Mwezi wa kwanza unaisha, siku 30 zinaenda kukamilika mwaka mpya 2020. Uzoefu mpya - China

impelle

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
832
1,100
Mwaka mpya 2020, ni mwaka umeandamana na matukio makubwa ya kihistoria kama Marekani kumuua kwa maksudi Kamanda mkuu jeshi la mapinduzi ya Iran J. Soleimani, kutunguliwa kimakosa kwa ndege ya abiria ya Ukraine huko Iran, kushambuliwa kwa kambi za kijeshi za marekani huko Iraq na kuzusha hofu kali juu ya kutokea kwa vita ya tatu ya dunia.

Tukio la pekee la Prince Harry kuikacha kasri ya kifalme huko nchini kwao Uingereza ili kulinda penzi lake kwa dada mrembo Meghan Markle, hukumu ya siku 6 ya Rais wa Marekani inayoendelea kwenye bunge la Seneti. Mlipuko wa virusi hatari aina ya Corona Virus hapa China, kifo cha ghafla ya mchezaji maarufu wa ligi ya NBA Kobe Bryant na bintiye Gianna (Gigi) kilichotokana na ajali ya helikopta waliyokuwa wakiitumia kusafiria na mengine.

Huko nyumbani, tukio kubwa ni lile la Mh. Rais Magufuli kumbaini mwanafunzi wake aliyekuwa anaigiza anafanya kazi pale kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani Mh. Kangi Alphaxad Lugola, kusainiwa kwa mkataba wa madini wenye kuzingatia maslahi ya taifa, na mengineyo.

Niongelee kidogo juu ya tukio hili linaoloendelea hapa nchini China na uzoefu ninaoupitia,

Corona virus wanaaminika kutoka kwa Wanyama wa mwituni kama Panyabuku, Popo, Nyoka aina ya kobra waliokuwa wakiuzwa na wachuuzi kwenye soko la vyakula katika jiji la Wuhan. Wanasayansi wa kachina bado wanatafuta chanzo sahihi cha hawa virus. Ugonjwa huu,unafanana na MARS na MERS ambao uliwahi kutokea miaka ya nyuma ingawa haikuwa serious kama hii.

Ugonjwa wa Corona Virus ni ugonjwa jamii ya mafua ambao unaenezwa kwa njia ya hewa kupitia kugusana, kukohoa, kupenga kamasi, kushikana mikono, kubusiana, kushika kitu chenye maambukizi kisha kujishika machoni, mdomoni n.k imegundulika kwamba muathirika anaweza kukuambukiza kama utamkaribia ndani ya mita moja.

Mara virusi hawa wamuingiapo mtu, anaweza kukaa mpaka siku 14 bila kuonyesha dalili, ingawa katika kipindi hicho hawezi kuambukiza. Ugonjwa pia unaua sana kwa watu wenye kinga ya mwili ndogo na makundi yanayoathirika zaidi ni wazee na watoto. Muathirika akibainika mapema, uwezekano wa kupona upo.

Huu ugojwa sasa umesambaa maeneo mengi duniani, mataifa kama Marekani, Canada, Australia, Ufaransa, Thailand, Japan, Korea ya kusini,Mexico, Taiwan na kwa bara la Afrika inasemekana Ivory Cost

Mpaka leo watu 80 wamefariki kutokana na huu ugonjwa, zaidi ya watu 3000 wakiwa tayari wamebainika na ugonjwa na zaidi ya 30,453 wakichunguzwa kama wana maambukizi na watu 46 hali zao zikitengemaa (recovered).

Kutokana na kwamba huu ni msimu wa sikukuu za mwaka mpya wa kachina na hivyo wachina wengi kutoka maeneo mbalimbali husafiri kurudi kwao kwa ajili ya kuungana na familia zao kuadhimisha mwaka mpya hivyo maambukizi yataendela kuongezeka.

Serikali chini ya CCP imeamua kufunga kabisa jiji la Wuhan na baadhi ya majimbo pia shughuli nyingi zimefungwa.Serikali inajenga hospital kubwa ya dharura ndani ya siku sita kwa ajili ya kuhudumia waathirika wa Coronavirus.

Maeneo mengi wanarecord body temperature ambapo ikigundulika body temperature ni kubwa, wanakuweka chini ya uangalizi maalumu.

Dalili za ugonjwa ni kama:
  • Mafua makali
  • Homa
  • Kupumua kwa shida
  • Kifua kuuma
  • Mbavu kuuma
  • Kupiga chanya mara kwa mara
Jinsi ya kuzuia:
  • Kuepuka kukaa kwenye mikusanyiko
  • Kuepuka kusafiri hasa kwenda kweny maeneo yaliyo athirika
  • Kuishi kweny mazingira masafi
  • Kuruhusu hewa ndani
  • Kuepuka kula nyama za porini nk
  • Kuvaa vifuniko vya uso maalumu
Jimbo ninaloishi mpaka sasa kuna case 6 zimeripotiwa, na huenda zikaongezeka baadaye.

Mimi nikitazama kwenye vyombo vya habari, hali inaogopesha sana hasa jinsi virusi anavyosambaa kwa kasi sana, rate ya watu wanaokufa na waopona, kweli hali inatia wasiwasi sana.

Ninaendelea kuishi maisha ya kawaida kabisa, kwa vile nina chakula cha kutosha kukaa tu chumbani kwangu kwa miezi miwili mbele, basi sina mpango wa kutoka nje. Kwenye hili jingo tupo foreigners zaidi ya 50 na mamlaka zinatuelekeza kuepuka kutoka nje, na kama ukitoka basi inabidi kutoa taarifa kwamba unaenda wapi, kufanya nini, unakaa muda gani.

Maisha hayapo kawaida baada ya mlipuko wa hiki kirus hii kwangu ni uzoefu wa kipekee kabisa. Maisha hayana uhuru tena, ni kusikiliza viongozi wanasemaje.

Kuna baadhi ya maeneo, vyakula vimeanza kuadimika na hata vinavyopatikana ni ghali sana, shughuli nyingi sana zimesimama (ingawa ni kawaida kipindi hiki cha sherehe za mwaka mpya), hapa kwetu tunarecord body temperatures kila siku, wenzetu waliokuwa wamesafiri kwenda maeneo mbalimbali kwa ajili ya utalii au kusalimia marafiki, wakirudi wanatengwa kwa muda wa wiki mbili.

IMANI yangu, kwa kuchukua tahadhari ya juu tutaendelea kuwa salama.

Serikali ya China kupitia chama kikuu CCP wanafanya kazi kubwa sana kuhakikisha wanashinda hii vita. Ninashuhudia viongozi wa ngazi zote wanavyopambana kizalendo kutokomeza hiki kirusi, watumishi wa afya wamejitoa kikamilifu kiasi cha kurisk maisha yao ili kuokoa maisha ya wengine (mpaka sasa daktari mmoja amefariki kutokana na corona virus).

Wanajeshi pia wako mstari wa mbele kuishinda hii vita, Walimu wapo karibu na sisi, wengine wamekuja kuishi na sisi. Wapo wananchi wazalendo waameamua kuruhusu hotel zao kutumika katika kipindi hiki cha dharura katika maeneo ambayo maambukizi ni makubwa (Hubei province), Viwanda vinazalisha kwa kujitolea materials zinazohitajika mfano musks, disfectants n.k

Kwa sababu huu ni msimu wa baridi wanategemea kwamba jinsi hali ya joto linavyoongezeka basi ugonjwa utapungua kusambaa maeneo mbalimbali.

Ninachoendelea kujifunza ni kwamba Uzalendo, Umoja, Kutii mamlaka ni mambo muhimu sana katika kuokoa taifa kutokana na matatizo tunayokumbana nayo inaweza isiwe Corona virus lakini ukawa ni Umaskini, Magonjwa, Ujinga, kujiletea maendeleo n.k

Taarifa zinatokana na vyanzo mbalimbali vya habari
 
Tutakufa tu hata kama hiki kirusi hakitafika ktk nchi hii ya uncle jiwe mavumbini tutarudi,

Mhm kujiandaa kabla ya kifo.
 
Back
Top Bottom