Mwigamba ampamba Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigamba ampamba Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanda2, Sep 24, 2009.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimesoma makala ya kusifiwa Mbowe na waandishi wake alianza KIBANDA sasa kaja huyu mwenzake.
   
 2. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Huyu ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA!

  BAADA ya makala ya Septemba 9, mwaka huu, wasomaji wengi walinipigia simu na wengine kunitumia ujumbe mfupi wakiomba niandike makala maalumu inayomwelezea Freeman Mbowe, Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Kwa kuwa wote waliowasiliana nami niliwaahidi kwamba nitafanya hivyo, naomba leo nitimize ahadi hiyo kwa kuwaletea kwa kifupi wasifu wa Mbowe ambaye leo anajulikana kwa jina la Kamanda wa Anga.

  Natangulia kumwomba radhi Mbowe kwa kuwa sikumshirikisha katika kuandaa makala hii. Kwanza, ili nisilalie upande wowote na pili, kwa sababu ilikuwa ngumu kumpata kwa kuwa alikuwa nje ya nchi.

  Freeman Aikael Mbowe, alizaliwa Septemba 14, mwaka 1961, ikiwa ni takriban miezi mitatu kabla ya Tanganyika kupata uhuru ambao ulitarajiwa kutangazwa rasmi Desemba 9, mwaka 1961.

  Baba yake (mzee Aikael Mbowe), alikuwa miongoni mwa wapigania uhuru wa Tanganyika akishirikiana vema na kina Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  Kwa sababu ya harakati alizozifanya na mapenzi kwa nchi yake, aliyotarajia iwe huru siku moja, mzee Mbowe aliamua kutombatiza mwanawe mpaka siku ya uhuru.

  Kwa hiyo, mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA, alibatizwa siku ya uhuru na kupewa jina la Freeman (akimaanisha ‘mtu huru').

  Mbowe ni miongoni mwa waanzilishi wa CHADEMA baada ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa kuruhusiwa tena rasmi mwaka 1992.

  Ndiye mwanzilishi wa CHADEMA aliyekuwa na umri mdogo kabisa kuliko wote walioianzisha CHADEMA. Katika kukitumikia chama kwa muda mrefu, alitumika kama Mkurugenzi wa Vijana makao makuu ya chama hicho.

  Mnamo mwaka 2000; Mbowe aligombea ubunge wa Hai kupitia CHADEMA, akashinda huku idadi kubwa ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho wakishinda na kuifanya CHADEMA kuunda Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro huku ikiiacha CCM.

  CHADEMA kilikua chama cha upinzani ndani ya Halmashauri ya Hai kama ilivyokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Kigoma Ujiji.

  Ndani ya miaka mitano ya ubunge wa Mbowe na utawala wa CHADEMA katika Halmashauri ya Hai, shule za sekondari zaidi ya 11 ziliongezeka na kuboreka kwa huduma ya elimu ndani ya wilaya hiyo pamoja na huduma ya afya.

  Si hivyo tu, bali Wilaya ya Hai ilichomoza kuwa wilaya ya kwanza kufuta kodi za manyanyaso, ikiwamo ile iliyoitwa kodi ya kichwa (kodi ya maendeleo) na kodi ya baiskeli, ikifuatiwa na halmashauri nyingine zilizoongozwa na CHADEMA.

  Jambo hili lilibezwa sana na viongozi wa serikali kuu inayoongozwa na CCM hadi leo wakidai halmashauri itakosa pesa za kujiendesha.

  Lakini, kinyume chake hatua ile iliwapunguzia wananchi mzigo na kuwatia moyo wa kutoa kodi za halali na kuiwezesha halmashauri kupata maendeleo ndani ya miaka mitano ukilinganisha na yale yaliyoletwa na CCM kwa miaka karibu 40 ya uongozi wao ndani ya jimbo hilo.

  Kwa ujumla Wilaya ya Hai na Karatu tayari zilishajenga sekondari kila kata kabla ya mwaka 2005, tena kwa ushirikiano mzuri kati ya wananchi na halmashauri, tofauti na mtindo wa kujizolea sifa uliofanywa na kina Lowassa (waziri mkuu wa zamani) baada ya mwaka 2005, ambapo walitoa maagizo tu kwa wakuu wa wilaya na wakuu wa wilaya nao wanatoa maagizo kwa wakurugenzi wa wilaya, na wao wanatoa maagizo kwa maafisa watendaji wa kata, ambao nao walishirikiana na maafisa watendaji wa vijiji kulazimisha wananchi kutoa pesa ili shule zijengwe, wanafunzi warundikwe humo bila walimu, bila vitabu wala vifaa vingine vya kufundishia.

  Matokeo yake ndiyo yale ya kina mama wajawazito kukamatwa na kufungiwa ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata na hatimaye wakajifungulia humo, kisa, eti wameshindwa kutoa sh 10,000 ya kuchangia ujenzi wa shule.

  Niliwahi kueleza hapa jinsi ambavyo shule moja ilianzishwa huko Shinyanga ikajikuta imepata mabinti wawili tu waliomaliza kidato cha sita ‘wakahudhuria' mafunzo ya ualimu kwa mwezi mmoja, narudia, mwezi mmoja halafu wakapangiwa shule na wakajikuta wako wawili tu na wote ni hao hao wa mwezi mmoja waliojulikana sana kama ‘voda fasta'.

  Ndipo mmoja akajiteua kuwa Mkuu wa Shule (Headmistress) na mwingine akawa Makamu Mkuu wa Shule (Second Mistress). Unaipata hiyo ya kina Lowassa na Kikwete ? Yote hiyo ili mradi wao watambe kwenye runinga kwamba wamejenga shule nyingi na wanafunzi wengi wameingia sekondari!

  Ajabu baada ya miezi mitatu, yule headmistress akajiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Sijamuuliza kwamba shule ilibaki na second mistress pekee?

  Ni katika kipindi hicho cha ubunge wa Hai ndipo Mheshimiwa Mbowe alipojitambulisha zaidi kuwa ni kiongozi imara, mwenye maono, asiyeyumba, na mchapakazi katika kutimiza malengo yaliyowekwa pamoja na mtetezi wa watu.

  Akiwa mbunge wa Hai, Mbowe alisikika sana ndani na nje ya Bunge kwa hoja zake moto moto bungeni. Lakini bado alijinyima mpaka kupata muda wa makala kwenye gazeti la Rai la wakati huo.

  Wengi tunamkumbuka kwa makala zake ambazo dhahiri ziliwatetea Watanzania kwa ujumla kwa ujasiri akiandika na kumkosoa rais wa wakati huo Benjamin Mkapa.

  Kupitia makala zake aliwaelimisha Watanzania wengi jinsi nchi hii ilivyo na uwezo wa kuwa miongoni mwa nchi tajiri lakini inafukarishwa na watawala walafi, mafisadi na wabinafsi waliojazana ndani ya CCM.

  Baadaye mwaka 2003, Mbowe akiwa na umri wa miaka 42 aliwaunganisha wabunge wote watano wa CHADEMA na kuanzisha ziara za mkoa kwa mkoa ili kukiimarisha chama huku wakitumia gharama zao binafsi (wakati huo chama kilikuwa kikipokea ruzuku ya sh milioni tano tu kutoka serikalini kwa mwezi).

  Wenye kumbukumbu watakumbuka kwamba Mbowe ndiye mwanzilishi wa vita dhidi ya ufisadi.

  Katika ziara hizo Mbowe alitembea na kijitabu cha ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambazo zilionyesha ubadhirifu wa mamilioni na mabilioni ya fedha za walipa kodi wa taifa hili kwenye serikali kuu na halmashauri zote zilizoongozwa na CCM kote nchini.

  Ni katika kipindi hiki pia alipokuwa akipambana na utawala mbovu na wa kiimla, si tu kwenye serikali bali hata bungeni wakati huo Spika wa Bunge akiwa mzee Pius Msekwa.

  Baada ya kumlipua majukwaani jinsi alivyokuwa akiendesha Bunge kwa upendeleo dhidi ya wabunge wa chama tawala huku akiwabana wa upinzani, Spika wa wakati huo akakimbilia kumshitaki Mbowe kwenye Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakati huo ikiongozwa na Eliakim Simpasa, mbunge katili na aliyefurahia sana ‘kuwanyonga' watu kwa kutumia kamati hiyo kiasi cha kamati hiyo kufikia kuitwa jina la ‘Kamati ya Simpasa'.

  Hata hivyo kamati hiyo iligonga mwamba kwa Mbowe ambaye alizijua haki zake na kukimbia mahakamani na mahakama kuzuia pendekezo lolote la kamati ya Simpasa dhidi ya Mbowe.

  Hivyo mpaka Bunge linavunjwa Agosti 2005, Mbowe hakuwahi kuadhibiwa na Bunge kwa kuanika hadharani upendeleo wa Msekwa katika kuliongoza Bunge.

  Pia Mbowe na wenzake wakaazimia kujichimbia katika jimbo la Simpasa huko Mbozi Magharibi na wakishirikiana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa wakati huo, Bob Makani, kumhakikishia Simpasa kwamba watahakikisha harudi bungeni 2005 na ndivyo ilivyokuwa.

  Walipiga kambi Mbozi wakamwanika mpaka wana CCM wenyewe wakamkataa kwenye kura za maoni, ingawa alikuwa amewatambia akina Mbowe kwamba kama wangeenda kumsema vibaya kule Mbozi Magharibi, wananchi wangewapiga mawe.

  Mwaka 2004, Bob Makani aliamua kustaafu uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya taifa na kumwachia Freeman Mbowe ambaye alikuwa mgombea pekee.

  Baada tu ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Machi mwaka 2004, Mbowe aliendeleza harakati zake za kukijenga chama na kukiimarisha akizunguka pamoja na wabunge wenzake ambao wengi wao walichaguliwa pamoja naye kuongoza chama.

  Yeye mbunge wa Hai alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa, Mbunge wa Kigoma mjini, Aman Kabourou, akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, akipitishwa kuwa Katibu Mkuu na kuwaacha wabunge wawili ambao hawakushika nafasi za juu za uongozi wa chama ambao ni Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Grace Kiwelu (Viti Maalumu).

  Chini ya uongozi wa Mbowe, ndipo CHADEMA kwa mara ya kwanza ikapata ujasri wa kusimamisha mgombea wa urais na kuibuka kikiwa cha tatu kwa matokeo ya urais Tanzania nzima lakini kikiwa cha pili kwa Tanzania Bara.

  Kikaongeza wabunge kutoka watano waliopatikana mwaka 2000 hadi 11 mwaka 2005. Kwa wingi wa kura walizopata CHADEMA sasa wanapata ruzuku ya takriban sh milioni 60 tofauti na sh milioni tano walizokuwa wakipata mwaka 2000 hadi 2005.

  Lakini, Mbowe ni mbunifu na wakati wote anatafuta fursa ya kukiimarisha chama chake na kukiweka juu huku akichukua tahadhari ya kuwa chama cha kidipromasia zaidi ya vurugu kwa kuwa anajua chama cha wastaarabu hakitaendekeza siasa za vurugu hata pale kinapoonewa.

  Ni kwa jinsi hiyo kwamba CHADEMA kimekuwa chama kitulivu ambacho hakirudishi baya kwa baya, ingawa yapo maonevu mengi ambayo kinafanyiwa na chama tawala, ikiwa ni pamoja na wizi wa kura mchana kweupe kama ilivyotokea kwenye uchaguzi wa 2005 na katika chaguzi ndogo za Tunduru, Kiteto, Tarime, Busanda na Biharamulo bila kusahau ile ‘rafu' ya kuenguliwa mgombea wao katika Jimbo la Mbeya Vijijini.

  Ni Mbowe aliyeanzisha mkakati, wakati wa uongozi wake, wa kuwatafuta na kuwakomaza vijana ndani ya CHADEMA, kama hawa kina Zitto Kabwe, John Mnyika na wengineo.

  Vijana hawa ambao aliwasaidia kwenda kugombea ubunge na kutoa upinzani mkali kwa wakongwe wa CCM, wamekuja kuwa hazina kubwa ndani ya chama na kuwa kivutio kwa vijana wengine ambao hivi sasa wanajiunga CHADEMA kwa kasi na kukifanya chama kionekane chama cha kizazi kipya, chama cha vijana na wasomi, chama kilichobeba maono ya vijana na wazee wakibaki kuwa washauri na watatuzi wa mambo magumu yanayoonekana kuleta shida, ambapo kamati ya wazee inatambulika kikatiba na mashauri yake hupewa uzito na vikao husika.

  Mbowe kafanya mengi ndani ya CHADEMA. Watanzania wasione tu chama hicho kikikua kwa kasi wakadhani kinaibuka kutoka ardhini.

  Hapana, kina mwenyekiti shupavu, mwenyekiti jasiri, mwenyekiti mbunifu, mtulivu hata pale anaposhutumiwa kwa shutuma za kijinga kabisa, mwenyekiti mwenye busara anayejali sana ni nini akiongee, wapi, mbele ya nani na wakati gani.

  Mwenyekiti anayekipenda chama kwa dhati ya moyo wake. Aliyekataa kulipwa na chama hata pale Kamati Kuu ilipopitisha kwamba sh milioni tano zitengwe kwa ajili ya mwenyekiti kila mwezi. Mwenyekiti anayetumia rasilimali zake kugharimia shughuli za chama.

  Ni mbunifu.
  Ndiye aliyebuni vazi la kombati ambalo hivi sasa limekuwa kama vazi rasmi la chama. Na hicho si kitu kidogo, kina ‘impact' kwenye siasa za CHADEMA.

  Alibuni pia kampeni kwa kutumia helikopta ambazo zimekuja kuonekana kwamba ni bei rahisi zaidi kwa kulinganisha na idadi ya mikutano ambayo hufanywa kwa siku na kama ungetumia magari kama yale mashangingi yanayotumiwa na CCM.

  Katika jumla ya
  sh milioni 753 zilizotumiwa na CHADEMA, kwenye kampeni za mwaka 2005, gharama za helikopta zilikuwa sh milioni 223 tu, zikijumuisha gharama za kuikodi, mafuta, uendeshaji, vibali na kodi za viwanja vya ndege.

  Helikopta huwezesha mgombea kuzunguka maeneo mengi kwa muda mfupi na husaidia kualika watu. Kuonyesha uzuri wake, hata CCM waliiga, ambapo waliitumia Kiteto na Tarime wakakodi mbili.

  Ni yeye aliyebuni mkakati wa CHADEMA ni msingi, ambapo baada ya kuonekana kutoleta matokeo mazuri sana,
  akaja na Operesheni Sangara, ambayo imeitetemesha CCM kwa kiasi kikubwa.

  Ndiye alileta wazo la kukizindua upya chama, wakabadili katiba ya chama, wakaongeza rangi za chama na kukipendezesha zaidi na akaja na kauli mbiu ya ‘CHADEMA TUMAINI JIPYA LA WATANZANIA'.

  Chama kilipozinduliwa upya Agosti 2006, kikaonekana kama kipya, kikaondoka na kasi kubwa zaidi huku yeye mwenyewe akiwa nyuma ya wabunge wake ambao hukaa nao kabla ya vikao na kupeana mikakati na hoja za kupeleka bungeni.

  Nilimwomba ofisa mmoja wa makao makuu ya CHADEMA, amwelezee Mbowe kwa maneno machache na alikuwa na haya ya kuniambia: "Mbowe ni mtu wa kanuni, husimama kwenye kanuni na hayuko tayari kumpendelea mtu yeyote anayekwenda kinyume cha kanuni zinazotuongoza hata kama ni rafiki yake kiasi gani.

  Ni mtu wa watu (social) anayeweza kuongea hata na walinzi na wahudumu wa chini kabisa na kutaniana nao, lakini asiyetaka mchezo kwenye kutekeleza wajibu wake.

  Huweza kujishusha sana kiasi kwamba wakati mwingine utamkuta
  tukiwa naye pamoja tukitoa photocopy za nyaraka za chama na yeye akishiriki hata kubana karatasi pamoja (stepling).

  Si ajabu basi kuona chama tawala kikimshambulia sana Mbowe maana kinajua ni wapi kaitoa CHADEMA na ni wapi anaweza kuifikisha.

  Propaganda zote za ukabila na mengineyo zinalenga kumdhoofisha na kuidhoofisha CHADEMA, lakini Watanzania washukuru kwamba huyu ni kamanda asiyerudishwa nyuma na propaganda za mafisadi na hivyo wategemee CHADEMA itawatoa kimasomaso!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  What is your beef?
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ina maana huyu Mwandishi pamoja na kuweka maelezo yote haya ameshindwa basi kuweka huo wasifu kwa kuonesha Mbowe amekata madarasa kwa kiasi gani?
   
 5. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Jasusi.

  Mwandishi kaandika mambo mengi ya kupika sio kweli mfano anasema kuwa MBOWE ndio alimtafuta na kumkomaza Zitto.WAKATI kwenye mahojiano mengi tu Zitto anasema yuko Chadema toka mwaka 1992.na Mbowe kapata uenyekiti 2004.

  yapo mengi ambayo anaonesha kuwa kaandikiwa na Mbowe au ni kujipendekeza kwake. swali la Msingi hajasema kuwa Mwenyekiti huyu kasoma shule gani ana elimu gani?wasifu gani wa mwenyekiti wa Chama ambao hauelezi elimu ya Mwenyekiti?

  kama Mbowe mpenda demokrasia kwanini hakumuachia Zitto nae awe Mwenyekiti kwa miaka mitano?mara Mbowe hapatokani alikuwa nje ya nje jee kwanini asimtumie email au sms?ili kupata ridhaa na ukweli wa habari kama hizo za ubatizo ambazo hazijathibitishwa na Mbowe mwenyewe na baba yake ameshafariki.ilitakiwa habari kama hizo zitoke kwake Mwenyekiti.angemtumia email kuulizwa maswali hayo.

  kila jambo Mbowe ndiye aliyebuni jee sio KAMATI KUU ya Chadema ndio inayoamua kuwa kuwe na Helkopta au operesheni Sangara n.k?basi hakuna haja ya kuwa na Chama kama kila kitu ni Mbowe.

  kama maendeleo ya Chadema huwezi kuandika na ukawaacha watu kama KABURU AMANI.pamoja na yote Kaburu anamchango mkubwa Chadema.mtu kama Zitto posible alipata ushawishi mkubwa toka kwa Kaburu.
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Maswali yako mengi sana kashindwa kuyaandikia majibu yake.ETI MBOWE NDIYE ALIYEKUWA KIJANA MDOGO KULIKO WOTE WA CHADEMA 1992.SWALI ALIFANYA UTAFITI HUO WAPI NA LINI? NAMPA CHANGAMOTO KUWA ZITTO KABIWE ALIJIUNGA CHADEMA MWAKA HUO HUO 1992.JEE ZITTO NA MBOWE NANI MKUBWA?

  ANATAKA KUTUDANGANYA KUWA MBOWE HAKUWA NA JINA KWA MIEZI MITATU HADI DECEMBER 1961?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mchango wa Kaburu ulikuwa ni kukimbilia CCM kuungana na Hiza Tambwe!
  Hata Mtemvu alikuwa na mchango TANU lakini sijaona anasifiwa.
  Bado nauliza what is yr beef? Take up the issue na mwandishi wa makala.
   
 8. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huu ndio mchango wangu,

  Hapana hatudanganyi kuhusu Mbowe kuwa au kutokuwa na jina kwa miezi mitatu.Kule uchagani ni kawaida mtoto anapozaliwa anapewa jina la kinyumbani.Kwa mfano Ndefanyakasi.Atatumia jina hili hadi abatizwe,mfano Peter.Mtoto huyu ataitwa Peter Ndefanyakasi JinaLaUkoo.Kuna tofauti ya kubatizwa na kuwa na jina.Mwandishi anazungumzia kubatizwa.Hazungumzii kutokuwa na jina.Hivyo Mbowe alikuwa na jina la kinyumbani kwa miezi hiyo mitatu na baadaye ndio akabatizwa na kuitwa Freeman.......

  Hayo mengine Mmmmmh!
   
 9. Painstruth

  Painstruth Member

  #9
  Sep 24, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wala hasemi kuwa ni mtoto wa Nyerere?
   
 10. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #10
  Sep 24, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi amesema Mbowe ndiye aliyekuwa MUASISI wa chama mwenye umri mdogo kuliko wote. Ukweli ndio huo. Mwandishi ameongelea waasisi wa chama na sio wanachama. Kama unamfahamu muasisi wa chama aliyekuwa na umri mdogo kuliko Mbowe ni bora ukamtaja.

  Kwanza kumbuka Mwenyekiti wa hiyo Kamati Kuu ni Mbowe. Hivyo unapoipongeza Kamati unaipongeza kwa kufanya kazi chini ya Mwenyekiti wake.

  Halafu kama mwanachama mmoja ni mbunifu ndio chama kisiwepo? Ina maana chama kinakuwepo tu kama watu wote ni mazezeta? Hapa yameandikwa maelezo kuhusu Mbowe na sio maendeleo ya chama. Kama unampenda sana Kaburu basi na wewe andika makala yako ya kumsifia.
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Acha uzushi wewe maana hata huyu mwandishi siyo KIBANDA, Umezoea kuwa kila kitu KIBANDA, Huyu ni SAMSON MWIGIMBA, na Tena hujiandae kupapambana naye kwenye ubunge Kupitia CHADEMA!! Kwani kuna nini kama gazeti likimsifia MBOWE, Sasa sio Ukweli, Acha mambo ya ajabu kama haya na uzushi kama huu hapa
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kanda2 vp tena mbona Mengi anatumia vyombo vyake kujisifia!
  Mbona Rostam nae anatumia vyombo vyake kujisifia nini cha ajabu hapo?
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu naona kuna ujumbe unataka kuutoa ila unazunguka zunguka tu. Sema nini kinakuudhi kuhusu Mbowe au kwenye hii makala. Au kipi kasema uongo na utuwekee ukweli unaoujua. Jamaa kaaamua kumsifia Mbowe kama ambavyo wewe pia waweza kuandika makala ya kumponda na kuipeleka kwa Mhariri wa hili gazeti au Uhuru.

  Hayo mengine ni kukosa hoja. Sehemu zote kushindwa kunachukulia kama udhaifu wa Mkubwa wa chama au taasisi husika. Kwa hiyo hata mafanikio yanapeleka safa kwake. Mbona Tz tunasema Uhuru uliletwa na Nyerere. Je, alifanya kazi zote peke yake? Na sasa tunamwita Baba wa Taifa, mbona Bibi Titi hatumwiti Mama wa Taifa? Kama una chuki binafsi basi andika makala tu badala ya kulalamika!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ulitaka aandike mawazo yako? Yeye kaamua kuandika hayo yaliyougusa moyo wake. Ongeza haya unayoyasema kama unataka. Hawezi kuandika kila kitu na mawazo ya kila mtu.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naona Kanda2 unataka kuleta majungu tu na si kingine waache watu wafanye kazi zao kama waandishi maana naamini huyo mwandishi wala hajafuatwa na Mbowe amsifie na wala Mbowe usikute hajui ni nn kimeandikwa.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kweli siasa ni ngumu ..
   
 17. N

  Nanu JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kuna cha uongo kilichoandikwa mtu akanushe na sio kubeza tu kwa sababu ya kubeza. Nawe fanya kazi ionekane uandikwe na sio kuwa radical wa propaganda tu. Kama Kaborou anacho alichofanya yaweke kwenye makala. Hapa mwandishi katuleletea wadhifu wa Mbowe wa utendaji wake kisiasa na wala hakuwa anazungumzia wasifu wa jumla (Carriculum Vitae, CV).

  Amemnyambulisha katika uwanja wa siasa tu. Ukweli ni kwamba amefanya kazi kama ilivyoandikwa kwenye makala haya. Kama kuna uongo basi nyambulisha na utueleze kwa kuweka bayana kila kitu. Mnyonge Mnyongeni haki yake mpeni.
   
 18. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa wasifu huu MBOWE anastahilii pongezi na kuwa mfano wa kuigwa kwa wale wote wanaopenda mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

  Ameonyesha anaweza na vijana wengi wakipewa nafasi na kuzungukwa na watu wanaofaa WANAWEZA.

  YES WE CAN
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Kuna watu humu jamvini wakiona maandiko yeyote yanayojaribu kukubali juhudi za Mbowe katika kujenga Chama na Taifa hili au kumkubali kuwa ni kiongozi thabiti wanatamani wanywe sumu. Mwandishi wa makala hiyo kaeleza muono wake kwa Mbowe ukoje, sasa mjadala wa nini tena? mara elimu yake, mara hakuwa kijana wakati wa uasisi wa chama nk.
  Kumbeza Mbowe kwa aliyoyafanya hadi sasa ni uendawazimu wa hali ya juu kabisa. Wangapi wana magunia ya shahada na tumewapa nafasi za kututumikia na wameshindwa kuthubutu kufanya kama sio kuharibu kabisa? Kwani hawafahamiki?
  Chuki binafsi na Mbowe tusizilete Jamvini, Ni kweli yaliyofanyika Chadema katika kipindi hiki yamewahusisha wengi, lakini yeye ndio Jemedari lazima apongezwe kwa uongozi wenye Tija. Jeshi japo liwe imara kiasi gani kama kamanda wake ni OVYO haliwezi kupata ushindi.
  KAZA BUTI MBOWE, ILI JINA LAKO LIINGIE KTK VITABU VYA HISTORIA KAMA MPAMBANAJI DHIDI YA UDHALIMU WA KIZAZI HIKI
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kanda2 ulimsikia yule kiongozi wa NCCR-Mageuzi alivyo chemka juzi?
  Kweli wale ndo walio ua chama cha NCCR mpaka leo hakipo kwenye chat wao wanadai lengo lao ni kusindikiza.
   
Loading...