Mwenzenu sasa naoa, naomba michango yenu tafadhali…………………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Kauli hiyo siku hizi ni ya kawaida sana, kwani kila uchao watu wanaoana, kila wiki siku hizi utasikia matarumbeta na nderemo kila kona na sio mijini tu bali pia hata huko vijijini watu wakishangilia na kufurahia tendo hilo la mwanamke na mwanaume kuungana na kuwa mwili mmoja, yaani kufunga ndoa.

Kwa akili za kawaida unaweza kudhani kwamba watu siku hizi wanaoana kwa sababu wanaheshimu ndoa na ndio maana wameamua kuishi maisha ya kindoa, lakini ukweli ni kwamba, siku si nyingi tendo la kuoana litaonekana kama kitu kisicho na maana tena.
Najua wapo watakaopinga jambo hili, lakini naamini ni kwa sababu hawajui ukweli halisi……….. nasema hawajui kwa sababu wao wanaamini kwamba harusi au kuoana ni suala la kimaumbile, yaani binadamu hawezi kuishi au kuzaana bila kuoana. Lakini ukweli ni kwamba kuoana ni suala ambalo lilipangwa na binadamu.

Katika kipindi cha miaka 45 iliyopita, dunia imekuwa ikishuhudia kubadilika kwa mitazamo mingi kuhusiana na na mapenzi na ndoa. Mapenzi na ndoa yalivyokuwa yakitazamwa miaka ya 1970 sivyo yanavyotazamwa leo kabisa. Siyo hapa kwetu tu, bali karibu duniani kote.
Labada nikukumbushe tu kwamba, hadi miaka ya 1980, ndipo tulipoanza kusoma au kusikiliza na pengine kuona habari za mahusiano zikigusa tendo la ndoa zaidi kuliko mapenzi, zikizungumzia tendo la ndoa kama kwamba linazungumzia kupendana. Jamii ilianza kuchukulia uhusiano kuwa ni kukutana kimwili, halafu basi, kwani kukutana kimwili peke yake inatosha bila upendo. Kuoana ikawa siyo lengo la mwisho wala la kwanza la watu kupendana, bali lengo lililopinda na kushindwa kueleweka.

Ndipo hapo watu wengi wakaanza kutumbukia kwenye mapenzi ya leo leo bila kujali kesho itakuwaje. Kumbuka kwamba hata hizi mimba za utotoni zilianza kuonekana kama kitu cha kawaida kwenye miaka ya 1990, kwani kabla ya hapo ilikuwa ni kashfa ya mtaa. Kufanya mapenzi kukapewa kipaumbele, kuoana ikawa ni mwanzo wa mwisho wa mapenzi.
Vitabu vya hadithi na vyombo vya habari vimekuwa vikielezea suala la kujaamiana ndio mapenzi yenyewe. Kama kujaamiana ndio mapenzi yenyewe, sasa kuoana kuna nafasi gani? Ni dhahiri kuoana kutakuwa na nafasi ndogo sana, kwa sababu hata bila kuoana, watu wanapata wanachohitaji.

Kama hujui, naomba nikwambie kwamba, kupanda kwa kiwango cha talaka kwa jamii kama yetu kulianza kwenye miaka ya 1980, na kumekuwa kunaendelea kwa kupanda hadi leo. Hakuna kujiuliza tena, kama mtu hawezi kupata bashasha na furaha kutoka kwa mtu mmoja basi anaweza kuipata kwa mtu mwingine, sasa kama ni hivyo, ndoa ina maana gani? Na ndio maana tafiti nyingi hivi sasa zinaonesha kwamba, ndoa sita kati ya kila kumi kwa wakati fulani wa maisha ya ndoa hizo hukabiliwa na kutoka nje.


Kabla ya kuzuka kwa dhana hii ya mapenzi ya kuhemkwa, ya mwili na yasiyo na mizizi, mahali pakee ambako mtu angepata penzi, ukiacha lile la wazazi na ndugu zake, ilikuwa ni kwa mke au mumewe. Kwa hiyo ndoa, ilikuwa ndipo mahali ambapo mtu angeweka nguvu na matarajio yake yote, kwani kuoana kulikuwa na maana pana na halisi ya mapenzi, na ndio maana wanandoa waliangalia na kuamini katika, "hadi kifo kije kitutenge." Kuwa na familia na kulea watoto likawa ndilo lengo kuu la watu kuoana.

 
Kichwa hakiendani na utumbo.

@FaizaFoxy........... Ni kweli kwa uelewa wako huwezi kunielewa, ni mtu mwenye utambuzi ambaye anaweza kuelewa nazungumzia jambo gani.......... Pole kwa kutonielewa...........
 
Sijui anazungumzia kuoa, sijui anazungumzia michango ya harusi nimesoma sijaelewa bwana Mtambuzi anamaanisha nini
Umesoma haraka haraka, huku ukiwa na majibu yako tayari....................Kichwa cha habari kinaendana na paragraph ya kwanza...............LOL
 
Back
Top Bottom