Mwezi wa saba, mwezi wa mateso, karaha, mauji , chuki kila baada ya miaka mitano

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana jamvi,

Kila baada ya miaka mitano, mwezi wa vituko unaanza, tunaanza na mipango ya bajeti mpya ambayo hatujui atayeitumia ni nani? Au atayeisimamia ni nani, tukiwa kwenye ombwe LA uchaguzi ni shuhuda nyingi tutazipata baada ya kura za maoni, itatokea chuki kubwa kati ya wapenda madaraka na wale wapenda kuongoza, chuki itakolezwa na vimbwanga vya kunyambuana na kutoleana siri nyeti zenye malengo ya kuharibiana.

Tayari CCM wametoa number za whatsap kuripoti atakayejipitisha kwa malengo ya rushwa. Wapo wasioridhika wakaama chama kwenda kuitwa makapi, wapo watakaobaki na kuitwa oilichafu. Vita itaamia kuviziana na kutoana ngeu. Kama Yale tuliyoyaona kwa Ndungai akimkita kwa kishindo mgombea mwenzake fimbo.

Vyama vitaanza kutumiana mamluki, uwezekana wa kumwagiana tindikali in mkubwa. Wale waamiaji toka vyama vya upinzani, wataanza ushindani na wenyeji, wenyeji hawatakubali hivyo chuki za kichochezi za kuitana wasaliti zitawakumba mpaka watajuta kwanini waliama maana watakuwa hawaaminiki tena kwenye jamii na wengi washapoteza kazi, hivyo lazima mapigano hayatakosa.

Mauaji uenda yakatokea kwani safari hii hakuna nguvu ya pesa. Hivyo wapendwao lazima wamalizwe mapema.

Polisi ina wakati mgumu kwani wengi wajiingiza kwenye siasa zaidi badala ya taaluma yao. Hivyo kuna watu watapendelewa zaidi Hivyo kuleta kutoaminika kwenye jamii. Wakati wa ufunguzi wa kampaini kutekana na kujeruhiana kutakuwepo sana miongoni mwa washindani bila kujali wapo chama gani ilimladi tu wanataka madaraka.

Hitimisho , mwezi ujao, polisi, wakae mguu sawa kukabiliana na matukio, waweke siasa kando, walinde watu na Mali zao. Polisi waweke number za Whatsapp za kutuma matukio ya kihalifu.
 
Back
Top Bottom