Mwigulu apongezwa Iramba, achinjiwa maksai Mwekundu, licha la kulalamikiwa miamala!

Lyambalyetu

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
261
235
Weekend hii Dr. Mwigulu amekumbuka kwenda kutoa shukrani jimboni kwake na kama kawaida kaendelea kuongea misamiati ya KiNyiramba huku akiwaona wasikilizaji wake kama hawana uelewa wowote ule.

Pamoja na kukwepa kugusia mambo ya kodi ya miamala lakini agenda kubwa ilikuwa ni kujiimarisha jimboni kwa kuongea hadaa nyingi za kujionesha yeye ndiye kila kitu jimboni wakati kwa miaka yake hii 11 hamna jambo amelifanya jimboni hata Taifani linalompa sifa kuwa yeye ni kiongozi mzuri.

Dr. Mwigulu uzuri wake ni ule wa kujibizana mitandaoni na kutetea hoja zisizo za maana ili kujikomba kwa viongozi. Hili,linaanza kuonekana vema baada ya kuonekana mapungufu makubwa yaliyopo katika Bajeti ya Mwaka huu ambayo inasmekana bajeti ya kujenga barabara ni shilingi milioni 500 tu.

Pamoja na kuanza ukwepa kujiita mamba aliyepo kwenye kina kirefu Dr. Mwigulu ameonge maneno mengi yanayoashiria kutamani kuongoza jimbo kwa miaka 20 ijayo. Hii ni pamoja na kuanzisha mkakati wa kuhamisha makao makuu ya Wilaya kutoka Kiomboi na kuyaleta mahali alipojenga nyumba yake barabara ya kuelekea Shinyanga na Tabora.
 
Hela zake akanunua ng'ombe na kulipa wachinjaji na kununua vinywaji sasa kwa nini usisifie ili hali nawe umepewa hela.
 
Huwa Siangalii nani amefanya bali nini kafanya...., Yaani hiki alichokifanya huyu Bwana hata angekifanya Cleopatra au Mfalme Suleiman bado ningemwambia hapa kwakweli sio sahihi...
 
Hiyo alikwenda Kwa yule mganga wake kurekebisha mambo baada ya kuboronga kwenye tozo za miamala! Kwa uchawi wa mamamganga yule Madame president atambakiza TU ofisini bila kumtumbua!

Ni suala la muda tu, madelu ataendelea kula kiyoyozi bila hofu Kwa msaada wa mganga wake!
 
Inaweza ikawa kweli eee?
 
Weekend hii Dr. Mwigulu amekumbuka kwenda kutoa shukrani jimboni kwake na kama kawaida kaendelea kuongea misamiati ya KiNyiramba huku akiwaona wasikilizaji wake kama hawana uelewa wowote ule.

Pamoja na kukwepa kugusia mambo ya kodi ya miamala lakini agenda kubwa ilikuwa ni kujiimarisha jimboni kwa kuongea hadaa nyingi za kujionesha yeye ndiye kila kitu jimboni wakati kwa miaka yake hii 11 hamna jambo amelifanya jimboni hata Taifani linalompa sifa kuwa yeye ni kiongozi mzuri.

Dr. Mwigulu uzuri wake ni ule wa kujibizana mitandaoni na kutetea hoja zisizo za maana ili kujikomba kwa viongozi. Hili,linaanza kuonekana vema baada ya kuonekana mapungufu makubwa yaliyopo katika Bajeti ya Mwaka huu ambayo inasmekana bajeti ya kujenga barabara ni shilingi milioni 500 tu.

Pamoja na kuanza ukwepa kujiita mamba aliyepo kwenye kina kirefu Dr. Mwigulu ameonge maneno mengi yanayoashiria kutamani kuongoza jimbo kwa miaka 20 ijayo. Hii ni pamoja na kuanzisha mkakati wa kuhamisha makao makuu ya Wilaya kutoka Kiomboi na kuyaleta mahali alipojenga nyumba yake barabara ya kuelekea Shinyanga na Tabora.

Ukila Maksai hata uwe na PhD, kichwani ni patupu​

Nilifikiri hii thread ni ya uzushi kumbe ni kweli Dr. Mwigulu Nchemba alienda kufanya sherehe kwao - wakala na kusaza. Kuna clip inatembea ikionesha tukio hilo! Sijui namna ya ku-upload hapa, ningewawekea!
 
Back
Top Bottom