MWIGAMBA: Kwenye mpambano kati ya Zitto na Maalim Seif, tayari Maalim ana ‘point’ moja!

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
MAALIM Seif Sharrif Hamad alihamia ACT-Wazalendo Machi 18, 2019. Hii ni baada ya ‘kusalimu amri’ kwenye mpambano wake na Prof. Ibrahim Lipumba kwenye CUF ya zamani. Maalim Seif aliingia kwenye mgogoro mkubwa na mwenyekiti wake Prof. Lipumba baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Maalim Seif alidai Lipumba alishajiuzulu uenyekiti wa CUF toka Agosti 2015 akipinga chama chake kumuunga mkono Edward Lowassa kama mgombea urais wa ushirikiano wa UKAWA. Maalim alidai kwamba Mkutano Mkuu wa CUF ulikutana na kukubali ombi la Lipumba la kujiuzulu.

Lakini Prof. Lipumba anadai kwamba kabla mkutano mkuu haujakutana kujadili ombi lake la kujiuzulu, alikutana na Maalim Seif wakazungumza na kuona umuhimu wa yeye kurudi kwenye uenyekiti na hivyo akaandika barua ya kufuta barua yake ya kujiuzulu. Kwa lugha nyingine Lipumba anasema kwamba wakati mkutano mkuu maalum unajadili kujiuzulu kwa Lipumba, ulikuwa unajadili barua hewa ambayo haikuwepo ilikuwa imeshafutwa!

Baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukubaliana na hoja za Lipumba na kuamua kumtambua kama Mwenyekiti halali wa CUF, Maalim Seif na kundi lake waliamua kukimbilia mahakamani. Kesi iliunguruma na hatimaye mahakama nayo kwenye hukumu yake ikakubaliana na upande wa Lipumba na kumtambua kama mwenyekiti halali wa CUF. Siku hiyo hiyo Mahakama ilipotoa hukumu yake ndiyo Maalim Seif na kundi lake walihamia ACT-Wazalendo.

Miezi mitatu baadaye yaani Juni 18, 2019 niliandika makala yenye kichwa cha habari: “Zitto ajiandae kupambana na Maalim Seif, hana hadhi ya kupambana na JPM. Nitakumbusha kidogo kwa nini nilisema wawili hawa lazima watapambana mbele ya safari. Moja nilisema huyu kijana ni mnafiki, kigeugeu na asiyeaminika! Akisema hasemi ukweli, akiaminiwa haaminiki na akiweka ahadi hatekelezi!

Zitto anaweza kuongea kama mpambanaji mkubwa dhidi ya ufisadi na wizi nchini kumbe ndiye fisadi wa kutupwa! Anaweza kuongea kama mzalendo namba moja wa nchi yake, kumbe msaliti na kibaraka namba moja wa mabeberu. Zitto ukiongea naye jambo usiku saa 3, usitegemee kwamba kukicha saa 12 asubuhi bado atakuwa nawe katika kile mlichoongea. Unaweza kukuta alishakugeuka ndani ya masaa 9 tu ya usiku.

Nilisema wazi kwamba nimekaa na kufanya kazi na wanasiasa wengi tokea niingie rasmi kwenye siasa. Katika wanasiasa wote niliofanya nao kazi mpaka leo, sijawahi kuona mwanasiasa mnafiki kama Zitto Zuberi Kabwe! Katika wanasiasa waliopata kuwa marafiki zangu sana kwenye siasa za nchi hii ni Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Anthony Komu, Kitila Mkumbo na Peter Mwambuja! Kati yao hakuna mnafiki, kigeugeu na asiyeaminika kama Zitto!

Hakuna mwanasiasa aliyewahi kumwamini Zitto Kabwe akaaminika. Kuanzia Freeman Mbowe aliyemwingiza kwenye siasa za kitaifa mpaka Kitila Mkumbo ambaye Zitto kwa kinywa chake aliwahi kututamkia kwamba Kitila ndiye alikuwa injini yake. Kwa kifupi Zitto aliaminiwa na Freeman Mbowe, Willibrod Slaa, Marehemu Chacha Wangwe, Anthony Komu na wakurugenzi wenzake wa makao makuu ya CHADEMA, Marehemu Bob Makani, Marehemu Philemon Ndesamburo, Marehemu Amani Kabourou, hakuaminika!

Aliaminiwa na vijana wake waliokuwa tayari kumsaidia kwa lolote dhidi ya Mbowe: akina Ben Saanane, Habibu Mchange, Juliana Shonza na Mtera Mwampamba lakini hakuaminika! Maswahiba wake wa kufa na kuzikana akina Msafiri Mtemelwa na David Kafulila nao wakamwamini lakini hakuaminika!

Kitila naye alimwamini Zitto lakini aliishia kuwa mhanga wa huyu mwanasiasa mdogo lakini aliyeumiza wengi! Zitto aliyedai kwamba kumwachanisha na Kitila ni sawa na kumwondoa kwenye siasa, ndiye Zitto aliyefanya mkutano na wanaandishi wa habari na kudai chama kimebariki uteuzi wa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Lakini nataka nikuhakikishie kwamba ni Zitto huyo huyo aliyeanzisha mchakato wa siri wa kumvua Kitila uanachama wa ACT-Wazalendo baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara kwenye serikali ya CCM.

Huyo ndiye Zitto Kabwe aliyekuwa upande wa Lipumba wakati mgogoro wa ndani ya CUF umeanza. Alimsaidia Lipumba kwa kumpa vijana wa kufanya fitna. Lakini pia alimpa Lipumba wanasheria wa kumtetea kwenye kesi aliyofunguliwa na upande wa Maalim Seif. Kabla kesi haijaisha akahamia upande wa Maalim Seif na leo Maalim Seif ni mwanachama namba moja wa ACT na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho.

Huyu ndiye Zitto Kabwe ambaye kwenye makala ile nilisema wazi kwamba, “Nguvu anazotumia kupambana na ‘jabali’ JPM anazipoteza bure na atazijutia. Magufuli anazidi kuchanja mbuga. Treni yake ya kuelekea uchumi wa kati imeshika kasi na kama Zitto anadhani anaweza kuizuia kwa tamaa yake ya madaraka, asimame relini kujaribu kuizuia ‘treni’ hii aone itakavyompasua vipande vipande! Nguvu anazotumia kupambana na Magufuli, azitunze aje azitumie kupambana na Maalim Seif.” Samson Mwigamba, Kalamu ya Mwigamba, Juni 18, 2019.

Kama utabiri huu alidhani ni ndoto za mchana, akumbuke matukio ya hivi karibuni tu wala asiende mbali. Akumbuke alivyoumbuka siku alipojaribu kumsingizia Rais Magufuli kwamba amemfukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi. Aangalie alivyokurupuka na jinsi watanzania walivyomshambulia mpaka kwa aibu akaja kukanusha habari yake yeye mwenyewe!

Kama hiyo haitoshi atazame juhudi zote alizofanya kuzuia mkopo wa Benki ya Dunia kwa Tanzania kwa ajili ya Mradi Kabambe wa Kuboresha Elimu ya Sekondari nchini. Amefanya jitihada kubwa za kuandika barua kwa kutumia nembo ya bunge, ameenda mwenyewe Marekani kuwashawishi wasitoe huo mkopo. Wakati akifanya hayo yote Rais Magufuli alikuwa hapa nchini anaendelea na shughuli zake wala hakuwahi kumtuma hata Afisaelimu wa Mkoa kwenda kuzungumza na Benki ya Dunia!

Lakini Zitto ‘ameangukia pua’ baada ya Benki ya Dunia kutangaza kwamba itatoa mkopo huo kwa serikali. Maelezo yaliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia, maelezo ya Mkurugenzi wa Benki hiyo hapa nchini, ‘yamemvua nguo’ Zitto akabaki uchi wa kisiasa! Kwa aibu akaandika andiko la kuipongeza benki hiyo na wanaharakani wenzake kana kwamba mkopo huo umetokana na juhudi zake na wanaharakati wenzake. Kweli kuongozwa na huyu jamaa kama kiongozi wako wa chama ni shida!

