Mwigamba: Sitoki wala siombi radhi. Atoa ufafanuzi kuhusu Waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013

Mwigamba: Sitoki wala siombi radhi. Atoa ufafanuzi kuhusu Waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013

Tarime2015

Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
8
Reaction score
22
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadena mkoa wa Arusha Ndg. Samson Mwigamba asema hatoki chadema,na wala hataomba radhi.

Source; Mwananchi

============

TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013


Jumatano, 27 Novemba 2013

Jana katika taarifa kwa waandishi wa habari, Mhe. Tundu Lissu na Mhe. John Mnyika waliudanganya umma kuhusu waraka unaohusu Mkakati wa Mabadiliko 2013. Katika maelezo yao waheshimiwa hawa, pamoja na mambo mengine, walidai kuwa waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni feki. Ukweli ni kwamba:

  1. Ninathibitisha kwamba waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya HabariLeo, Jamhuri na Rai, pamoja na nakala iliyopo Jamii Forum. Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndio wenyewe, nawatumieni ‘soft copy' kutoka kwenye kompyuta mpakato (laptop) yangu ambako ndiko ulikoibwa na viongozi wa chama baada ya kunipora kwa nguvu laptop yangu Oktoba 25 na kukaa nayo hadi jioni ya Oktoba 28. Naomba kila mtu asome neno kwa neno waraka ninaowapa leo halafu afananishe na ule uliopo kwenye magazeti na kwenye mtandao ili mjiridhishe kama kweli sio wenyewe. Kama Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu wamekwama!
  2. Waraka huu si wa uhaini wala mapinduzi wala usaliti kama inavyodaiwa na akina Lissu. Huu ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama ambao ulikuwa ufanyike Desemba 2013, na ambao sasa umesogezwa mbele.
  3. Napenda ijulikane kwamba wakati wa uchaguzi si jambo la ajabu kuwa kwa wanachama kuwaunga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti Mbowe kwa miaka mingi na ninajua kwamba yeye naye anao mkakati tena unaohusisha mbinu haramu za kuhakikisha anammaliza Zitto na yeye kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi huo. Wanaoshiriki mkakati wake ni pamoja na Lema, Lissu na wakurugenzi kadhaa waliopo makao makuu.
  4. Waraka huu ulipaswa kuwa siri ndani ya watu watatu tu (M1, M2 na M3) na haikutarajiwa kwamba ungevuja kwa jamii. Bahati mbaya viongozi wa chama baada ya kuunasa waraka huu kutoka kwenye komputa yangu mpakato (laptop), na baada ya kikao cha Kamati Kuu, waliamua, kwa jazba na bila kutumia busara ya kiuongozi, kuusambaza waraka huo kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwakomoa na kuwadhalilisha waandaji. Sasa baaada ya kugundua madhara ya waraka huo machoni pa jamii wameamua kuukana. Ni ajabu kwamba wanaukana waraka ambao waliusambaza wenyewe.
  5. Nasisitiza kwamba mambo yaliyopo kwenye waraka ni bayana na dhahiri. Sibahatishi kwa sababu mimi nimefanya kazi makao makuu kama Mhasibu Mkuu hadi Mwezi Aprili 2012. Ni kwa kutambua uozo uliopo katika uongozi wa chama makao makuu niliona umuhimu wa kubadilisha uongozi kwa njia za kidemokrasia ili tukiokoe chama na hatukuwa na nia wala sababu za kuanika haya yote kwenye umma. Kwa sababu za chuki na kukosa busara za kiuongozi huyo anayeitwa Mwanasheria Mkuu akawashauri viongozi wetu kijinga wauanike waraka mbele ya macho ya watanzania. Wangekuwa na akili na busara baada ya yote haya kutokea wangejiuzulu au kuitisha uchaguzi mara moja.
  6. Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa siku nyingi sana na wametamani kumfukuza siku nyingi. Hata hivyo, ninawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama kwa sababu yeye hahusiki na waraka wetu wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 hata chembe, pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa na bado ndiye mlengwa mkuu, kama atakubali.


Samson Mwigamba (M3)
Arusha
Jumatano, 27 Novemba 2013.
 
