Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kama ambavyo siku zote nimekua nikisema kua mimi ni mkweli daima na fitina kwangu mwiko. Ni MwanaCCM hai niliyekitumikia muda mrefu na bado naendelea. Rais wangu ulikosea mambo machache sana pamoja na mengine mengi makubwa uliyofanya.

MAISHA MAGUMU KWA WATANZANIA
Mwenyekiti wangu, maisha ni magumu sana kwa watanzania wote hata mtu kupata milo miwili kwa siku ni shida. Kama wasaidizi hawasemi ukweli mkuu huko mitaani watu taabani kuliko awamu iliyopita. Watu walioko vijijini hawataki kujua Dar es salaam kuna marababara za juu au kuna Airport, hawajui kama kama kuna makubwa yamefanyika. Wao wanataka maisha mazuri.
Kiukweli akitokea mgombea atakayewaambia vizuri walalahoi hawa kura zote atapewa.

BIASHARA KUWA NGUMU
Kwa sasa maisha ya wafanyabishara yamekua magumu kabisa kila mahali kuliko awamu iliyopita, lipo tatizo kubwa ambalo kama tusiposema ukweli CCM hakuna mfanyabiashara atakayetupatia kura.

MAISHA MAGUMU KWA WAFANYAKAZI WA UMMA
Ni muda sasa wafanyakazi wa umma wanalia na maslahi duni, wengi hawana amani.
Hapa kura hatupati kabisa katika kundi hili tupende tusipende. Akitokea mgombea atakayeongea vizuri na kundi hili anaweza kuvuna kura nyingi sana na atapewa ushirikiano mkubwa .Wao wanaangalia mtu atakayewajali vizuri.

Mimi najaribu kusema msije mkasema hatukurlshauri.
 
Ambao wako taabani huko mitaani ni wale waliozeoa mishemishe na kuishi kisanii, sisi ambao tunajitambua na kuamini jasho lako ndio mkombozi namba moja tunaona maisha ni kawaida tu.

Changamoto haizwezi kukosekana katika maisha. Kama wewe ni mmoja wa wale walionufaika na ubabaishaji uliokiwepo awamu iliyopita, lazima awamu hii uone maisha magumu.

Changamsha akili, si Magufuli, Lisu, Membe n.k atakaebadilisha maisha yako.
 
Ndugu Mahanju, ni kweli unayoyasema; Lakini, nawaomba Watanzania tutangulize uzalendo kwanza. Uzalendo ambao ndani mwake mna kujitoa (mhanga) kwa hali na mali kwa ajili ya Nchi; kuna kujikana nafsi na kutengeneza kwa ajili ya watoto wetu, watoto wa watoto wetu, watoto wa watoto wa watoto wetu, na kuendelea.

Hebu jiulize, lipi bora, kujinyima (kwa muda) ili kile tunachokusanya tukitumie kujenga kwanza miundombinu mbalimbali (SGR, Stiglers HEP, Barabara nzuri, hospitali na vifaa tiba, eropleni, mifumo ya maji, mashule na vyuo, n.k.); Au, tukitumie kuongeza mishahara ya watumishi, na kadhalika?

Ni wazi huwezi fanya mambo yote kwa wakati mmoja. Hakutokuwa na efficiency. Lazima uwe na priority and options.
"Roma haikujengwa kwa siku moja"; hali kadhalika Ulaya magharibi au Asia. Watu walijifunga vibwebwe na leo hii vitukuu wa vitukuu ndio wanafaidi jasho la babu zao
Kwa hiyo, JPM yuko sawa. Watumishi wa Serikali na Watanzania kwa jumla, tunapaswa kujifunga mkanda na kuridhika na hiki kidogo tunachopata sasa.

Ni dhiki ya muda tu kwani tukiisha kamilisha kutengeneza miundombinu hii, Pesa inayokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali itatumika sasa kuboresha maisha ya watu.

Tena kwa ulaiini kabisa. Serikali itakuwa na uwezo wa hata kufanya KCCCM kuwa zaidi ya 2,000/= kwa mwezi!
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki JPM.
 
Eti uzalendo, na kujinyima!!
Uzalendo na kujinyima ni kwa watu wa chini huku yeye anagawa mapesa barabarani!!
IMG_20200808_090022.jpeg
 
Ambao wako taabani mitaani ni wale waliozeoa mishemishe na kuishi kisanii, sisi ambao tunajitambua na kuamini jasho lako ndio mkombozi namba moja tunaona maisha ni kawaida tu. Changamoto haizwezi kukosekana katika maisha. Kama wewe ni wa wale walionufaika na ubabaishaji uliokiwepo awamu iliyopita, awamu ghii uone maisha magumu. Changamsha akili, si Magufuli, Lisu, Membe n.k atakaebadilisha maisha yako.
Mimi nina mdogo wangu amegraduate udsm mwaka 2016 na hana ajira hadi leo. Huyu alikuwa mpiga dili gani???

Mie niligraduate SUA mwaka 2009 na 2010 kipindi cha JK nilipata kazi kwenye kampuni binafsi ya utafiti wa mazao!!

Magufuli wenu amefeli vibaya na lazima aanguke mwaka huu pamoja na kubebwa na vyombo vyenu vya Habari uchwara.
 
Wapo walio graduate mwaka huo huo wakaanzisha ufugaji wa kuku kwa msingi wa TZS 2,000,000 sasa hivi they are talking of 3 - 4mil a month. Msubiri Lisu, wengi wenu mnaamini nyumbani kwake amefunga bomba la ajira ambalo anasubiri achaguliwe ili alifunguwe ambao hamna ajira mpate ajira.
 
Ndugu Mahanju, ni kweli unayoyasema; Lakini, nawaomba Watanzania tutangulize uzalendo kwanza. Uzalendo ambao ndani mwake mna kujitoa (mhanga) kwa hali na mali kwa ajili ya Nchi; kuna kujikana nafsi na kutengeneza kwa ajili ya watoto wetu, watoto wa watoto wetu, watoto wa watoto wa watoto wetu, na kuendelea.
Hebu jiulize, lipi bora, kujinyima (kwa muda) ili kile tunachokusanya tukitumie kujenga kwanza miundombinu mbalimbali (SGR, Stiglers HEP, Barabara nzuri, hospitali na vifaa tiba, eropleni, mifumo ya maji, mashule na vyuo, n.k.); Au, tukitumie kuongeza mishahara ya watumishi, na kadhalika?
Ni wazi huwezi fanya mambo yote kwa wakati mmoja. Hakutokuwa na efficiency. Lazima uwe na priority and options.
"Roma haikujengwa kwa siku moja"; hali kadhalika Ulaya magharibi au Asia. Watu walijifunga vibwebwe na leo hii vitukuu wa vitukuu ndio wanafaidi jasho la babu zao
Kwa hiyo, JPM yuko sawa. Watumishi wa Serikali na Watanzania kwa jumla, tunapaswa kujifunga mkanda na kuridhika na hiki kidogo tunachopata sasa. Ni dhiki ya muda tu kwani tukiisha kamilisha kutengeneza miundombinu hii, Pesa inayokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali itatumika sasa kuboresha maisha ya watu. Tena kwa ulaiini kabisa. Serikali itakuwa na uwezo wa hata kufanya KCCCM kuwa zaidi ya 2,000/= kwa mwezi!
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki JPM.

mkuu umeandika vizuri ila tu kwa hoja za mtoa mada mfano , wafanyabiashara na wafanyakazi kaongea vizuri sana , inawezekanaje watumishi wafunge mikanda wengine hawafungi yahani mwalim umlipe laki nne kama mtumishi wakati yupo mtumishi mwingine analipwa mpaka 6 M, ALAFU tz hatuko kwenye vita wala nchi haiwezi jengwa kwa mara moja kwamba watu wafunge mikanda ,
pia swala la wafanyabiashara tatizo kubwa imekua kodi kubwa ambazo zimekua mizigo kwa wafanyabiashara sasa ukisema nao wafunge mikanda kuvumilia kodi hambazo hazilipiki na wakati huo wanafilisiwa na kufunga biashara kweli hapa kuna tija.

Maisha magum kwa tz chanzo kimekua na mzunguko mdogo wa pesa na nafikili wenda pia sababu za kuchangia hili kati ya mengine wenda hata hayo niliyotaja hapo juu yakawa yanachangia.

Mwisho ni lazima tuijenge tz yetu ila kufunga mkanda nakataa na hakuna sababu ya kufanya hivyo na wala mtumishi hawezi kukuelewa kwamba waendelee kufunga mikanda mpaka maendeleo yapatikane wakati nao ni sehem ya kuleta maendeleo
 
Wapo walio graduate mwaka huo huo wakaanzisha ufugaji wa kuku kwa msingi wa TZS 2,000,000 sasa hivi they are talking of 3 - 4mil a month. Msubiri Lisu, wengi wenu mnaamini nyumbani kwake amefunga bomba la ajira ambalo anasubiri achaguliwe ili alifunguwe ambao hamna ajira mpate ajira.
Endelea kuleta maneno ya mtaani na nadharia tu ukijifanya Eti unampamba au kumjenga huyo Magufuli kumbe unazidi kumuharibia.

Na marafiki zangu waliopoteza kazi Quality Group baada ya kampuni kufungwa kutokana na Mwenye kampuni kufirisiwa na serikali na kubambikiwa makesi na Serikali ya Magufuli nao unawaambiaje????

Na rafiki yangu ambae Ghala lake limeuzwa na bank baada ya kushindwa kurudisha mkopo baada ya serikali kuwapiga marufuku kununua korosho na kuchukua korosho kupitia jeshi nae unamwambiaje??? Tena kwenye kampuni yake alikuwa na watumishi 12 nao unawaambiaje????

Magufuli is a failure ndugu. Habebeki huyo mtu wenu. Kaharibu uchumi wa nchi!!
 
Kama kwa akili yako umefikiri kuandika haya basi Watanzania kwa uwingi wetu tunashida katika mifumo yetu ya fahamu.
Na kama kuna mtanzania wa aina yako anaetegemea Lisu ndio atabadilisha maisha yake, nakubaliana na wewe kua mna shida kwenye mifumo yenu ya fahamu. Maisha yako utayabadilisha mwenyewe kwa kuonyesha uthubutu katika kupambana na maisha badala ya kusubiri mwanasiasa akufanyie hivyo. Utasubiri sana kijana.
 
2020 watanzania tutamchagua JPM kwa kura za kutosha.
Mazuri ya JPM ni mengi sana,changamoto huwa zipo tu.hata U.S kuna raia wanalalamikia changamoto za taifa lao. ilhali tunaambiwa U.S ni kinara wa kila jambo la kimaendeleo.
Unapotaka kutowa mifano kumtetea kipenzi chako basi linganisha na nchi kama Rwanda, Kenya, Burundi, msumbiji and likes, usifananishe mlima Kilimanjaro na kichuguu utaonekana una kaswende ya ubongo.
 
Wapo walio graduate mwaka huo huo wakaanzisha ufugaji wa kuku kwa msingi wa TZS 2,000,000 sasa hivi they are talking of 3 - 4mil a month. Msubiri Lisu, wengi wenu mnaamini nyumbani kwake amefunga bomba la ajira ambalo anasubiri achaguliwe ili alifunguwe ambao hamna ajira mpate ajira.
Hizi kuku wanafugia wasapu na Instagram?

Unajuwa ufugaji wewe au unachamba mdomo tu?
 
Na kama kuna mtanzania wa aina yako anaetegemea Lisu ndio atabadilisha maisha yake, nakubaliana na wewe kua mna shida kwenye mifumo yenu ya fahamu. Maisha yako utayabadilisha mwenyewe kwa kuonyesha uthubutu katika kupambana na maisha badala ya kusubiri mwanasiasa akufanyie hivyo. Utasubiri sana kijana.
Watu wamethubutu, pita Quality Center sasa hivi frem zipo tupu maduka yamefungwa.
 
Endelea kuleta maneno ya mtaani na nadharia tu ukijifanya Eti unampamba au kumjenga huyo Magufuli kumbe unazidi kumuharibia.

Na marafiki zangu waliopoteza kazi Quality Group baada ya kampuni kufungwa kutokana na Mwenye kampuni kufirisiwa na serikali na kubambikiwa makesi na Serikali ya Magufuli nao unawaambiaje????

Na rafiki yangu ambae Ghala lake limeuzwa na bank baada ya kushindwa kurudisha mkopo baada ya serikali kuwapiga marufuku kununua korosho na kuchukua korosho kupitia jeshi nae unamwambiaje??? Tena kwenye kampuni yake alikuwa na watumishi 12 nao unawaambiaje????

Magufuli is a failure ndugu. Habebeki huyo mtu wenu. Kaharibu uchumi wa nchi!!
Whether he is a failure or not, not of business coz simtegemei magufuli kwa namna yeyote ile. it seems huna upeo wa kutosha wa kuelewa mfumo wa maisha ulivyo. Hao unaowatokea mifano hujui matatizo yao yaliyopelekea kujikuta katika hali waliyonayo. Kama wewe ulikua unaibia serikali kwa nini usifilisiwe. Kwa nini hutetei watumishi hewa? Bring facts and figures kuthibitisha magufuli ameharibu uchumi, usikariri maneno ya wengine.
 
Back
Top Bottom