Mwigulu anusurika, apotea angani saa sita

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,338
Ni jana muhezaTanga, kwenye ziara yake ya chama/serikari.

Baada ya dereva wa chopa aliokodi kutoona pakutua, Tanga ni shideee, lakini story hii imefichwa sana na vyombo vingine, more story nipashe front page.

Mwigulu anusurika, apotea angani saa sita

18th January 2015

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amenusurika kifo, baada ya kupotea angani kwa saa sita akiwa ndani ya helikopta iliyokuwa inazunguka sehemu mbalimbali mkoani Tanga.

Ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano na waongoza ndege, inayotumika katika mikutano yake kwa vile pamoja na uwaziri ni Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.
Tukio hilo lilitokea jana wakati anatoka Kilindi kwenda wilayani Muheza, kwa ajili ya mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike kwenye uwanja wa Orofea.

Kiongozi huyo kabla ya kupata mkasa huo, alihutubia mkutano wa hadhara na alipomaliza alianza safari kuelekea wilaya za Pangani, Mkinga na Muheza kwa ajili ya mikutano.

Nchemba alisema kuwa wakati anatoka Kilindi alipoteza mawasiliano na kulazimika kuzunguka angani zaidi ya saa sita.

Baadaye rubani alipofika wilayani Muheza, alipata mawasiliano japo walikuwa wamechelewa. Nchemba akiwa ndani ya ndege hiyo alitua salama katika uwanja wa mpira wa Jitegemee wilayani Muheza ambapo alipokelewa na mwenyeji wake mbunge wa jimbo la Muheza Herbert Mntangi (CCM) na Mkuu wa Wilaya ya Subira Mgalu.

Akiwa katika mkutano, alisema kuwa watahakikisha tatizo la maji katika mji wa Muheza linamalizika na kwamba katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 watatenga fedha za ndani bila kujali wahisani.

Chanzo: Nipashe
 
Waache kuiga. Waliona Chadema wakiruka wakasema ni gharama, sasa wameanza na wao bila kuangalia kama hizo chopa wanazokodisha zina rada. Ukiiga tembo kunya............ CCM yenu ni makilimo kwanza waache makamanda wakomae angani.
 
Huyu Mwigulu naye ni laana zinamsumbua. Sifa zote hizi anazozitafuta kwenye mitandao ni za nini? By the way, hii nayo ni habari katika jukwaa la kisiasa?!! Siasa za kishamba hizi!
 
Huyu Mwigulu naye ni laana zinamsumbua. Sifa zote hizi anazozitafuta kwenye mitandao ni za nini? By the way, hii nayo ni habari katika jukwaa la kisiasa?!! Siasa za kishamba hizi!

Kama jana alifanya mikutano tanga nzima alivyoleta habari hapa, wakati masaa sita alikwama angani kwana ukweli hapo???

Na kuhusu jukwaa ni sawa, kwani alipotea akifanya siasa.
 
Mwingulu, Mwingulu Mchemba, huyu jamaa kwa kuutafuta umaarufu. Ngojeni kidogo, atasema CDM ndo wiloingilia mawasiliano ya chopa lake.
Umaarufu banaa agrrr. Apotee masaa 6 halafu aonekane, labda ka alifika mahali akaishiwa oil wakatumia miguu mpaka Michungwani kununua.
Asichezee Mungu. Ayakumbuke alotenda Arusha zile damu bado zinamtafuta
 
Huyu Mwigulu naye ni laana zinamsumbua. Sifa zote hizi anazozitafuta kwenye mitandao ni za nini? By the way, hii nayo ni habari katika jukwaa la kisiasa?!! Siasa za kishamba hizi!
Vipi ile ishu ya Igunga amesha clear!
 
Ni jana muhezaTanga, kwenye ziara yake ya chama/serikari.

Baada ya dereva wa chopa aliokodi kutoona pakutua, Tanga ni shideee, lakini story hii imefichwa sana na vyombo vingine, more story nipashe front page.

SOURCE: Nipashe.
mmh isijeikawa ni kisingizio alikua na mke wa mtu mahali akasingizia chopa imepotea. Tangu shughuli yake kule Tabora simwamini Kabisa mtu huyu
 
Waache kuiga. Waliona Chadema wakiruka wakasema ni gharama, sasa wameanza na wao bila kuangalia kama hizo chopa wanazokodisha zina rada. Ukiiga tembo kunya............ CCM yenu ni makilimo kwanza waache makamanda wakomae angani.

hapa naona umewamaliza, ccm ni kukopi na kupesti tu hawana lingine
 
Mwingulu, Mwingulu Mchemba, huyu jamaa kwa kuutafuta umaarufu. Ngojeni kidogo, atasema CDM ndo wiloingilia mawasiliano ya chopa lake.
Umaarufu banaa agrrr. Apotee masaa 6 halafu aonekane, labda ka alifika mahali akaishiwa oil wakatumia miguu mpaka Michungwani kununua.
Asichezee Mungu. Ayakumbuke alotenda Arusha zile damu bado zinamtafuta

Kaja kukanusa kitoto sana, wakati hii habari imeandikwa vizuri kwenye nipashe tena na jina la mwandishi lipo.
 
Back
Top Bottom