Mwezi mmoja wa Ndoa Sasa Tangu niolewe na mwanaume ambaye nilimpata kupitia JF

Nasiche

JF-Expert Member
Jun 18, 2019
291
732
September 28 ,2019 nikiwa nimekosa uelekeo wa maisha ya kimahusiano nilikuja hapa jukwaani ,Nikasema natafuta Mume ,kiukweli uhitaji nilikiwa nao lakini sikuwa naamini kama huku nitapata mtu,pili niliogopa ningeonekana kuhuni au kutoaminika so ilikuwa kama njia TU ya kujiondolea stress walikuja watu wengi sana Pm Kwa sababu sikuweka vigezo hivyo sikuweza kumjibu yeyote.Niliamuwa kupost tena na kuchanganua nini nataka ,wapo wengi sana walinifata tena ,nilikuwa napitia post ya mtu mmoja baad ya mwingine katika wote nilijibu post Moja tu nayo iliandikwa hivi

Habari Mimi naitwa Frank nipo Dar naomba tufahamiane
Hii post ilikamata Moyo Wangu Kwa namna ambayo sikujuwa Kwa nini nilimjibu na baada ya siku kadhaa alireply ,tukapeana mawasiliano tukaonana.

Nilipomuona tu, nilijuwa nimemuona mume wangu, uwiiii he was so romantic,he was so caring he was so humble , handsome na Kila kitu (pita kwenye post zangu za nyuma).

Tumekaa kwenye mahusiano Toka 2019 mpaka tarehe 13/11/2021 tulipofunga pingu za maisha.

Nina mwezi mmoja Sasa kwenye Ndoa Namshukuru sana Mungu,Kwa kunipa mume mwenye Hofu ya Mungu na mwenye mapenzi ya dhati.

Mume wangu najuwa upo busy lakini Kuna siku utasoma huu ujumbe nashukuru Kwa kuniamini , nashukuru Kwa kunipenda nashukuru Kwa kuniowa.Isingekuwa rahisi kuaminika.

Moral of the story:Mtandaoni Kuna watu waongo ,waharibifu na walioshindikana lakini pamoja na hayo Kuna watu waaminifu na wazuri sana ,inakutaka kutulia kumuomba Mungu kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano ya Mtandaoni.

Asante kama una swali uliza ,nipo free Leo nitamjibu kila mtu.

#Ukipitia post zangu za nyuma utaweza kuelewa zaidi.
 
Hongera sana kwa kupata hi itaji la moyo wako,

Sema na nyie mnaopata wapenzi humu, kwann msiwe mnatualika sisi members/mods tujumuike pamoja Kwenye izo harus zenu?
Mimi binafsi nilisahau ,usiku wa Jana ndo alinikumbusha kuleta mrejesho

Ni Kwa sababu baada ya kujuana alikuwa hakai mbali na napokaa Mimi so tulizoeana mpaka tukasahau kuhusu Jf
 
Embu Tulia tulia kwanza.

Kwani umeshawahi kutapika akadeki?
Kunya akaflash?
Kuumwa akakuletea poti la kujisaidia akamwaga?
Kuzaa ukanyonyesha nyonyo zikalala zikawa ndala?
Kujamba ukiwa usingizini baada ya kula maharage na yeye yupo macho chumba kizima kikawa hoi?

Na yeye umeshamfanyia baadhi ya hayo?

Embu kuwa na subira huku ukimuomba MUNGU awatangulie. Kila la heri.
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom