Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu CCM Taifa, Rais Dkt. Magufuli tafadhali achana na Kauli kama hii katika 'Kampeni' zako kwani zinakuharibia na zinachanganya

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
"Leo tutakubaliana?, kwa sababu siku nyingine huwa nawaeleza halafu hamfuati,niliwaambia mnichague mimi mkasema sawa, nikawaambia mnichagulie na mbunge wa CCM hamkunichagulia, nataka niwaeleze ukweli wala siwafichi asingekuwa Kapuya hii barabara nisingeijenga, mambo ndivyo yanavyokwenda hivyo".Dkt.Magufuli

ITV Tanzania / Nipashe

Hivi nyie mlio karibu nae akina Dkt. Bashiru Ally na Mzee Philip Mangula kwanini msishauri aachane na Kauli za 'Kibabe' kama hizi? Tunachoka sasa!
 
Magufuli anachofanya sio sahihi alitakiwa ajiulize kwanini wabunge wa chama chake hawachaguliwi na sio kulazimisha wachaguliwe. Kila mtu ana uhuru na sababu kwanini amefanya maamuzi ya kuchagua kiongozi fulani.

Kama serikali ilinifanyia dhuruma kwanini niichague au kama imeleta kiongozi mbovu kwanini nichague lakini kitendo chake cha kukataa kuleta maendeleo kisa wamechaguliwa upinzani mbona kodi zao anachukua
 
Back
Top Bottom