Haya mambo bwana, kwani yeye kama hawamtaki atalazimisha?? Kwa ustaarabu wengi wakikukataa utang'ang'ania vipi?? Siku zinazidi kupungua, mbivu na mbichi kujulikana!
 
Nafikiri atakuwa amechanganyikiwa kutokana na dhambi ya USALITI aliyoifanya. Maana ata Yuda alipo msaliti Yesu alichanganyikiwa na kuamua kujinyonga.

wakuu, pamoja na u-cdm wangu ila daima suingi mkono katabia kalikozuka siku za karibuni kwa kila mwanachama mwenye mawazo tofauti na wengi wetu kubatizwa jina 'msalati' au 'mhaini' na mengine kama hayo. hakika kwa staili hii ya kupenda kuambiwa tunayopenda kuyasikia masikioni mwetu tu kuwang'oa maccm itakuwa ni safari ndefu!! kwa nini tusikubali ukweli wa kukosolewa ili tujirekebishe na kuwa bora zaidi - yaani mtu akimkosoa dr slaa au mbowe basi atakuwa msaliti, jamani kwa wao ni malaika hawakosei?? tujiulize swali dogo tu............mh lema alikuja na tuhuma nzito tu dhidi ya zzk hapa jf (haijalishi ni za kweli au la), by then zzk alikuwa pia ni kiongozi wa chama ni kwa nn kamanda lema asipeleke mashtaka yake ndani ya vikao halali vya chama na hatua stahiki kuchukuliwa haswa ikizingatiwa na yeye pia ni mshirika wa vikao hivyo?! cku zote chama kimekuwa kikisisitiza, viongozi kupeleka malalamiko (haswa dhidi ya jambo lolote kinyume na utaratibu ya chama) ndani ya vikao vya chama kwa hatua zaidi na sio VINGINEVYO. mbona mwigamba yeye alipolipuka hapa jf alilalamikiwa kwa kutosemea ndani ya chama......huu sio undumilakuwili??!! kwa nn sheria Ibague wakati tunaambiwa sharia ni msumeno unaokata kuwili?! jamani wanachadema wenzangu ifike mahali tusiwe wanafki, tusikimbilie kusema 'Lumumba buku 7', 'msaliti' 'mhaini' pasipo kuangalia mantiki ya hoja yenyewe.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadena mkoa wa Arusha Ndg. Samson Mwigamba asema hatoki chadema,na wala hataomba radhi.

Source; Mwananchi
Huyu si ndio yule wanamtandao wenzake wanasema kwenye waraka kuwa hali yake kiuchumi si nzuri na asaidiwe milioni 2 ili afungue mradi?

Kama ndivyo alivyosema basi ni kweli basi he's financially broke and politically dead. Wenzake saa hizi wanapigania mkate wao, wamemsahau.
 
Nakuunga mkono kamanda mwenzangu,ni kweli Zitto na wenzie ni wakosefu lakini pia Mbowe na wenzie Si malaika..Kuna haja ya kuchukuliwa hatua kina Lema,Kilewo,Saa nane na wengine waliokuwa wakimshambulia Zitto kwenye media.

Watakupiga tofali.
 
Wenye nyumba wamekwishakufukuza sasa unang'ang'ana nini tena!? Hawa mapandikizi wana matatizo makubwa sana. Hayo maamuzi ya kutotoka CHADEMA yatakuwa yametolewa na MACCM ili waendelee kufanya umamluki wao wa kukiharibu chama.

Ndiyo mikakati waliopeana ili wabaki kuwa wanachama wanaotumika kuharibu chama. CDM fanyeni maamuzi magumu, wafukuzeni uanachama hawa watu. Anzeni maisha upya.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadena mkoa wa Arusha Ndg. Samson Mwigamba asema hatoki chadema,na wala hataomba radhi.

Source; Mwananchi
Kiburi cha kipuuzi hichi - ni sawa na kufanya uwamuzi wa kuketi katikati ya barabara kubwa!!
 
Huyu si ndio yule wanamtandao wenzake wanasema kwenye waraka kuwa hali yake kiuchumi si nzuri na asaidiwe milioni 2 ili afungue mradi?

Kama ndivyo alivyosema basi ni kweli basi he's financially broke and politically dead. Wenzake saa hizi wanapigania mkate wao, wamemsahau.

Ndo kaisha huyo maskini..
 
Back
Top Bottom