Mwigulu ashutumiwa kwa kuleta mkanganyiko Arumeru - Apendekeza Jina la 1 hadi 4 yakatwe

UTANIPENDA

Member
Feb 25, 2012
31
12
Kumezuka mgogoro ndani ya UVCCM arusha kuwa mhe mwigulu nchemba amekuwa akifanya ziara arumeru mashariki ambayo haikuwa na baraka za chama. Mmoja ya vigogo wa UVCCM mkoa wa arusha amesema huyu mbunge anataka kulazimishia apewe umeneja wa kampeni kitu ambacho UVCCM arusha wamesema wao wamejiandaa na wameandaa pendekezo la jina la meneja wa kampeni za arumeru ambaye atatoka arusha.

UVCCM kupitia mwenyekiti wake James Ole Millya wameendelea kushikilia msimamo wao kuwa mgombea aliyepitishwa jina lake lisikatwe na kuwa wao wako tayari kufanya kampeni za ushindi.

Source: Arusha
 
Ila kule kuna genge la wazee wa kishiri sijui...ala ala na wake za watu,wataua mtu.
Ishu ya washili karibu inafikia mwisho sijui kama Sarakikya ni mshili, kama si mshili wale wazee waliosingiziwa kuua itabidi waombwe radhi kwanza kwa kusingiziwa pili kwa kuwaondolea mtoto wao Sioi, kuhusu Mwigulu hatakiwi na vijana kwa vile yeye ndiye kapendekeza Sioi apigwe chini, ngoja tuone sinema inakoelekea.
 
Kikao cha CC kinachoendelea kinasemekana kitakuwa kugumu kutokana na taarifa ya mwigulu nchemba aliyoiwasilisha kwa CC kuleta mkanganyiko.

Taarifa hiyo inapendekeza kuwa ili kuondoa makundi yanayoonekana kushamiri sasa majina ya wagombea namba MOJA hadi NNE yakatwe na majina ya namba TANO na SITA yafanyiwe maamuzi ya mmoja wao kupitishwa. Mkanganyiko katika jambo hili unakujwa pale ambapp mgombea namba TANO Antony Musani ameshajitoa CCM na kwenda CHADEMA ambako nako amechukua fomu ya kugombea ubunge. Mgombea namba SITA URIO aliyepata kura 11 yeye alishachoka katika hatua za awali na kuwa alishatangaza kujitoa kwenye mchakato.

Habari zinasema UVCCM arusha wamekasirishwa na taarifa hiyo ambayo wameilalamikia inajadiliwa kwa sababu zipi wakati ujio wake na ziara yake arumeru haukuwa wa kutumwa na CC ili kutoa mapendekezo.
 
Enzi za miaka ya 90 kulikuwa na kipindi ITV cha Hawavumi lakini wamo, tutajuaje yupo kama hafanyi haya ya kuchonganisha?
 
Bw feedbak kile kipindi kimereje,huyu migulu baja anajipendekeza na hapo anataka kumbeba Kaaya wa AICC
 
Yote haya yanatokea kwa sababu chama kimekumbatia rushwa kama njia sahihi ya kupata wagombea! Ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe! acha wachanganyane!!
 
Kinachofanyika kwa sasa ni kujitahidi kwa kila hali kuwatangaza wagombea wa vyama kabla ya kampeni.Hizi zingine ni stories tu zinatengenezwa ili kuwafanya wadanganyika wawaongelee sana as a result kufahamika na kusikika kabla ya kampeni.Good technic by the way....!
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake
Kwanza karibu jamvini, pili usisahau kutupa Breaking news Immediately mtakapopitisha jina la mgombea wa CCM. yote ni hapa hapa JF.
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake

Pole kama unasingiziwe kiongozi........watu wengine wazushi
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake
Karibu. Tunasubiri maamuzi ya kikao. Pamoja na hayo hujasikia fukuto lolote huko UVCCM pamoja na huyo Msami kukimbilia CDM?
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake
Ile skafu unavaa shingoni kwa maana gani?..Unaipenda sana Tanzania?....Mbona unakaa meza moja na mafisadi?
 
Wana Jf salam. Naomba kuweka wazi kuwa kika cha cc kufuatana na ratiba kitafayika saa nane hivyo bado hakijafanyika na pia mimi sina report yeyote cos nilifungua kikao tu sikuendesha zoezi hilo. Anayesema hayo ana lengo lake
Hee! kumbe na wewe umeshajiunga na jamvi letu!!!?
Mkuu,karibu sana JF. Pia nina swali moja kwako na nitafurahi kama utanijibu kwa faida ya wanaJF wote.
Kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki, Je,unafikiri mgombea wa chama chako(ccm) anaweza kuibuka mshindi Arumeru?
 
Kanyaga huku meru tartiibu mwigulu,huku jamaaa hawana simile,mapanga shabab...by tha way ccm mnajisumbua pale
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom