Mwenza wako anapokataa kufunga ndoa lakini anataka muendelee kuwa pamoja nini maana yake?

prince uweri

Senior Member
Feb 6, 2016
112
82
Wakuu nisaidieni mawazo kidogo,

Nina jamaa yangu hivi majuzi kalazimika kurudisha pesa za michango ya harusi yake baada ya mwenza wake kugoma kufunga ndoa. Ishu iko hivi jamaa anafanya kazi Shinyanga maeneo ya Kahama lakini familia maana ya mke na watoto wake wawili wanaishi Mwanza ambako wamejenga.

Baada ya kupanga na mwenzake waliyeishi nae miaka tisa kuwa sasa ni wakati wa kuhalalisha ndoa wakakubaliana vizuri. Kijana kaanza michakato na mambo yakaanza kwa kasi sana ikiwa ni taarifa kwa ndugu jamaa na marafiki am apo vikao vilianza na taratibu zingine za kikanisa.

Hivyo jamaa akawa kila anapopata likizo ni kufuatili kamati ya vikao imefikia wapi na kwa bahati hakuna kilicho haribika mpaka tarehe ikawa imeshajulikana na ikawa imebaki mambo ya kusubiri tarehe.

Ikiwa imebaki mwenzi mmoja kufika tarehe husika, ikatokea ishu ya ajabu sana yaani huyu akapata likizo kama kawaida kamtaarifu mwenzake kuwa anakuja lakini kabla ya kufika Mwanza akamwambia mwenzie kuwa atapita kwanza kwao (kwa kijana) amboko shughuli ingefanyika.

Lakini mke akamwambia aache tu kuwasumbua ndugu zake kwasababu yeye hayuko tayari kuishi nae. Kijana hakuamini ikabidi kweli aache kwenda kwao na kuelekea Mwanza ambako mbaya zaidi hakumkuta mkewe na akakuta watoto wameachwa kwa jirani. Alipouliza majirani walimjibu huyu kasema kaenda hospitali. Kijana alipojaribu kuwasiliana nae simu yake haikujibiwa.

Kijana hakuhamaki akabuy time mpaka siku iliyofuata. Baada ya hapo ilimchuku siku kama 5 bila mawasiliano na alipoona muda wa kurudi kazini umewadia na mdada hapatikani kwenye simu aliwasiliana na ukweni nako hawakuwa wanajua chochote. Jamaa akatoa ripoti polisi na ustawi wa jamii.

Hivo akachukuwa watoto wake akapeleka kwa dada yake nje kabisa ya mwanzani nyumba akaweka mlinzi yeye akarudi zake kazini. Akiwa huko baada familia yake kuchanganyikiwa walianza kumtafuta yule mdada kila sehemu waliloamini anaweza kuwepo bila mafanikio.

Baada ya wiki mbili hivi mdada akaibuka na kudai ni kweli hana mpango wa kuuishi na mshikaji kisa anadai ajisikiii tu. Basi vikao mbli mbali vya familia viakaamua hiyo mipango ya ndoa ife na jamaa akalazimika kuanza kurudisha hela za watu. Baada ya muda huyu msichana kaanza kurudi kwa jamaa eti anaomba msamaha hii ni halali jamani?.

Kisa ni cha kweli.
 
Haina haja kurudiana nae, kumsamehe ruksa amsamehe rakini si kukubari kuishi nae tena hafai tena huyo kwani kichwani hakuna kitu, anaweza siku kusema hajisikii kuishi au kusaidia wakwe.
 
Hata picha haoni, ni jamaa yako au ni wewe mkulu
Hata picha haoni, ni jamaa yako au ni wewe mkulu
Hapana mkuu siyo mimi ni jamaa yangu wa karibu sana. Sasa cha ajabu sana ni kuwa jamaa amefikia hatu anaonesha dalili za kulegeza uzi make familia ilipiga marufuku kwa wanafamili wote kutojihusisha na yule mdada. Lakini juzi mshikaji kaaja kwao anaomba kuitisha kikoa ili familia ione namna ya kumsamehe lakini familia imechomoa. Kwa kuwa alishindwa kueleza kama anafahamu alikokuwa kajichimbia kwa kipindi chote cha wiki mbili. Kwa sasa mdada yuko kwao.
 
