TANZIA Mwenyekiti wa zamani wa TFF, Alhaj Said Hamad El Maamry afariki dunia akiwa ana umri wa miaka 86

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,335
aliyewahi kuwa mwenyekiti wa FAT taifa Sasa tff bwana Said el MAAMRY amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

=====

MWENYEKITI WA ZAMANI WA TFF, ALHAJ SAID HAMAD EL MAAMRY AFARIKI DUNIA AKIWA ANA UMRI WA MIAKA 86.​

MWENYEKITI wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho (TFF) na aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini, Wakili Said Hamad El Maamry amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam akiwa ana umri wa miaka 86.

Alhaj El Maamry amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi kwa zaidi ya miaka mitano, yaliyomsababishia maradhi ya kifua, shingo na mkono wa kulia kushindwa kufanya kazi kwa kipindi chote hicho.

El Maamry ambaye mwaka 1973 kwa mara ya kwanza alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa FAT katika uchaguzi mkuu uliofanyika Tanga, amewahi kuwa mjumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuanzia mwaka 1980 hadi 1986 kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa heshima mwaka 1998.

El Maamry ambaye akiwa kiongozi mkuu wa soka ya Tanzania, Taifa Stars ilicheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza mwaka 1980, amewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Mwaka 1976 Waziri wa Michezo, Mirisho Sarakikya alivunja Kamati ya Utendaji ya FAT iliyoongozwa na El Maamry kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utawala mbovu, akambakisha madarakani Katibu Mkuu, Hassan Chabanga Dyamwalle pekee (marehemu pia).

Hayo yalifanyika wakati Taifa Stars ikiwa na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Nigeria kujiandaa na mechi za kufuzu kucheza Fainali za Afrika ambazo zilikuwa zikifanyika Addis Ababa Ethiopia ndipo El Maamry akaambiwa kuanzia siku ile si Mwenyekiti tena wa FAT lakini aendelee kuwa karibu na wageni mpaka watakapoondoka.

Hata hivyo, serikali ikamruhusu kugombea katika uchaguzi wa FAT uliofanyika mwaka huo huo na akashinda na kuendelea kuongoza hadi mwaka 1986 alipoondoshwa akiwa kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Mexico ambako alialikwa, kabla ya kupigwa marufuku hata kugombea aliporejea kufuatia mchujo wa wagombea kufanywa akiwa nje ya nchi.

Katika uchaguzi mkuu wa FAT uliofanyika Mbeya, nafasi ya Mwenyekiti hakupatikana mtu, hivyo Makamu Mwenyekiti Mbeyela akakaimu nafasi ya Mwenyekiti hadi mwaka 1989 alipochaguliwa Mohamed Mussa kuwa Mwenyekiti aliyeongoza FAT hadi mwaka 1992 huku El Maamry akibaki kuwa Mjumbe wa Heshima wa CAF tangu alipoteuliwa mwaka 1998.
Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.
Marehemu Said El Maamry (kulia), hapa akiwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Morogoro akimshuhudia Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo, Lawi Nangwanda Sijaona akikagua timu ya soka ya Jeshi la Polisi Morogoro mwaka 1965.
 
Mwenyekiti wa zamani wa FAT(kwa sasa TFF) amefariki dunia alipokuwa anapata tiba Muhimbili. Alikuwa na Miaka 80+.

Chanzo cha habari: Daily News

Gwiji la soka la Tanzania limetutoka.
 
Mwenyekiti wa zamani wa FAT(kwa sasa TFF) amefariki dunia alipokuwa anapata tiba Muhimbili. Alikuwa na Miaka 80+.

Chanzo cha habari: Daily News

Gwiji la soka la Tanzania limetutoka.
Haya tumekusikia. Ulikua unakimbilia wapi mpaka kuandika hivi?

RIP
 
Rip Kiongozi El-Maamry.

Alikuwa Shabiki wa Simba huyu, hivyo ni dhahiri leo Simba itashinda.
Kwenye Game ya Simba na Kaiza pia tulifiwa na Bibi yake Haji (Tunajua matokeo yalikuwaje)
 
CHAMA CHA MAPINDUZI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kiongozi wa zamani wa soka nchini Said Hamad Elmamry na Mwanamuziki maarufu wa bendi ya Kilimanjaro (wana njenje) Ndugu Waziri Ally Kisinger.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amesema vifo hivyo ni pigo kwa tasnia ya michezo, sheria pamoja na muziki.

“Tunaziombea familia za Mwanasheria Elmamry na Waziri Ally kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na ustahamilivu” Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Said Hamad Elmamry katika maisha na uhai wake aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania 2009-2018, Mkuu wa Polisi Mkoa Morogoro, Wakili mashuhuri, Mjumbe wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki (CECAFA) na Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu (Tanzania Football Associations of Tanzania- FAT) kwa miaka kadhaa.

Kwa upande wake mwanamuziki Waziri Ally Kisinger ameacha unyonge na simanzi katika anga la muziki kutokana na umahiri wake wa upigaji wa kinanda, ubunifu wa midundo, utunzi wa nyimbo na uimbaji wake.

Chama cha Mapinduzi(CCM) kinaziombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze Roho za marehemu mahali pema peponi pia kinaziombea familia za marehemu hao azipe ustahamilivu na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na wapendwa wao.

Sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
25 Julai, 2021
 
Rip

IMG-20210724-WA0080.jpg
 

Said El Maamry afariki dunia, kuzikwa leo Dar​

4 weeks ago
Mwenyekiti wa Zamani wa Chama cha soka nchini (FAT) sasa TFF Said Hamad El Maamry amefariki dunia. El Maamry ambaye alikuwa pia Mwanasheria maarufu aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT, amefariki usiku wa kuamkia leo Hospital ya Taifa Muhimbili.
Tayari familia ya marehemu imeshatangaza taratibu za maziko ya Marehemu mpendwa wao.

RATIBA YA MAZIKO ya ALHAJ SAID HAMAD EL MAAMRY
Jumapili tarehe 25/07/2021
Saa 9:00 Alasir: Mwili wa marehemu ALHAJ SAID HAMAD EL-MAAMRY utakuwepo Masjid Al Maamur.

Shughuli zote za maziko zitafanyika Masjid Al Maamur (kwa wanawake na wanaume).

Mwili wa Marehemu utaswaliwa baada ya Swalat Asr.

Marehemu ALHAJ SAID
EL MAAMRY ataenda kupumzishwa katika makaburi ya Kisutu baada ya Swalat Asr. Mwenyezi Mungu ampe Mzee wetu mapumziko mema na amuweke pamoja na waja wema peponi, Ameen.
 

Said El Maamry afariki dunia, kuzikwa leo Dar​

4 weeks ago
Mwenyekiti wa Zamani wa Chama cha soka nchini (FAT) sasa TFF Said Hamad El Maamry amefariki dunia.
El Maamry ambaye alikuwa pia Mwanasheria maarufu aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT, amefariki usiku wa kuamkia leo Hospital ya Taifa Muhimbili.
Tayari familia ya marehemu imeshatangaza taratibu za maziko ya Marehemu mpendwa wao.
RATIBA YA MAZIKO ya ALHAJ SAID HAMAD EL MAAMRY
Jumapili tarehe 25/07/2021
Saa 9:00 Alasir: Mwili wa marehemu ALHAJ SAID HAMAD EL-MAAMRY utakuwepo Masjid Al Maamur.
Shughuli zote za maziko zitafanyika Masjid Al Maamur (kwa wanawake na wanaume).
Mwili wa Marehemu utaswaliwa baada ya Swalat Asr.
Marehemu ALHAJ SAID
EL MAAMRY ataenda kupumzishwa katika makaburi ya Kisutu baada ya Swalat Asr.
Mwenyezi Mungu ampe Mzee wetu mapumziko mema na amuweke pamoja na waja wema peponi, Ameen.

Apumzike kwa amani Said El Maamri.

Itakuwa siyo Corona.

Ila tarehe hapo zinasoma July ..?!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Waislam uwa awacheleweshi kuzika ila uyu hadi Jumapili. Noma.

Apumzike kwa Amani.
 
Back
Top Bottom