Kwenye makala yangu ile nilisema Maalim Seif kwa upande mwingine ni Sultani. Kwenye kila chama anachokuwemo Maalim Seif, kila mpemba aliyemo kwenye chama hicho anakuwa kiongozi na thamani zaidi ya kiongozi yeyote wa bara. Mpemba anaweza kuelekeza jambo lolote ndani ya chama alichomo Maalim Seif.

Msimamo na malengo ya chama ni lazima yajikite Zanzibar kibajeti na kimikakati. Lazima kutakuwa na kikao cha wazanzibari walioko kwenye uongozi wa chama hicho nje ya vikao vya chama vya kikatiba kabla na baada ya vikao hivyo. Kila mtanganyika ni adui wa Zanzibar hata kama ni mwanachama wa chama alichomo Maalim Seif.

Maalim Seif ni Sultani wa pili wa Zanzibar baada ya yule wa kwanza kuondolewa kwa mapanga kwenye mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964. Sultani wa pili anawekwa mbali na ikulu kwa sanduku la kura! Sultani huyu ana wapambe wake akina Ismail Jussa Ladhu, Salim Bimani, Nassor Mazrui na Issah Kheri. Kwenye chama chochote alichomo Maalim Seif, yeye na hawa wapambe wake ndio watakuwa na maamuzi.

Naweza kutamka bayana sasa kwamba kwenye mpambano kati ya Zitto na Maalim Seif, tayari Maalim ana ‘point’ moja! Amejipanga tayari ndani ya ACT tena akiwa makini asirudie makosa aliyoyafanya kwenye CUF mpaka kuja kutimuliwa. Zitto alipomtaka Maalim kwenye ACT alipewa masharti ambayo Maalim alijua kabisa kwamba yatamlinda atakapoanza usultani wake. Alipelekwa mpaka kwa wazee wa Pemba wakamwapisha na kumpa masharti akakubaliana nayo!

Akihojiwa na Shirika la Habari la BBC kabla ya uchaguzi wa ndani ya ACT, Maalim aliulizwa kwamba tayari alishapewa nafasi ya kuwa Mshauri Mkuuwa chama hicho kwa nini amechukua fomu ya kugombea uenyekiti? Akajibu kwamba, “Ukiwa mshauri unashauri na ushauri wako unaweza kukubaliwa au kukataliwa. Mimi nataka niwe Mwenyekiti ili niweze kufanya maamuzi siyo kushauri!” Sultani huyo!

Mwaka jana nilisema, “Hivi tunavyozungumza karibu wote hawa na wengine wengi wa upande wa Maalim Seif wameshaingizwa kwenye kamati kuu. Baada ya uchaguzi wa ndani ya chama, watazidi kuingia wengine.” Fuatilia leo ‘composition’ ya Kamati Kuu ya ACT uone. Theluthi mbili ni watu wa Maalim Seif.

Nilisema, “Tayari mikakati ya ‘kuwapiga chini’ baadhi ya viongozi wa zamani ndani ya ACT imeshaanza. Hata uchaguzi uliosimamiwa na viongozi wa zamani kwenye majimbo na mikoa nusura ufutwe na kamati kuu ili uanze upya.” Leo ninapoandika makala hii kuna barua za viongozi wa ACT-Wazalendo mikoa mitatu ya Ruvuma, Singida na Manyara ziko kwa Msajili wa Vyama. Viongozi wote hawa wanalalamikia kuenguliwa kwenye mkutano mkuu wa chama uliofanyika Machi 14 mwaka huu uliowachagua akina Zitto Kabwe na Maalim Seif.

Kutoka upande wa bara ni majimbo 68 tu yaliyoruhusiwa kupeleka wajumbe kwenye mkutano huo wakati Zanzibar majimbo yote yaliruhusiwa. Nia ilikuwa ni kuhakikisha wajumbe wa bara ambao ndio wangewanya kura zao kati ya Maalim Seif na Yeremiah Maganja, wanakuwa wachache sana. Lengo lilikuwa wajumbe wote wa Zanzibar wakimpa kura Maalim Seif na wachache wa bara wakagawanyisha kura zao, ni rahisi Maalim kushinda. Ndivyo ilivyokuwa wakiongeza na mbinu nyinginezo, Maalim akashinda kwa asilimia 93.

Mabadiliko ya Katiba ya ACT nayo ni kwa ajili ya kumsaidia Maalim Seif. Tutayajadili wakati utakapowadia. Tusubiri kwanza wayapitishe mabadiliko hayo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zito siyo nyumbu alikataa udikteta wa Mbowe.

Sent using Jamii Forums mobile app
SIMLAUMU Zitto Kabwe NAWALAUMU WALIOISHI NAE NA HAWAKUMUELEWA.

Ilinichukua miezi tisa kumuelewa Zitto na kupingana kabisa na aina yake ya siasa, utamaduni wake wa kutumia nguvu za watu kujineemesha na hulka yake ya kuwadharau watu baada ya kuwatumia kufikia malengo yake.

Hivi mtu Kama Samson Mwigamba aliyefanya harakati nyingi na Zitto ila akashindwa kumuelewa huyu na Zitto nani alaumiwe? Huwezi kuwa mwanaume tena mwenye akili timamu ukatumiwa miaka yote unakuja kushtuka tayari ushageuka Condom iliyotumika. Wewe lazima utakuwa kilaza.

Wiston Andrew Mogha huyu hawezi kabisa kumlaumu Zitto ila ajilaumu yeye mwenyewe kwa kukubali kuwa slow learner. Amekuwa mpambe wa Zitto kwa muda kweli ila bahati mbaya kaja kumuelewa kipindi ambacho anaachana na ujana kuukaribisha uzee.

Eti Edna Sunga alimuelewa Zitto mapema kuliko Maganja, huu uanaume wa wapi? Mtoto wa kike sawa na mjukuu wako anawezaje kuutambua ukweli kabla yako mtoto wa kiume na mwenye mishahada kibao kichwani mwako?

Eti Ambakisye Mwakisyala Mlima anauelewa mpana sana kuliko Karama Kaila ambaye kwa sasa kuondoka Act Wazalendo anaona aibu ila moyo na akili zishakimbia.

Hawa kina Wilson Elias Mwambe ni walewale walitumiwa kutukana watu wakiamini wataaminiwa daima, leo wameshtuka wanageuka mbogo.

Shaaban Mambo mzee wangu pamoja na kuwa mwanasiasa mkongwe nashangaa unalalamika leo kuchezewa rafu na kijana uliyemuhusudu na kumsifia kila ulipopewa nafasi.

Watu wameanza kumuelewa Zitto nasikitika muda umeenda ila hakuna marefu yasiyo na ncha, Mpaka sasa uwezo wa kurirudisha jimbo ni mdogo sana, ni ndoto za alinacha. Njia pekee aliyobaki nayo ni kupiga ruzuku na ili apige Ruzuku ni lazima awekeze Zanzibar kwa Maalim huku bara hana lake kabisa.

Utabiri wangu, Mgombea wa NCCR Mageuzi Jimbo la Kigoma Mjini ni Wiston Mogha na kwa jinsi upepo unavyovuma huyu ni mshindi tayari.

Asubuhi njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli we unamjua zitto. Unayoyasema ndio anayofanya sasa. Hata ishu ya CAG mstaafu ye ndio alisema katekwa na wasiojulikana. Badae Prof Assad akasema alikuwa kisarawe kwenye shughuli zake.

Ni zitto huyu huyu aliyefunga safari hadi bukoba kumzika mama yake Kabendera lakini alishindwa kumpatia hata dawa wakati kabendera alipokuwa lockup na huku akijipambanua ye ni rafiki sana wa kabendera.

Sie wengine tulimfahamu huyu mtoto kuwa sio wa kawaida toka alipowekwa na kina mzee kikwete kwenye ile kamati ya madini. Mswahili mpe ulaji tu, akiwa na njaa utadhani ni mzalendo kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwigamba! Pole sana wewe na wahanga wenzako wa demokrasia akina daza steven etal.

ACT inapita kwenye wave na sasa iko kwenye 3rd Wave.

1st Wave walikuwa waasisi. Wengi wao walikuwa wadau wa mabadiliko wa kweli na walikuwa wakijitolewa kwa hali na mali wakiamini ACT itakuwa na brand mpya ya siasa za Tanzania. Wave hii iliondolewa rasmi mwanzoni mwa Mwaka 2015.

2end Wave, Kundi lililotoka CHADEMA likiongozwa na zitto. Kundi hilo lilienda ACT likiamini lenyewe ndilo linaloimiliki ACT. Lilivyofika likatupilia mbali kilichoitwa misingi iliyokiasisi chama hicho na kuanza vita ya madaraka ilikiwa na element za fitna na hila kwa ndani na kwa nje kukimbizana na matukio, kosa ambalo limekuwa likifanywa na vyama vyote vya upinzani katika zama zote.

3rd Wave: ndio hiyo unayozungumzia hapo juu ambapo mamlaka inahamia Zanzibar.

Kwa lugha nyingine wakati wa 1st Wave, nguvu ilikuwa kwa Watu wa kawaida kabisa wakiongozwa na nguvu ya hoja na misingi, 2end Wave, nguvu ikahamia kwa Zitto personaly na 3rd Wave nguvu inahama kuelekea kwa Maalim. Tunasubiria 4th Wave ambapo 2end Wave itapambana na 3rd wave.

Kwa ujumla siasa za madaraka na vyeo huwa zinakuwa hivyo na hakuna lakufanya.
 
Ukweli ni kuwa kwa sasa ACT wazalendo nguvu zake ziko Zanzibar, na Maalim Seif ni nguli hasa wa siasa. Na ukweli kuwa nguvu ya ACT iko Zanzibar hilo Maalim Seif analijua vyema. Hakuna namna yoyote Maalim seif ataacha kuwaweka Wapemba mbele, wakati anajua fika 99% ya majimbo ya ACT yatatoka Zanzibar.

Maalim seif na wafuasi wake hawakwenda ACT kufanya siasa, bali wamehamia kwenye nyumba ya dharura baada ya nyumba yao halisi CUF kukumbwa na dhoruba. Anachowinda Zito ni ruzuku ili ajijenge huku bara, lakini anajua fika kwa huku bara, cdm ndio chama halisi cha upinzani chenye uungwaji mkono mkubwa.
 
Shetani wa Siasa ni mbaya kuliko shetani mwingine yeyote Yule,

Kila kukicha kwenye siasa yanazaliwa mengine mabaya kuliko ya juzi na Jana, Shetani wa kwenye siasa Yuko tayari kumtumia mtu Kwa ajiri yake binafsi na kuliacha kundi kubwa likiishi Kwa dhiki kubwa na mateso

Shetani la kwenye Siasa halina aibu Wala kumbukumbu za badae itakuweje, Shetani la siasa, linawaondolea watu ufahamu Wao na hawajui kama ufahamu Wao umeondolewa,

Shetani la siasa, linamfanya mtu awe Dikiteta, linamfanya mtu awe muuwaji wa watu wengine, kudhurumu, kupola mali za wengine na kuwakandamiza,

Hilo ndilo shetani la siasa bhana, shetani la siasa linaweza kuwadanganya walionje ya siasa, watu wawili wanasiasa kuanza kupondana,kutukanana Kwa matusi yote kumbe Lao moja, huyo ndiye shetani wa siasa
 
Ndugu mwigamba acha chuki Binafsi kwa Zitto.

Kwanza nataka uelewe malengo ya chama chochote cha siasa na pia usisahaui kufanya analysis ya hali ya siasa ilivyo kwa sasa.

Miongoni mwa malengo ya chama chochote ni kukuwa na kuishi. Katika hali hii ya dhoruba servival ya chama ni m,uhimu kuliko chochote.

Upande wa Bara ACT ina kazi ya kujieneza kutokana na uwepoi wa vyama vyenye nguvu tayari.

Zito na wenzake ndani ya ACT wamefanya analysisi ya kutumia loop hall ya Zanzibar kumpata kiongozi kama Maalim Seif na kundi kubwa alilonalo ambapo chama chochote kingefanya.

Hata Maalim angeenda NLD ingekuwa hivyo.

Mazingira ya Zanzibar yanakihakikishia ACT kukua na kupata kjiimarisha zaidi hapo mbele kuliko wakati wowote ule baada ya uchaguzi wa 2020 kwenye majaaliwa.

Mtu kama wewe kuanza kutumia element za usultan wa Maalim Seif ni kujejea somo la sayansi ya siasa. Unapotosha wakati unajuwa Maalim Seif ni Asset kwa siasa za Tanzania upande wa Zanzibar.

Lengine ni hili la kuanza kutumia fitna za Ubara na Upemba. Siasa za Zanzibar zijuwe kwamba zina Ajenda ya kudumu. Hilo usilisahau. Viongozi wa CCM hapo ndipo wanakwama kuidhibiti Zanzibar na hatimae huishia kufuta chaguzi tu. Kule watu wanataka mabadiliko ya Muungano hilo lijue. Njia za kistaarabu ni kutumia vyama kama mfumo rasmi wa kuleta mabadiliko.

Mwigamba elewea kwama hizi fitina hazisaidii kuijenga ACT kwa sasa kwa kupenyeza sumu ya ugomvi na kupandikiza fitna ili ionekane kuna ACT bara na Zanzibar kwa sababu ya kuja Maalim Seif. Maalim Seif amekuja ACT with full enegry. Hilo kila mtu analijuwa. Hapa ishu ni vipi ACT itaweza kuhimili siasa za wakati huu na kujihakikishia survival?

Sio kwamba huelewi lakini umeamua kupotosha bure.

Hao akina Maganja na wengine wanaojitoa ACT wanaongozwa na maslahi binafsi badala ya kutazama mambo at a focus na kwa jicho la mbali.

Nakushauri Mwigamba uwe Karibu na Msajili wa Vyama na ingia katika hio kamati ya kutaka kuleta vurumai kwenye ACT ili Msajili alete Fitna kama aliyofanya kule CUF. Jitahidi kufanya hivyo ili malengo yenu yatimie kabla ya uchaguziu wa 2020.

ACT kwa Upande wa Zanzibar ni more than strategy elewa hivyo. Upotoshaji huo wa Ubara na Upemba ulifanywa sana na haukusaidia.


Kila chama kilihitaji support ya Maalim Seif kupenya Zanzibar na ACT imepata hio bahaTI. oNA ccm INAVYOTUMIA jESHI KUPENDWA NA KUBAKI ZANZIBAR. KILA MTU APEWE HADHI YAKE.


Kishada
 
Hiki ni kipindi cha kukijenga chama na kukiimarisha, sio wakati wa kusaka tonge na kukimbia safari iliyoanza.

Political build up ya Tanzania huwezi kuiacha Zamnzibar na nguvu za Maalim Seif kwa Sasa. Dunia nzima hilo wanalijuwa.

Chama kama ACT kupata bahati ya kujieneza kirahisi Zanzibar ambapo kunaihakikishia kupata fursa ya kukua na hata Bara hapo baadae liachwe bure kwa klisingizio cha Usultani wa Maalim Seif? Fursa hio waliipoteza CCM, CUF ya Lipumba na hata Chadema walihitaji sana kumpata mtu kama Maalim Seif.


Matatizo yote inayoipata Tanzania katika Mahusiano ya Kimataifa na kidiplomasia ni kutokana bna kusiginwa haki za kisiasa na demokrasia Zanzibar ambapo huwezi kukamilisha stori bila kumtaja Maalim Seif.


Huyu Maalim ambaye ndio nembo ya Upinzani kwa Zanzibar na Tanzania uache fursa bure wakati malengo halisi ya chama hayajafikiwa huko ni kuwehuka.

Subiri uone CUF itakavyokuwa baada ya 2020 ndio utajuwa maana ya Maalim Seif kwenye siasa za nchi hii.
 
Back
Top Bottom