Mwenzio akinyolewa>>: Mfalme wa saudi arabia afanya kweli!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenzio akinyolewa>>: Mfalme wa saudi arabia afanya kweli!!!

Discussion in 'International Forum' started by Ngekewa, Mar 19, 2011.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Baada ya kuona yanayotokea kwa wenzake Mfalme Abdalla kule Saudi Arabia ameamuwa kutowa mambo kadhaa kwa wananchi wake, miongomi mwake ni:
  - Malipo ya mshahara wa miezi miwili kama bonasi kwa wafanyakazi wote wa Serikali na malipo ya miezi miwili kwa matumizi wale walioko nje masomoni.
  -Malipo ya SR 2000 =$ 530 kwa wasiio na kazi kila mwezi.
  -Kupandisha kiwango cha chini cha mishahara na kuwa Reale 3000 =$ 800
  - reale billioni 250 kwa ajili ya kujenga makazi fleti 500,000 nchi nzima.
  -Kuundwa kwa comisheni ya kupigana na rushwa (TAKUKURU).
  -Reale billioni 16 kuboresha huduma za Afya!
  - Kuongeza kiwango cha mkopo wa kujengea nyumba kutoka SR 300,000 mpaka SR 500,000
  - ongezeko kwa mkopo kwa Hospitali binafsi kutoka SR milioni 50 mpaka SR 200
  - Kutowa nafasi za ajira za askari 60,000
  Kuongezwa malipo kwa maaskari wote kwa gredi moja juu kwa kila askari.
  -kuengeza matawi ya kamati ya utowaji wa Scholarship (labda tuseme kama bodi ya mikopo hapa kwetu)
  -SR milioni 200 kwa idara inayoangalia mambo ya maadili.
  - Nafasi 500 mpya kwa wizara ya Biashara katika kufatilia mambo ya soko na namna ya kuwaadhibu wanaokwenda kinyume na mfumo wa bei kwenye soko.

  Sijui kiasi gani people Power ya Tanzania inaweza kutuahidi nini tukishawaondoa CCM, jee tutapata angalau nusu ya haya ya Mfalme?
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huyo mfalme amefanya hivyo kwa sababu nchi yake ina uwezo wa kugawana kilichopo. Kinachopaswa kufanya Tanzania iwe hivyo hivyo, yaani mgao sawa wa kile tulichonacho, kiwe kingi kiwe kidogo; tafauti na hivi sasa ambapo kila siku tafauti baina ya masikini na matajiri inaongezeka. Walio matajiri wanakwa matajiri zaidi na masiki wanakuwa masikini zaidi.

  Ufanisi wa nchi hautokani tu na serikali kumwaga mapesa bali pia kila raia popote alipo kujituma kwa uwezo wake. Lakini kujituma huko hakuwezekani ikiwa hakuwezeshwa na serikali. Leo hii Tanzania utendaji umeshuka sio tu kwa kukosa elimu inayofaa na vitendea kazi, bali kwa mtindo ulioanzishwa na CCM wa kujichukulia chako mapema, kila mtu yuko tayari kufanya analoweza kupora chochote (iwe pesa, dawa, madaftari, vipuri, mafuta....) kwa sababu asipofanya hivyo hawezi kuishi;na wale wanaoweza kuishi, ikiwa watapata fursa wanapora kwa sababu ndio mtindo. Kauli ya kufunga mkanda inaonesha inaelekezwa kwa walala hoi tu wakati walio karibu na mlo hawafanyi hivyo.
   
 3. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Watamtoa tu Libya vipi hivyo vyote ni bure,hata vijana wanaokwenda kutembea ulaya walikuwa wanapewa USD 5000 kwa ajili ya matumizi still watu hawamtaki Gaddafi sidhani kama atadumu na ufalme wake.
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya Gadafi alikuwa peke yake na pia anachukiwa na Wakubwa,kwa upande wa Saudi Arabia uko ukoo mzima na kila mmoja ana jeshi lake na kikubwa ni kuwa Saudi Arabia anafanya vyovyote anavyoambiwa na Marekani.
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  The monarch in Saudia is safe and ok
   
 6. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Huu ni ujinga ambao kila siju tunauzungumza sasa hizi pesa zote zilikuwa
  wapi,kama si kuwataabisha watu tu wasio na hatia katika nchi yao.
   
 7. s

  shadhuly Senior Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  yah true marekani na uingereza wana maslahi makubwa pale na wao ndio wanaoulinda ufalme ule.na wanafaidika sana so mfalme wa saudi ni puppet leader.so hata wakiasi wananchi watasaidiwa kuzima uasi at any cost.tofauti na libya marekani na rafiki zake ndo wanaongoza mapambano ya uasi.
   
 8. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kasoma alama za nyakati na kujirekebisha mapema. so he is safe. Ghadafi hakusoma alama za nyakati ndo tatizo lake. Si kweli kuwa alikuwa akiwapa watu kila walichotaka etu dola 5000 kwenda ulaya kama mr. nguluvisonzo alivyotaka tuamini.
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  They say "Money cannot buy freedom" ....Saudi Dictator and other obscenely wealthy Gulf Arabs are resorting to their old tactics which is bribing their fellow citizens will $$z. Extra cash will not solve the social ills of their countries instead it would raise the inflationary pressures and that would further exacerbate the situation.
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Misemo si maandiko ya vitabu vitakatifu. Kumuongoza binaadamu kunataka akili. Hapa kwetu mbona Lowassa na RA hawawezekani kuangushwa kwenye majimbo yao? Kama ni msemo basi pia msemo unaosema " Panapo udhia penyeza Rupia.
  Na mfalme nae kaona hivyo na ukiangalia sana utaona ametowa motisha kubwa kwa maaskari? Na huko Saudia kila watu watano inawezekana ikawa watatu ni maaskari au mashushushu.
   
Loading...