Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Baada ya kuona kombati alizoanza kutumia Mbowe CHADEMA na kisha kukubalika kwa watu wengi nchini, hasa vijana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Kaka Mwigulu Nchemba naye ameamua kuwa muasisi wa kombati zenye rangi ya kijani na njano, lengo lake akitaka vijana wavue kaki (Gwanda) wavae nyano na kijani (gamba). Ni wazo lake jipya akifikiri itakuwa ni mbinu ya kuwateka vijana wengi ambao kiukweli wako upande wa gwanda. Sasa hata ameamua kuweka chini skafu aliyozoea kuivaa na badala yake ameamua kuning'iniza shingoni ifananayo na zile za CHADEMA. Nisiseme mengi, wenyewe mwoneni hapo chini na vazi lake: