Mwezi mwandamo, Zuhura, Utarid zote angani Magharibi

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Zuhura, Utarid na Mwezi hilali utaziona jirani angani upande wa magharibi karibu na upeo mara baada ya machweo. Picha inaoensha mpangilio wao kuanzia leo 21 Mei hadi Jumapili 24 Mei, zikibadilisha nafasi siku hadi siku. Siku ya Ijumaa 22 Mei sayari mbili, Zuhura (Venus) na Utarid (Mercury) zitonekana jirani kabisa angani. Hii ni fursa ya kipekee kuweza kuona sayari ya Utarid kwa macho ingawa kawaida inafunikwa na mwanga mkali wa Jua.

Jumamosi Mei 23 Mwezi mwandamo unaingia anga ya jioni na unaweza ukaonekana jirani na upeo kuashiria Iddi, na siku ya pili yake Jumapili 24 Meu utakuwa juu zaidi na hilali kubwa ya kutosha na kuonekana kwa urahisi kwa hiyo ujitayarishe kutafuta Mwezi mwandamo kuanzia Jumamosi.

Upeo wa magharibi ukiwa wazi bila mawingu Mwezi mwandamo unaweza ukaonekana jioni ya Jumamosi inapoigia giza kiasi kabla Mwezi kuzama saa 12:45. Mwezi utakuwa juu kidogo ya sehemu ambapo Jua limezama upeoni na pia utawa chini ya sayari Zuhura.

Mabadiliko siku hadi siku ya Zuhura, Utarid na Mwezi Hiliali mwandamo tarehe 21 hadi 24 saa ma...png


Mwezi Mwandamo wa Iddi 23-24 May 6.30pm.png

Ukiangalia Zuhura kwenye darubini utaona kuwa ina umbo la hilali wakati huu. Baada ya siku chache Zuhura itapotea chini ya upeo wa magharibi ifikapo mwisho wa Mei. Zuhura imekuwa ikionekana iking'aa vikali kwa miezi 8 iliyopita kama Nyota ya Jioni tangu mwaka jana Septemba 2019. Kuanzia mwanzo wa mwezi ujao Juni, Zuhura itaanza kuonekana katika anga ya asubuhi na kung'aa kama Nyota ya Asubuhi na kubaki anga za mawio kwa miezi mingine 8.

Zuhura nayo hilali.png
 
KUMBE VENUS NDIO ZUHURA?

AHSANTE KWA ELIMU YA NYOTA/UNAJIMU/JIOGRAFIA MKUU
 
Back
Top Bottom