Mwenyekiti wangu Mbowe miaka 20 na ukimya wa haya 10

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Na Johnson Swai, USA RIVER

Mimi ni mwanachadema kindakindaki lakini siingia vikao vitukufu vya juu vya Chama hivyo leo nimeona nikuulize maswali haya 10 na wanachana wenzangu ili tuone kama wewe Mwenyekiti wetu unafaa uendelee tena au ndio chama chetu tuzidi kushindwa na CCM?

1. Miaka 20 Uenyekiti gani huu Ndugu Mbowe ina maana kwenye Chama hakuna wengine?

2. Kwa nini familia ya Chacha Wangwe na wanachama bado wanalia chini kwa chini kutokana na kifo cha utata cha Msaidizi wako huyo na kwa nini, tofauti na mengine, haujawahi kuomba wachunguzi wa kimataifa katika hili?

3. Kwa nini uongoze Chama huku kinanuka damu kinahusishwa na mambo ya kuumiza watu; rejea kujitoa kwa Zitto Kabwe akisema alitegeshewa mpaka sumu, mateso ya Kangezi yule Mlinzi wa Dkt. Slaa akiwa katika ofisi za Chama na wengineo?

4. Kwa nini Chama miaka 20 kinapanga kwenye kajumba kamtu kasiko na hadhi. Hii nyumba ni ya nani hasa na upeo wako ndio umeishia hapo?

5. Kwa nini katika miaka yako yote 20 haujawahi kuongoza maandamano wilayani Hai ambako ndiko ngome yako?

6. Kwa nini Chama hakitoi maelezo ya kutosha kuhusu matumizi ya ruzuku na wanachama wengi hadi wabunge wanalalamika?

7. Nataka unapoomba kura pia utusaidie kujua kama yale magari ya Chama yaliyonunuliwa na kuandikwa majina ya watu binafsi yamerudi na ni kina nani walifanya hivyo?

8. Tueleze hizi tuhuma za kupokea fedha za Lowassa zikoje, Je, fedha hizo ziko wapi na zilitumikaje?

9. Ni kweli kwamba umeshaingia dili lingine na Membe na ndio maana gazeti la familia yako, Tanzania Daima, siku hizi linamfagilia Membe kuliko hata chama chako na wewe binafsi?

10. Tuhuma za ukanda, ukabila na wabunge Viti Maalum kupitia mchakato wa kuvua chupi, ikiwemo wewe mwenyewe hadi kuzaa na baadhi ya wabunge wa Chama chako, haujawahi kukanusha wala kuzungumza chochote, unadhani bado una ushawishi wa kukiongoza chama chetu?

Naomba nisaidiwe kuuliziwa haya.

Asanteni


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mimi namshauri Mbowe kwasababu ameshakuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa muda mrefu sana huku akijaribu kushika dola na hajafanikiwa, ni vema sasa akawaachia na wengine wafanye kadri ya uwezo wao kukipeleka chama mbele na yeye Mbowe abaki kama mchauri tu. Sema ndio hivyo haiwezekani, atang'ang'ania nafasi hiyo kwasababu ndio inamfanya aweze kucontrol chama katika nyanja zote kususan MAPATOOO
 
Kama kweli Mbowe alisababisha kifo cha Chacha Wangwe serikali ingemuacha??
Acha mihemuko tumia akili!!
pale Soweto Ars yalirushwa mabomu watu wakafa wengine kwa risasi za polisi, sakasema Chadema wamejilipua mabomu.
Hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa!!
Lissu bado kwa mvua zote za risasi bado hakuna aliyekamatwa.
Wewe bado tuu hujui adui wa nchi hii ni nani anafuata propaganda za Lumumba??
Fungua macho uone ukweli, mbunge wako wa Meru Nasari kakimbia naye kakoswakoswa na risasi!!
Bado unamuonaMbowe mbaya, MaCCM wanataka kufanya CDM kama CUF ya Lipumba.
Acha Mbowe aimarishe chama ukombozi utapatikana, ukweli utajulikana siku moja!!
 
maramla,
Hayakuhusu hata kidogo.
Kam ni mfanya biashara kwa sasa ni msimu wa sikukuu n mwisho wa mwaka fanya biashara mzee inalipa kweli.
Kama ni mkulima mzee kalime kwani kilimo kinalipa tazama mvua zinanyesha kinoma.

Achana na siasa za vyama visivyokuhusu kwani unajulikana kabisa wewe ni chama gani kwa nn kujitaabisha kwa kujipa uanachama wa chama kingine?

Jitahidi kufana yanayokuhusu tu
 
Back
Top Bottom