Wakuu nisaidieni mawazo kidogo. Nina jamaa yangu hivi majuzi kalazimika kurudisha pesa za michango ya harusi yake baada ya mwenza wake kugoma kufunga ndoa. Ishu iko hivi jamaa anafanya kazi shinyanga maeneo ya kahama lakini familia maana ya mke na watoto wake wawili wanaishi mwanza ambako wamejenga. Baada ya kupanga na mwenzake waliyeishi nae miaka tisa kuwa sasa ni wakati wa kuhalalisha ndoa wakakubaliana vizuri. Kijana kaanza michakato na mambo yakaanza kwa kasi sana ikiwa ni taarifa kwa ndugu jamaa na marafiki am apo vikao vilianza na taratibu zingine za kikanisa. Hivyo jamaa akawa kila anapopata likizo ni kufuatili kamati ya vikao imefikia wapi na kwa bahati hakuna kilicho haribika mpaka tarehe ikawa imeshajulikana na ikawa imebaki mambo ya kusubiri tarehe. Ikiwa imebaki mwenzi mmoja naa kufika tarehe husika, ikatokea ishu ya ajabu sana yaani huyu akapata likizo kama kawaida kamtaarifu mwenzake kuwa anakuja lakini kabla ya kufika mwanza akamwambia mwenzie kuwa atapita kwanza kwao (kwa kijana) amboko shughuli ingefanyika. Lakini mke akamwambia aache tu kuwasumbua ndugu zake kwa sababu yeye hayuko tayari kuishi nae. Kijana hakuamini ikabidi kweli aache kwenda kwao na kuelekea mwanza ambako mbaya zaidi hakumkuta mkewe na akakuta watoto wameachwa kwa jirani. Alipouliza majirani walimjibu huyu kasema kaenda hospitali. Kijana alipojaribu kuwasiliana nae simu yake haikujibiwa. Kijana hakuhamaki akabuy time mpaka siku iliyofuata. Baada ya hapo ilimchuku siku kama 5 bila mawasiliano na alipoona muda wa kurudi kazini umewadia na mdada hapatikani kwenye simu aliwasiliana na ukweni nako hawakuwa wanajua chochote. Jamaa akatoa ripoti polis na ustawi wa jamii. Hivo akachukuwa watoto wake akapeleka kwa dada yake nje kabisa y mwanzan nyumba akaweka mlinzi yeye akarudi zake kazini. Akiwa huko baada familia yake kuchanganyikiwa walianza kumtafuta yule mdada kila sehemu waliloamini anaweza kuwepo bila mafanikio. Baad ya wiki mbili hivi mdada akaibuka n kudai ni kweli hana mpango wa kuuishi na mshikaji kisa anadai ajisikiii tu. Basi vikao mbli mbali vya familia viakaamua hiyo mipango ya ndoa ife na jamaa akalazimik kuanza kurudisha hel a z watu. Baada ya muda huyu msichana kaanza kurudi kwa jamaa eti anaomba msamaha hii ni halali jamani.......kisa ni cha kweli.
No komenti, ila asante kwa taarifa.
 
Kuna wakati huwa namkosea Mungu wangu kwa makusudi kwa kuamini kua yule Mungu aliyemuumba Adam siyo yule aliyemuumba Hawa
 
mwanamke akikuambia hawez kuolewa nawe huwa ana maanisha kweli.
Huyo mwanamke atakuwa na jamaa yake huko sasa kaona jamaa haeleweki ndio karud kwa jamaa.
Huyo jamaa ajitambui kbs mwanamke anafikia hatua ya kukudharirisha kias hicho halaf unamkubali.
Jamas apige chin huyo sio mwanamke.
 
Kwanza anaanzaje kurudi kuomba msamaha? Kwa kuwa hajisikii basi aendelee kutokujisikia
 
Back
Top Bottom