Mwigulu alikwenda kujifunza nini China?

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Mwigulu Nchemba mwezi wa Tano mwaka huu alikuwa safarini nje ya nchi 'kikazi' na inasemekana alikuwa China.
Wakati anaondoka kwenda huko hakutueleza humu JF lakini aliporejea tu nchini alituambia amerejea lakini hakutuambia nini hasa kilimpeleka huko.

Watu wengi wana wasiwasi mkubwa na Mwigulu kuhusu kitu alichokwenda kujifunza au kufanya huko Ughaibuni ukizingatia mabadiliko kadhaa yaliyojionyesha wazi wazi mara tu aliporudi, kwa mfano:

1/Amefuga ndevu nyingi na kumfanya kuonekana kama Jonas Savimbi, na kila aliyemuona aliona sura ya utisho au ukatili fulani.

2/Anavaa mavazi ya rangi ya kijani yenye mwenekano na muundo wa kijeshi kijeshi.

3/Anavaa kofia maalum na yenye alama ya nyota nyekundu(Hii ni kofia aliyokuwa inapendwa kuvaliwa na mkomonisti wa China Mao, mafashisti kadhaa duniani na baadhi ya madikteta wa Asia , Amerika ya kusini na Africa hapo zamani)

4/Ametoa mwongozo na msisitizo mkubwa sana kuwepo kwa makambi ya vijana wa CCM huko Mbeya na kupewa mafunzo maalum yenye mlengo na mwelekeo wa kijeshi.

5/Amekuwa akitoa kauli za kiamri kwa wananchi na wanaCCM kila alipopita kufanya mkutano au kikao.

6/Amekuwa akitoa kauli zenye kuonyesha kiburi cha CCM kuendelea kutawala kwa gharama yoyote(Kwa mfano, juzi Arusha alikaririwa akisema ''Wakazi wa Arusha wasipoichagua CCM wajiandae kufa!!'' na pia aliwahi kusema ''Mpende msipende CCM ni lazima itangazwe mshindi'')

7/Amekuwa akitoa Amri tatanishi kwa maRPC, DC, RC nk utadhani yeye ndiye aliyewaajiri(Amefanya hivyo Mbeya, Arusha na Manyara)

9/Amebadilisha mfumo mzima wa kufanya siasa, kwa sasa amekuwa akitembea na Shonza, Mwampamba na
Peter(Kijana aliyeharibika sura kwa kumwagiwa Tindikali) karibu kila mahali badala ya kuwabeba wajumbe muhimu wa juu wa chama.

9/Amekuwa akitoa fedha nyingi sana kwa vijana wake anaotaka kuwatuma kwenda kufanya shughuli fulani za kisiasa zenye hatari kubwa (Mfano kwenda kutiShia watu wanaiunga mkono CHADEMA hasa vijijini)

10/Amekuwa akiaandaa mikutano na Operesheni za Chama pasipo kupata maoni au ushauri wa wajumbe wengine wa Secretarieti ya CCM
(Yeye mwenyewe anadai baadhi ya makada wenzie ni waoga na pia kuna wanaotaka kumhujumu kwa sababu zao binafsi na hapo anakumbushia suala la Lwekatare namna walivyomwacha mwenyewe wakati shughuli ilipaswa kufanywa zaidi na Dola kuliko yeye binafsi)
 
Ukatili wowote anaoufanya na vilio vya wanyonge wasio kuwa na hatia yoyote ni laana. Yeye ajiande kuvuna anachopand, wala siku si nyingi tutajionea wenyewe maana mkono w Mungu si mfupi kushindwa kuchukua hatua mathubuti, Jicho la Mungu si bovu lisiweze kuona na kushuhudia uchafu huu,
Ni heri Mwigulu na Nape wangekuwa wazee ili wasione mabadiliko yajayo kupitia damu za wasiokuwa na hatia.

Heri waliolala mbele ya haki kuliko mimi na wewe tunaotenda uovu mkuu wa kukatisha maisha ya wasiokuwa na hatia.

HAKIKA MUNGU ALIYEKO JUU MBINGUNI ATATENDA JAMBO KUTUONYESHA YOTE HAYO YANAYOTENDWA SIRINI NA HAO WANAOJIITA CCM NA WATU WAO.
 
Kofia anayovaa Mwigulu pia nimemwona nayo jana mbunge Martha Mlata ktk taarifa ya habari itv naona ni sare yao mpya aliyowaletea toka China.
 
mnajadili mavazi ya mwigulu au mnajadili mwenendo wa chama chenu cha kigaidi
 
hii ni taarab tu mkuu, ngonjera ambazo hazina ukweli wowote kuwa mzalendo acha majungu
 
mnajadili mavazi ya mwigulu au mnajadili mwenendo wa chama chenu cha kigaidi
Jibu hoja na sio kuropoka uchafu wako hapa.
Kama Mwigulu alikwenda kujifunza kuvaa kikomonisti sema lakini sio kukwepesha hoja.
Kama huna hoja, ni bora ukaa kimya tu.
 
mnajadili mavazi ya mwigulu au mnajadili mwenendo wa chama chenu cha kigaidi

Jibu hoja moja baada ya nyingine, sema kama hayo yaliyotajwa ni kweli au si kweli. Yaani wote wapenda CC
M akili na uweze wenu unatia mashaka. Watu km wewe ndo mtaji wa CCM wanaofaidika na ujinga wako
 
Mtabadilisha sana JF ID's na kuja na vi-thread vya kibavicha bavicha ambavyo havijibu hoja za msingi kama hizi,



Halafu kitu kama hiki kitatakiwa kujibiwa mahakamani,



Pia hii evidence lazima ipate jibu. God is Great. Hakuna Mwenye mamlaka zaidi ya Mwenyezi Mungu. People did'nt get injured and die in VAIN. Shetani lazima atalipa.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    165.9 KB · Views: 48
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom