Mwezi Mwandamo Agosti 21 Kuashiria Kupatwa Kwa Jua = August 21 New Moon Brings a Total Solar Eclipse

Uliweza kuona hilali ya kwanza siku gani?

  • Jumatatu Agosti 21

    Votes: 0 0.0%
  • Jumanne Agosti 22

    Votes: 0 0.0%
  • Jumatano Agosti 23

    Votes: 0 0.0%
  • Sikuweza kuona

    Votes: 1 100.0%

  • Total voters
    1

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
English version - Click here:
August 21 New Moon Brings a Total Solar Eclipse


Kawaida, kila baada ya kupatwa kwa Mwezi, kupatwa kwa Jua hufuata wiki mbili baadaye. Na hivyo ndio itatokea baada ya kupatwa kwa Mwezi tuliyoshuhudia hivi majuzi tarehe 7 Agosti. Wiki mbili kamili baada ya Agosti 7, kutatokea kupatwa kwa Jua tarehe 21 Agosti. Ila, sisi hapa Tanzania hatutaweza kuona tukio hilo moja kwa moja maana litatokea mbali, huko Marekani.

Tukio la kupatwa la tarehe 21 Agosti ni kupatwa kamilifu kwa Jua ambapo Mwezi hufunika sura ya Jua. Watu wachache sana hubahatika kuona Jua lote likifunikwa kwa vile inatakiwa uwe ndani ya eneo la kilomita 100 ambamo, kwa dakika tatu, mchana hugeuka kuwa usiku. Kwa tukio la Agosti 21, eneo la giza litatengeneza mkanda mwembamba utakata nchi nchi nzima ya Marekani kutoka ukingo wa magharibi hadi wa mashariki

Kupatwa kwa Jua hutokea wakati Mwezi unkuwa kati (siyo katikati) ya Jua na Dunia na magimba yote tatu yamepangika kwa mstari ulionyooka. Kupatwa kamili kunatokea kwa sababu Mwezi unaweza kuufunika Jua barabara. Ukubwa wa Mwezi na Jua sawa sawa kabisa kwa jinsi tunavyoziona kutoka hapa Duniani. Hasa ukiwa umebahatika kuuangalia Jua kwa kutumia miwani maalum ya Jua, utatambua kuwa Jua linoonekana kubwa kama vilie Mwezi.

Ingawa kihalisi Jua ni kubwa sana, yaani mara 400 kuliko Mwezi, Jua pia lipo umbali wa mara 400 kuliko ule wa Mwezi kutoka Duniani. Hivyo kipenyo cha Jua na Mwezi hufana kabisa, yaani ni nusu nyuzi.

Utakumbuka tukio la Kupatwa Kipete kwa Jua ambalo lilitokea kusini mwa Tanzania tarehe mosi Septemba, ambapo mduara wa mwanga ulibaki ukionekana katika mzingo wa Jua. Hii inamaanisha kwamba ukubwa wa Mwezi ulikuwa mdogo kidogo kuliko ule wa Jua. Hii ilitokea kwa vile siku hiyo Mwezi ulikuwa mbali kidogo kuliko umbali wa kawaida, hivyo Mwezi ulionekana kuwa mdogo kuliko Jua na kuacha mzingo mviringo wa moto wa Jua.

Mchoro wa Mpangilio wa Kupatwa kwa Jua.jpg

Watu wachache huona tukio la kupatwa kwa Jua ukilinganisha na wale wanaoweza kuona kupatwa kwa Mwezi. Mwezi ni mdogo kuliko Dunia, hivyo kivuli chake ni kidogo, na sehemu ndogo tu ya sura ya Dunia hufunikwa na kivuli wakati wa kupatwa kwa Jua. Pia, theluthi moja tu ya Dunia ni ardhi kwa hiyo sehemu ambazo watu tukio la kupatwa kwa Jua zinapungua zaidi. Ukilinganisha hali hii na ile wakati Mwezi unapatwa, utaona kuwa kivuli cha Dunia ni kikubwa sana, kwa hiyo Mwezi unweza kubaki ndani ya kivuli cha Dunia kwa muda mrefu na sehemu nyingi za Duniani wataona Mwezi uliopatwa.

Mimi mwenyewe nimeshuhudia kupatwa kamili kwa Jua. Mara ya kwanza ilikuwa Lembeni, kaskazini mwa Tanzania tarehe 16 Februari 1980, na ya pili ilikuwa huko Lusaka, Zambia tarehe 21 Juni 2001. Kwa matukio yote mawili ili bidi ni safiri ili kufika ndani ya mkanda wa giza kamili na kuweza kuona Jua likipatwa kamilifu.

Ni shuhuda ajabu kuweza kuona vivuli vikigeuka kuwa hilali na mchana kukgeuka kuwa usiku, hata ndege na wanyama wakianza kurudi nyumbani kwao. Kubwa zaidi ni kuweza kuona anga ya ajabu inayoizunguka Jua, ambayo inaonekana kwa dakika tatu tu wakati Jua limepatwa kamilifu

Pale Marekani, ambapo nchi nzima watashuhudia kupatwa kwa Jua Agosti 21, na hasa sehemu ambazo litapatwa kamilifu, wanaastronomia wamewatayarisha watu kuangalia Jua kwa usalama na kufurahia tukio la ajabu, na wanafunzi kutumia nafasi hii kujifunza elimu ya anga za juu. Matayarisho makubwa yalianza kufanyika miaka miwili kabla ili kuwahimiza watu kusafiri kwenda katika maeneo ya kupatwa kamilifu kwa Jua na kuliangalia kwa usalama kwa kutumia miwani maalum. Kwa wanasayansi, tukio la kupatwa kamilifu kwa Jua ni nafasi pekee ya kupima na kuchunguza tabia za anga ya Jua maana hakuna njia nyingine kuiona kwa uwazi hivyo.
ANGA YA JUA - Helmet_streamers_at_max=.jpg

Tukio la Agosti 21 limekuja kujulikana kama “Tukio Kabambe la Kupatwa Marekani” na hiyo imeenea duniani kote kwa mtandao. Kuna habari potofu pia zinasambazwa kwamba Dunia nzima litakuwa na giza siku hiyo ya Agosti 21, ambayo si kweli hata kidogo. Giza litaonekana katika mkanda mwembamba utakao kata nchi ya Marekani na kwa dakika tatu tu.

Ingawa tukio hili litatokea mbali na kwetu, wale wengi ambao hawatakwenda Marekani kulishuhudia, wanaweza kufuatilia tukio mubashara katika mtandao. Kwa saa za Tanzania, muda wa kupatwa ni kati ya saa 12:46 jioni ya Agosti 21, hadi saa 6:05 usiku. Mviringo nyeusi ya Mwezi itaanza kufunika Jua kuanzia saa 1:46 jioni hadi saa 5:02 usiku. Usikose hasa kuuona Jua likiwa limefunikwa kamilifu saa 3:25 usiku. Unaweza kutumia tovuti kufuatilia tukio mubashara, kwa mfano: Total Solar Eclipse 2017: Here Are the Best Live-Video Streams to Watch.

Kupatwa kwa Jua hufuatana na Mwezi mwandamo. Mwezi mwandamo hutokea wakati Mwezi unkuja kati ya Jua na Dunia. Yaani wakati wa machweo, wakati Jua linzama chini ya upeo wa magharibi, upande wa usiku wa Mwezi unatuangalia sisi Duniani, na Jua linakuwa upande huo huo kwa hiyo Mwezi hauwezi kuonekana. Kumbuka kwamba wakati wa Mwezi mwandamo, Jua, Mwezi na Dunia haziwi katika mstari mnyoofu, kwa hiyo ingawa Mwezi huandama kila mwezi, Jua halipatwi kila mwezi.

Vile vile, wakati wa Mwezi mpevu, magimba matatu hayo yamepangika kama wakati wa kupatwa kwa Mwezi na Dunia huwa kati ya Jua na Mwezi, ile haziwi katika mstari mnyoofu. Ndio maana, ingawa Mwezi huwa mpevu kila mwezi, Mwezi haupatwi kila mwezi.

Siku za Mwezi mwandamo ni muhimu sana kwa wale ambao hufuata kalenda ya Mwezi kwa vile zinaashiria mwanzo wa mwezi. Mwezi mwandamo wa Agosti 21 unatokea saa 12:30 jioni kwa hiyo hauwezi kuonekana jioni hiyo. Siku inayofuata, tarehe 22 Agosti, Mwezi utakuwa umesogea juu angani kwa nyuzi kiasi kumi juu ya upeo wa magharibi wakati wa machweo na hilali nyembamba itakuwa imejitokeza. Kuona hilali hiyo, yaani Mwezi wa kwanza wa mwezi, utahitaji kuwa na upeo uliowazi upande wa magharibi na mbali na miti au majengo. Machweo ni saa 12:20 jioni, kwa hiyo saa 12:30 au 12:40 kutakuwa na giza ya kutosha kuweza kuona hilali nyembamba ya Mwezi wa kwanza wa mwezi.

HILALI NYEMBAMBA.jpg

Ili Kuwa na uhakika wa kutosha wa kuona hilali ya Mwezi wa kwanza wa mwezi siku ya Agosti 22, inabidi ujitayarishe kwa kutafuta eneo wazi unaoonesha vizuri upeo wa magharibi. Angalia mahala ambapo Jua linazama upeoni. Anga likianza kupata giza angaza macho nyuzi chache juu ya mahala ambapo uliona Jua likizama na subiri anga lipate giza ya kutosha. Siku hiyo Mwezi utazama mara baada ya saa moja jioni, kwa hiyo utakuwa umeuona Mwezi kabla ya hapo. Lakini siku ya pili yake, yaani Agosti 23, Mwezi utakuwa umepaa zaidi angani kiasi cha nyuzi 20 juu ya upeo wakati wa magharibi, kwa hiyo hilali ya Mwezi itakuwa kubwa zaidi na itang’aa zaidi, wa hiyo itaonekana wazi na kila mtu ataweza kuona.
 
It looks like you are not very convinced. I can explain further.

1. The shadow of the Moon is very small so it covers only a small area on Earth. So only a few people can see a solar eclipse.

2. The shadow of the Moon will fall only on North America and the dark shadow (umbra) will be in a narrow path in USA only, so darkness will be seen in that narrow band in the US and the rest if US will see partial solar eclipse in which the Sun will be a crescent. Africa is too far away and outside the shadow of the Moon so we cannot see this August 21 solar eclipse.

3. People who do not know about solar system and orbits of Moon and Earth cannot understand that eclipse is a normal thing that can happen. So they think of strange ways to explain it and frighten people.
 
Maelezo mengi mkuu, we niambie huku kwetu kyela ntaona hilo tukio au silioni?
 
to explain it and frighten people.
Maelezo mengi mkuu, we niambie huku kwetu kyela ntaona hilo tukio au silioni?
Maelezo mengi mkuu, we niambie huku kwetu kyela ntaona hilo tukio au silioni?
Kuna matukio mawili katika makala yangu.

Moja ni lile la kupatwa kwa Jua. Tukio hilo halitaonekana Kyela, maana ni Marekani wataliona.

La pili ni lile la kuona hilali ya kwanza. Hilo litaonekana Kyela siku ya Agosti 22 au 23 yaani kesho jioni au kesho kutwa jioni mradi hali ya anga haina mawingu.
 
nini maana ya kuona hiyo hilal ya kwanza hapo Agosti 22 au 23

Mkuu elezea faida za kuona hilali ya kwanza
 
H
nini maana ya kuona hiyo hilal ya kwanza hapo Agosti 22 au 23

Mkuu elezea faida za kuona hilali ya kwanza
Hilali ya kwanza inatafutwa na wale wanaotumia kalenda inayoendana na Mewzi, yaani ndiyo mwanzo wa mwezi. Mwezi wa Dhulhaj utanza kwa kuona hilali ya kwanza.
 
Back
Top Bottom