Mwenyekiti wangu wa Jumuiya anataka tuanzishe mahusiano ya kimapenzi

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
368
425
Habari wana jukwaa,

Mimi ni mwanaume nina mke na watoto wawili, mke wangu nimefunga naye ndoa kabisa kanisani.Sasa kuna hili tatizo linanisumbua karibu miezi miwili sasa, ni mama mmoja ambaye ni Mwenyekiti wangu wa Jumuiya anataka tuanzishe mahusiano ya kimapenzi.

Ki umri amenipita miaka takribani 9, yeye ni mjane mumewe alifariki miaka 5 iliyopita. Amekuwa akinisumbua sana huyu mama mpaka naona kero sasa.

Naomba wana Jukwaa mnishauri nifanyeje.

Nawaza nimripoti kwenye Jumuiya au nikamripoti kwa Paroko ila naona kama nitamdhalilisha.
 
Kama hupo serious mwambie "sitaki kufanya zinaa"

Na akiendelea kamshati kanisani/Mwenyekiti wa kanda Wa jumuiya.
 
Hakuna haja ya kumripoti popote, mwambie ukweli tu kwamba hakuvutii na una mkeo na hauko tayari kuitaka papuchi yake. Akiendelea kukusumbua ndiyo umripoti lakini kumbuka ni lazima uwe na ushahidi wa kutosha vinginevyo anaweza kukugeuzia kibao na kuonyesha wewe ndiye ulikuwa unampigia speed kila kukicha.

 
Ana mihemko inamsumbua,anataka stress zake za mihemko ikuvunjie ndoa. Heshimu ndoa yako,mkemee huyo shetani. Akizidisha usumbufu toa taarifa ila kama alivyosema BAK hakikisha unakuwa na ushahidi.
 
Back
Top Bottom