Mwenzenu, usiku leo silali........................ !

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Mwenzenuu, usiku leo silali,

Nateseka usingizi sipati huwa nabaki nahangaika,

Kuyasema yote, ninayaona siwezi, yasije yakaleta, udadisi kwa watu bure…

Shahidi yangu ni mama watoto, yeye anajua,, kwani huwa aniona ninavyohangaika…X 2


Naalalaaaa, kwa kwa tabu mie, walisema watu lisemwalo kama halipo laja………..X 2

Ingekuwa ni ndoto wala mimi nisingejali oooo, nawaelezea enyi walimwengu muyajue mateso yangu…..

Naalalaaaa, kwa kwa tabu mie, walisema watu lisemwalo kama halipo laja………..X 2

Uwaonao wazuri, wabaya ni hao haooo………………. Tena wapo humu humu JF…

Amini usiamini kukuchekea sio kufurahi na we dada aaaa……………….

Naalalaaaa, kwa kwa tabu mie, walisema watu lisemwalo kama halipo laja………..X 2


**************************************************************

Leo nimekumbuka wimbo huu wa Sikinde enzi hizo nikiwa bado damu inachemka.......................
 
Senksi mkuu, mimi ni kizazi cha dot.com, unaweza kunipa line-up ya Sikinde wakati huo?
 
Senksi mkuu, mimi ni kizazi cha dot.com, unaweza kunipa line-up ya Sikinde wakati huo?
sobhuza Enzi hizo kulikuwa na:
Maalimu Muhidin Gurumo
Shaaban Dede
Hassan rahani Bitchuka
Michael King Enoch (Marehemu)
Cosmas Chidumule
Abel Baltazari (Marehemu)
 
Last edited by a moderator:
Wakti huu nasikiliza wimbo wa Shamar - A Night To Remember (1982); Nimekumbuka mbali, wakti huo ndo nimeanza kuota chunusi usoni. So nina motive behind. Wewe je?
Enzi hizo (1982) ndio nilikuwa najifunza kufukuzia visichana kijijini, halafu unatembea kilomita 5 kwenda kijiji cha jirani kufuata walimbwende na tochi yenye mwanga hafifu ukipita katika msitu mnene.............LOL
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom