Mwenyekiti, wanaCCM 415 Ngorongoro watimkia CHADEMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,652
2,627
Welcome back..nliwamiss sana JAMVINI. Kwa mujibu wa Aman Golugwa...mwenyekiti wa kijiji anamotoka mbunge wa ngorongoro Saning'o ole telele ni miongoni mwao..M4C NI NOUMER

Kutoka Gazeti la Mwananchi

VUGUVUGU la mabadiliko (Movement for change) na oparesheni ‘Vua gamba, vaa gwanda' jana vimeingia katika Kijiji cha Endulen, wilayani Ngorongoro baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho, Pettei Kitaika kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), akiwa na kundi la wanachama 415.

Mwenyekiti huyo aliyeshinda kiti hicho kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na mabalozi 10 na wenyeviti wawili wa vitongoji walijiunga Chadema baada ya kujiengua kutoka CCM.

Kijiji cha Endulen ndiko anakotoka Mbunge wa Ngorongoro, Saning'o Ole Telele (CCM).

Baada ya kupokewa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Mchungaji Amani Golugwa na kukabidhiwa kadi ya Chadema. Kitaika aliahidi kuibomoa CCM katika kijiji hicho na kuhakikisha Serikali yote ya kijiji inahamia upinzani.

"Naendelea na majadiliano na baadhi ya wenyeviti wa vitongoji na mabalozi wa nyumba kumi ambao wengi wameonyesha kuchoshwa na vitendo vinavyoendelea ndani ya CCM ili wote wahamie Chadema siku ambayo viongozi wa mkoa watafika kufanya mkutano wa hadhara Endulen," alisema Kitaika.

Akizungumzia wanachama hao wapya, Mchungaji Golugwa alisema kuwa kuhamia Chadema kwa wanachama hao wa CCM ni mwendelezo wa harakati oparesheni za kuhimiza mabadiliko katika mfumo wa uongozi kisiasa, kiuchumi na kijamii ulioanza kuenea nchi nzima baada ya kuzinduliwa mkoani Arusha mwezi Machi, mwaka huu.

Alisema katika mfululizo wa mikutano ya oparesheni vua gamba, vaa gwanda unaoendelea sehemu mbalimbali nchini, Chadema itawapokea na kuwafundisha viongozi na wanaCCM wote watakaoonyesha kujitambua na kujutia ushiriki wao kwenye matendo ya kuhujumu uchumi, masilahi na rasilimali za taifa.

Alisema mipango iko njiani kupeleka mikutano ya vuguvugu la mabadiliko katika wilaya zote za Mkoa wa Arusha katika ziara zitakazoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema pamoja na James Ole Millya aliyejiengua CCM na kujiunga na Chadema hivi karibuni.
 
Hapa ni kukaza buti, mwendo ni kuvua gamba na kuvaa gwanda...
 
No empire has ever lasted for ever; never! THIS IS INDEED THE CHANGE WE NEED! God bless this poor nation!
 
Katibu mchungaji Golugwa akimkaribishj katibu padri mstaafu Slaa. Propagandaa..
 
Nilimsikia Nape kupitia TBC akikanusha kkuwa hizi taarifa ni za uongo na zina kuuzwa sana na vyombo vya habari

" numefuatilia takwimu hadi sasa vongozi waliohamia CDM hadi sasa hawazidi 6 mmoja ni m/kiti wa UVCCM mkoa mfulani sijui na hawa wananchi wanaosemwa kuwa wamehamia CDMkwa makundi ukifuatilia record watu hao hawapo "

my take NAPE: Mchungaji mwema huacha wengine 99 na kumtafuta mmoja tu aliye potea
 
Nilimsikia Nape kupitia TBC akikanusha kkuwa hizi taarifa ni za uongo na zina kuuzwa sana na vyombo vya habari

" numefuatilia takwimu hadi sasa vongozi waliohamia CDM hadi sasa hawazidi 6 mmoja ni m/kiti wa UVCCM mkoa mfulani sijui na hawa wananchi wanaosemwa kuwa wamehamia CDMkwa makundi ukifuatilia record watu hao hawapo "

my take NAPE: Mchungaji mwema huacha wengine 99 na kumtafuta mmoja tu aliye potea

kwa makusudi kabisa .... nape yupo kwa ajili ya kukiua chama cha mapinduzi
 
mnisamehe bure SIPENDI neno ALIYEKUA MBUNGE WA ARUSHA mjini wakati mimi na wengine wana wa chugga tunamtambua kuwa yeye ndiye chaguo letu!
M4C DAIMA ...1
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom