Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe



Kuna binadamu alinifanyia kwazo la hali ya juu, nikavunja mahusiano nae.

Kiukweli nimemsamehe ila kumbukumbu haijafutika, nikimuona sisikii hasira au uchungu ila sitaki mazoea zaidi ya salamu.

Bora mtu acheze na mali zangu kuliko acheze na maisha yangu, pesa inatafutwa ila maisha yakipita hayajirudii hasa muda na umri.
 
Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.
Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.

Mungu akubariki sana!
 
Back
Top Bottom