MC Chere
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 586
- 400
Heri na iwe kwenu nyote mlioamka muwazima wa afya njema.
Mwenzenu nimefufua kaofisi nilikokafunga mwaka jana,ni siku 3 tangu nianze kazi lakini usiku wa kuamkia leo wadokozi wamenipitia,wamechukua kiasi fulani cha mzigo kwa kuvunja kufuli na wameondoka nayo,na hivi mpaka sasa mlango hauna kufuli na hata sijataka kununua kufuli jingine maana naona haina msaada zaidi ya kumpata huyo mdokozi anirejeshee vitu vyangu.
Hatua za awali nilizochukua ni kutaarifu mamlaka za kiserikali kuwa wanaendelea na uchunguzi na nimewaambia kuwa ninachohitaji ni kurejeshwa mzigo wangu ikizingatiwa huku ni kijijini na haya mambo ni adimu.
Siwezi hata kusamehe maana namna ambavyo nimepata huo mtaji kwa usawa huu Mungu ndiye anayejua.
Hoja imewekwa mezani kwa wazoefu wa mambo kwa uzoefu wenu nifanyeje mwenzenu ili changu kirudi.
Nitashukuru kwa michango yenu.
Area KILOLO-IRINGA