Mwezi wa nane sasa baada ya mke kubakwa, nafanyaje naye mapenzi?

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,266
2,870
Mashaka(si jina lake kamili) alivuta kiti pembeni yangu.ilikuwa ni jioni baada ya kutoka kazini tumekaa baa flan maeneo ya sinza. Mchana alinipigia simu nikiwa ofisini na kuniuliza kama ningeweza kuonana naye jioni nikitoka kazini. Ilikuwa ni Ijumaa tarehe 23/12/16 . nliwah kutoka kazini so haikuwa na shida kuonana naye. Akanielekeza nimkute wap maana yeye alikuwa likizo.

Mashaka alianza kunisumulia kuwa ni miaka 5 sasa yupo na shemeji yangu yaani mkewe. Na hapo katika waliyumba sana kiasi hata gari wakauza wakawa hawana usafiri. Kipindi hicho walikuwa wanakaa tabata segerea. Mkewe anafanya kazi bank posta na yeye anafanya kazi serikalini.

Mkewe ni mnywaji kama naye pia alivyo ingawa mara nyingi amekuwa akimsisitizia mkewe asinywe pombe ikiwa hawapo wote.

Siku ya tukio mkewe anasimulia alikuwa ametoka kazini late sana saa 12. Akiwa amesimama pale mnazi mmoja likaja gari noah ambalo lilikuwa lina abiria 2 wa kiume ndani na likatangaza kuwa segerea nauli tsh 2000 akapanda yeye na dada mwingine mmoja.

Hakuwa na shaka maana aliona kuna abiria wengine mle ndani na mwingine alipandia pale hivyo kuwa na abiria wa nne nyuma na mbele mmoja.

Anasema walipofika tabata matumbi abiria wa mbele alishuka na waliendelea mpaka tabata aroma yule wa kike akashuka. Hivyo akabaki yeye na wanaume wawili. Yule mmoja akawambia ampishe akae karibu na mlango maana yeye anashuka kituo kifuatacho. Mke wa mashaka akakaa katikat.

Toka hapo hakumbuki kilichotokea ispokuwa asub yake alizinduka baada ya kumwagiwa maji akiwa amezungukwa na watu kadhaa amefunikwa khanga tu. Aliibiwa simu na poch yake ,akavuliwa nguo na kubakwa.
Wasamalia wema waliomba ipigwe simu kwa mtu wake wa karibu na namba aliyoikumbuka ni ya mumewe.alimpigia. mashaka usiku wote hakuwa amelala akihangaika kwa ndugu na jamaa mpaka saa 8 usiku alipopata msg kuwa " nitalala msibani simu imeisha charge ntakutafuta kesho" ile simu haikupatikana tena.

Asub ndo anakuja kukuta mkewe yupo vile. Amebakwa na kutupwa mtaroni.alikuwa na majeraha kidogo kichwan.alipelekwa hosp wakamchek na taratibu zote.akawaambiwa akapime baada ya miezi mitatu.

Mashaka anasema toka siku hiyo ameishiwa hami ya kufanya mapenz na mkewe. Walala wote lakin hapati hamu. Tukio la mkewe kubakwa linamjia kila mara. Anashindwa aamini lip kati ya aliloambiwa na mkewe au waswas wake pia kuwa pengine mkewe alichukuliwa kwenye bar maana ni mtu anayekunywa sana.

Lakin mbal na hilo.alishawah mwonya mkewe kuwa ni bora atumie tu Public Transport kwa kuwa kumekuwa na wizi sana miaka hii na asiamini kabisa watu wa magari. Mkewe alimjibu tu kuwa yeye hataki shida. Kama vipi amnunilie gari mbona wanaume wenzie wananunulia magar wake zao.

Sasa mashaka anaomba ushauri afanye nini. Maana picha mkewe kuingiliwa na wanaume wa tatu haimtoki kichwan. Pamoja kuja kuonekana mkewe hajaathirika(HIV) Lakini kisaikolojia Mashaka ameathirika sana.

Hii ni habari ambayo alinihadithia mashaka ambaye hili si jina lake halisi. Ambaye kwa sasa anaishi sinza maana ilibidi wahame segerea kutokana na mkasa huu kufahamika kwa watu
 
Dah pole yake ila huo nimkasa so sioni haja yakumuhukumu muhusika, chamsingi ajitahid kutafuta njia mbadala ili ayasahau namaisha mengine yaendelee
 
daahh!haya mambo tuyasikie tu kama hivi unasimuliwa Ila yakikukuta...

yanaumiza sana!

mi nashauri amsamehe na kama anadanganya Huyo mke atajua yy na Mungu wake

Ila kwa picha ilivyo kuna uwezekano pombe zilimzidi walimtoa baa hao washikaji maana kwa kazini Segera ninavyojua mie hiyo gari isingekua na abiria wanne..
Hapo kachemka Huyo mama!
 
Siku zote wema ni Akiba,
Kama huyo mke wake alikua mwema kwake na anamuheshimu mme wake kabla ya kubakwa basi Bwn Mashaka hana budi kumsamehe, lakini km huyo mwanamke alikua Jeuri na hakuwahi kumsikiliza na kumuheshim mme wake basi huu ndiyo wakati wa bwn Mashaka kumchinjia baharini.
 
daahh!haya mambo tuyasikie tu kama hivi unasimuliwa Ila yakikukuta...

yanaumiza sana!

mi nashauri amsamehe na kama anadanganya Huyo mke atajua yy na Mungu wake

Ila kwa picha ilivyo kuna uwezekano pombe zilimzidi walimtoa baa hao washikaji maana kwa kazini Segera ninavyojua mie hiyo gari isingekua na abiria wanne..
Hapo kachemka Huyo mama!
kwani issue ni kusamehe? jamaa stress tu zinamtesa hataki kiporo eti
 
mimi ndio maana nikiwa narudi toka safarini lazima nitoe taarifa kwa mke kwmba narudi sitaki kufumania nikateseka bure!mkiniona boya poa tu ila mimi huwa nampa nondo tu ili ajue kwamba kuchepuka sio dili!kwanza haina raha unafanya kwa uoga maradhi kibao ukifanya mchezo wajukuu utaskia kwenye bomba
 
Kama umefunga nae ndoa ya kanisan kumbuka Kiapo cha ndoa yako(kuvumiliana natoka shida na raha ,magonjwa na dhiki) pia wanaume hebu tuwe na Moyo wa msamaha,kuiona unakumbuka kosa alokufanyia mtu ujue hujasamehe Sawa sawa.Hata yesu alisema'baba wasamehe kwan hawajui watendalo'Nawe msamehe mkeo na umpe haki yake ya ndoa.
 
Chamsingi hapo awe jirani zaidi na mkewe..mambo mengne huondoka taratibu. Apate pia mda wa kutoka out hasa nje ya jiji atarudi tu ktk khali ya kawaida
 
Punguza feelings hzo. Usimfanye mke wako awe na mawazo zaidi. Unauwezo wa kurudi ktk khali ya kawaida.
 
Yn haya matukio ni mengi..nna watu wawili nawafahamu tena wake za watu walifanyiw hivi hiviii...sijui ht waliyahandle vipi haya.... magari yakuitiwa sijui buku buku 2 sio mazuri.
..na pia wanawake ulevi hautupendezi kabisa..
Mshauri awe close na mkewe..asali sana...ipo siku
INGAWA NI NGUMU AISEE..LILE TENDO LINAHITAJI AMANI YAMOYO
 
mwanamke kibur na hakumsikiliza mumewe Labda n kwa sababu ya kipato na kaz anayofanya.

Mwanamke kunywa pombe haon aibu....?

Pole mashaka
 
Pole kwao mashaka na mkewe, aende hospital akapate ushauri inaeza msaidia
 
Back
Top Bottom