Mwigizaji maarufu 'Steve Nyerere' achukua fomu za kugombania ujumbe wa NEC ya CCM

Hapo mwanzo sikuwa nikifahamu kuwa kaka yetu STEPHEN NYERERE yupo CCM Lakini imethibitika Leo pale alipokuwa akichukua fomu za kugombea nafasi ya kamati kuu ya Chama hicho wilaya ya kinondoni. Ushauri wa bure ninaoweza kumpa ni kwamba aachane na Chama ambacho hakijaleta mabadiliko coyote tokea kichaguliwe kwa mbwembwe zote mwaka 2005 kwa ahadi hewa za ARI NGUVU NA KASI MPYA but nothing doing!!?? Mwaka 2010 ARI NGUVU KASI ZAIDI Still nothing!!??

Steve wewe ni kijana bado unganika na vijana wenzako kulikomboa taifa hili...

Another TRAGEDY OF MISCALCULATION, kazi ipo!
 
MSANII mwenye kipaji na upeo wa hali ya juu ukilinganisha na SUGU huyu anaweza kufanya kitu. Ngoja nije nipitie CV zao nilinganishe nadhani NYERERE atakuwa juu.

Kumbe wote wawili huwajui, ili kulinda heshima yako kaa kimya. Kulikuwa na sherehe ya kutoa tuzo za kilimanjaro music awards pale milimani city. Unaweza kukumbuku ujinga alioufanya jukwaani huyo mgombea wenu steven nyerere?
 
Hapo mwanzo sikuwa nikifahamu kuwa kaka yetu STEPHEN NYERERE yupo CCM Lakini imethibitika Leo pale alipokuwa akichukua fomu za kugombea nafasi ya kamati kuu ya Chama hicho wilaya ya kinondoni. Ushauri wa bure ninaoweza kumpa ni kwamba aachane na Chama ambacho hakijaleta mabadiliko coyote tokea kichaguliwe kwa mbwembwe zote mwaka 2005 kwa ahadi hewa za ARI NGUVU NA KASI MPYA but nothing doing!!?? Mwaka 2010 ARI NGUVU KASI ZAIDI Still nothing!!??

Steve wewe ni kijana bado unganika na vijana wenzako kulikomboa taifa hili...

siasa za nchi zinazoendelea hasa africa , na hasa kwetu bongo ni mchumia tumbo.Ni vyema kuangalia chimbuko la steve wapi ametoka na umaarufu ameupataje.Kimsingi amebebwa na mafisadi kwa kiwango kikubwa kila mara kutembeza bakuri kwa makala, kwa rizwan, kwa lowasa, kwa makamba , kwa membe nk.si kweli nimwana siasa kihivyo na si kwamba anaouwezo wa kuleta mabadiliko hasa kwa vijana walio wengi bali ni kutafuta umaarufu zaidi na pia kuwa karibu na mafisadi papa na si siasa.
 
Huyu ni msanii,anagombea uongozi kwa nguvu ya usanii,kama George Weah. It is a free nation. Ni haki yake kufanya hivyo.

Hata Arnold ,Na wengine wameingia katika siasa.Sijui upeo wa Steve nyerere.Ila kuna tofauti ya wasanii wa nje na wetu hata katika magenge ya bangi.Kwa aliyewahi msikia casillasi,Arnold ,Cosby,messi ,jamaa wa NBA lazima wawe na shule, actors wengi lazima college degree etc ataona kuwa hawa jamaa ni zaidi ya wasanii,ni intellectuals.Sijui kama itakuwaje naye kama atakuwa kama akina nanihii.
 
Jamani cha ajabu nini hapa? Mbona nyepesi nyepesi zinadai mwenzetu, kijana wetu Sikonge pamoja na mchezaji Asha Madinda wanajitosa pia.
 
Huyu MSANII uchwara nilijua ataishia huko kuzimu kwani kwenye interview zake na vyombo vya habari haishi kumtaja RIDHIWAN na BABA AKE.

Tena anawasifu kweli hadi nikawa napata wasiwasi mtoto wa kiume kuwasifia wanaume wenzie kwa kiwango kile jamani huyu tumsamehe bure hajui kusoma alama za nyakati na njaa zake.
 
Nchi hii ilishauzwa na Chama cha Mapinduzi kwa wazungu na mafisadi. Kazi ya kuiuza nchi ilianzishwa enzi za uenyekiti wa CCM taifa wa B. W. Mkapa; Mwenyekiti mpenda starehe alipoingia madarakani kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya akakamilisha kazi hiyo. Madini na nishati, ardhi, wanyama vipo mikononi mwa mabepari wa ulaya na mafisadi waeusi wa TZ.

Huyo Nyerere msanii anataka kukamilisha ndoto yake ya kumiliki mali za watanzania isivyohalali
.
 
Sioni tatizo huyu dogo kuchukua form kugombea ujumbe wa NEC ya CCM,ni haki yake ya kikatiba.Huyu ni msanii kwa hiyo mwacheni akafanye usanii wake vizuri akiwa ndani ya chama chake "sikivu"
 
Hicho chama atakachohamia chenyewe una uhakika kitafanya nini kama siyo yale yale ya LIBYA, TUNISIA na MISIRI.

NAPE kichatutanabahisha bwana nchi itauzwa kwa bei chee sana huko tuendako.
Vyama vilivyokuwa madarakani toke Uhuru vimeshapotea imebakia tuipoteze CCM katika medani za siasa
 
Ndo chama kinapotea, yani Steve Nyerere nae inawezekanaje? Ukijulikana kwa sifa zozote mbaya au nzuri unang'oa post. Wasomi vijana mko wapi muokoe chama?
 
Dah njaaa mbaya sana,huyu jamaa njaa ndio inayomsumbua,ameshindwa kusoma alama za nyakati!
 
Duh, tunakuombea mapambano mema, manake si mchezo chaguzi za CCM, usionge kitumbua jombaaaa!
 
Hapo mwanzo sikuwa nikifahamu kuwa kaka yetu STEPHEN NYERERE yupo CCM Lakini imethibitika Leo pale alipokuwa akichukua fomu za kugombea nafasi ya kamati kuu ya Chama hicho wilaya ya kinondoni. Ushauri wa bure ninaoweza kumpa ni kwamba aachane na Chama ambacho hakijaleta mabadiliko coyote tokea kichaguliwe kwa mbwembwe zote mwaka 2005 kwa ahadi hewa za ARI NGUVU NA KASI MPYA but nothing doing!!?? Mwaka 2010 ARI NGUVU KASI ZAIDI Still nothing!!??

Steve wewe ni kijana bado unganika na vijana wenzako kulikomboa taifa hili...

sasa CCM a.k.a Bongo Movie...CDM a.k.a HIP HOP
 
Huyu nadhani anaingia katika uongozi kwa nia ya kuchuma fedha. huko alikoenda ni sawasawa.
 
Back
Top Bottom