atatayetuwakilisha huko, sisi tutaenda kumnadi tu! Obviously, kuna watu wanamuogopa Mwigulu (Jembe la ukweli kutoka Iramba Magharibi) na kwa vyovyote vile akipewa jukumu hilo atawasumbua sana tu maana hana papara na anaweza mikiki mikiki ya siasa za sasa...
Ngoja tumwambie Beatrice Shelukindo upo huku JF akuibukie ili huku nako upotee ingawa tunatamani uzidi kuwepo.
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.
Hujajibu hoja: ulikwenda Arumeru kama nani na kufanya nini? Kuwa makini kijana...
 
nimemuona mwigulu hapa jf...kwa kuwa amejiunga hapa basi ajue kiburi chake hakihitajiki humu ndani
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake
Mwigulu heshima yako,

Huwa naheshimu sana mtu mwenye msimamo kama kweli ulifanya utafiti na kuona fulani hauziki ni jambo la busara sana kuwa muwazi na kusimamia ulichokiona, utaheshimika na chama na jamii kwa ujumla. Ukianza kuruka sasa na endapo mambo yakaharibika au kuwa mazuri hatutakubali utetezi wako mwingine.

Juzi kwenye post zako za mwanzo ulisema kabla ya kuingia kwenye kampeni ni vizuri kufanya research na ukasema uko Tengeru kwa ajili hiyo, ulipoulizwa unaonaje tetesi za rushwa ndani ya CCM ukasema katika kufanya utafiti wako lazima vijana unaowatuma (Toyo) uwape pesa kwa vile jioni lazima wapeleke hesabu, sasa unapokataa kuwa si wewe uliyeshauri Sioi au wagombea no. 1-4 watoswe unanishangaza kidogo. Au hiyo ID Mwi gulu si yule Mwigulu tunayemjua?
 
Luhwege unataka majibu gani ya igunga mbona hayo yalitolewa maelezo jana? Unaonekana ni mwana JF wa msimu. Soma thread ya jana kiongozi alitolea majibu yote hayo na kama hujaridhika uulize. We are fed up na lugha hiyo ya wake za watu, hivi hata kama ni kweli hivi alibaka? Kama kuna hoja great thinkers ijadiliwe iliyo. Nayo kama ni hoja ajitokeze mme au shuhuda aliyefumania na kuliko kutembelea habari za kusikia. Crucial man comment zako masaburi kwelikweli. Mwigulu big up kwa kujitokeza jana na pia nimefurahishwa na maelezo yako.
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.
Vipi mheshimiwa na ile tabia yako ya kumendea wake za makada wa chama chako kwa kisingizio cha kampeni umeachana nayo? Kama utaiendeleza Arumeru, ni bora ukatayarisha sanda yako kabisa ya kukuzikia.
 
Ndg wana JF. Kwanza naomba niweke wazi kuwa mtu kuongoza kampen anateuliwa na cc na kupitishwa na nec. Hilo lilifanyika na kwa taarifa tu kuongozakampeni sio starehe na sio jambo la kuombea. Hivyo mimi ningetamani kikombe hicho kipitie mbali ila ninapotumwa nakwenda. Pia anayedhani nina printing kariakoo namruhusu aichukue iwe yake kuanzia leo.

ole wako na huko arumeru uchukue wake za watu......utanyongwa kwa kutumia ile skafu yako unayovaa shingoni
 
Mwigulu amependekeza vipi Sioi akatwe jamani? Utaratibu wa maamuzi ya chama unafanywa kwa vikao, na Mwigulu si mjumbe wa vikao vya huko Arusha na wala hana mandate ya kuamuru nani akatwe na nani asikatwe...tusubirini vikao vya juu viamue nani atatayetuwakilisha huko, sisi tutaenda kumnadi tu! Obviously, kuna watu wanamuogopa Mwigulu (Jembe la ukweli kutoka Iramba Magharibi) na kwa vyovyote vile akipewa jukumu hilo atawasumbua sana tu maana hana papara na anaweza mikiki mikiki ya siasa za sasa...
Msije baadae mkakana kwamba huwa humuingiagi JF na wala hamuitambui. Maana alianza ndugu yako Nape na tunategemea ndivyo itakavyokuwa kwako bwana Said Bagaile.
 
Mwigulu amependekeza vipi Sioi akatwe jamani? Utaratibu wa maamuzi ya chama unafanywa kwa vikao, na Mwigulu si mjumbe wa vikao vya huko Arusha na wala hana mandate ya kuamuru nani akatwe na nani asikatwe...tusubirini vikao vya juu viamue nani atatayetuwakilisha huko, sisi tutaenda kumnadi tu! Obviously, kuna watu wanamuogopa Mwigulu (Jembe la ukweli kutoka Iramba Magharibi) na kwa vyovyote vile akipewa jukumu hilo atawasumbua sana tu maana hana papara na anaweza mikiki mikiki ya siasa za sasa...
Mkuu Kigwangalla, kwanza habari yako vipi na wewe uko kwenye list ya madame ya kuachia ubunge?

Tuachane hayo, Mwigulu ndiye aliyepewa jukumu la kutafiti upepo wa wapiga kura Arumeru Mashariki na amekuwa kule kwa kipindi kirefu sasa, kwa maana hiyo ndiye aliyetegemewa kutoa ripoti ya mapendekezo kuhusu nani anakubalika kati ya wagombea 6. Tunaposema ni yeye ameshauri Sioi akatwe si kwamba tunatunga iko wazi na kila mtu anajua. A simple logic, hivi akishauri Sioi akatwe na Sarakikya akashinda atakataa kuwa yeye hakupendekeza.
 
Kujiunga kwa Mwigulu hapa ndani ya JF na hivyo kuleta wabunge wengi zaidi ni dalili nzuri sana na kwa mbaali mwanga wa mabadiliko unaanza.

Nafikiri wengi mnakumbuka miaka kadhaa watu walitishiwa kufukuzwa kazi kwa kusoma JF ila sasa naona imeshakuwa historia kwani viongozi vijana (bila kujali wapo upande gani) wameanza kuingia hapa moja kwa moja kwa majina yao.

PJ, muache kwanza mgeni basi azowee maana hayo maswali yatakuja baadaye. Mwigulu Nchemba, karibu sana.

Kujiunga kwao inawezekana pia ukawa ni mkakati wa kuiweka sawa JF na kuiondoa kwenye mrengo wa chama fulani.
 
Uwepo wake hapa JF nadhami sasa tutapata ufafanuzi wa kilichojili Igunga!
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake

mkuu mwigulu nchemba madelu karibu sana hapa jukwaani.

tunakuomba ujitokeze mara kwa mara kujibu hoja mbalimbali zinazokihusu chama na hata mwenyekiti wa taifa kikwete kama ulivojiteza hapa kwenye hili linalokuhusu.

hili ni jukwaa huru pia waambie na viongozi wenzako hasa vijana na waingie kwa majina yao halisi wakisaidie chama,acheni kulala.

otherwise nikutakie uchaguzi mwema huko arumeru
 
Kiongozi big up kwa ufafanuzi. Watu wengine wa ajabu sana sijui ni chuki binafsi? JF inasomwa na wengi na kuaminiwa mtu unapoandika kitu cha kizushi huwatendei haki wanaotegemea JF kama chanzo cha kuaminika. Mwigulu is not such a cheap person na infact ndiye pekee so far hajakumbwa na kansa ya makundi. Kama kijana mwenetu bila kujali itikadi nampongeza kwa kuwa independent in thinking, keep it up. Wanaokupakazia wataendelea kuumbuka kama huyu ndugu yetu mwenye chuki binfsi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom