Salama jamani.
Huu mwaka 2022 kiboko naona walimu watakuwa wamechoka sio kwa hali hii tunayoenda nayo.
Nahic hata wanafunzi nao watakuwa hoi bin taabani.
Toka January hakuna kupumzika mpaka leo. Hapa kati mwezi wa nne kidogo kulikuwa na vimapumziko vya hapa na pale lkn kifupi ngoma imekuwa ngumu mwaka huu.
Na inaelekea hii ngoma itadunda hadi mwezi wa saba mwishoni naona walimu watakuwa hoi.
Kupumzika ni muhimu ili kujenga afya ya mwili na akili.
Basi niwaombe walimu kitu ..Kuna kipindi waziri mmoja alitoa tamko kuwa wakati wa likizo wanafunzi wapumzike pamoja na walimu.
Kusiwepo na masomo ya ziada watoto waende nyumbani kupumzika ili kulinda afya zao, vile viratiba mnavyojiwekea walimu wakati wa likizo vinatakiwa vife ili kuwezesha wanafunzi na ninyi wenyewe mpumzike.
Kuna viratiba vya usafi kwa wanafunzi pia kuna viratiba vya masomo kwa baadhi ya madarasa.
Sijui inakuwaje wakati wa likizo lakini bado unawaona wanafunzi wanaenda shuleni na mafagio wanaenda kufagia.Sijui maana ya kupumzika hapo.Maana ya likizo ni kuwa hutakiwi hata kuliona eneo lako unalofanya kazi au kusoma.Yaani unakuwa 'free mind' hata dhararu wakati mwingine hazitakiwi,likizo ni likizo jamani.
Nenda kapumzike ufikirie na mambo mengine. Pumzisha akili kidogo na yale mambo ya kuamka asubuhi kurudi jioni au usiku.
Sasa mwaka huu inaenda robo tatu mwaka shule hazifungwa ni hatari kwa afya. Ni muhimu kupumzika wapendwa.
Kuna baadhi ya shule unakuta wanafunzi wanaingia asubuhi saa moja wanatoka saa 11 jioni, wengine saa 10 wengine saa 9.Sijui kama kuna wa mpaka saa 12.
Na sijui kama wanaelewa au hilo nawaachia wenyewe.