Mwenyekiti wa zamani UWT kortini kwa kughushi cheti cha ndoa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda amedai leo Ijumaa Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Anifa Mwingira kuwa Februari 4, 1995 jijini Dar, es Salaam kwa nia ya kudanganya mshtakiwa huyo alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078.

Amedai kuwa alifanya hivyo kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na Silvanus Mzeru (marehemu) Februari 4, 1995 katika kanisa Katoliki Mburahati wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, amekana na kudai Mzeru ni mumewe.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Mtubika Godfrey na Juma Nyamgaruri waliiomba mahakama kumpatia dhamana mteja wao kwa sababu shtaka linalomkabili kwa mujibu wa sheria linadhaminika.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo namba 365 ya mwaka 2019 hadi Julai 17, 2019 itakapotajwa tena huku mshtakiwa akiachiwa kwa dhamana.
 
UWT ya kina Sophia Simba ilikuwa hatare kweli, ilijaa Minyakanga na Mikungwi ya Mjini mitupu!

Husna Mwilima, Asha Baraka huku Sophia mwenyewe

Anne Kilango alijaribu kusogeza Kwato yake akashindwa
Mbona mashambulizi kwa uongozi wa awamu ya nne. Sofia Simba anahusikaje na ndoa ya mtu. Sifia Simba ni wa mjini, Jakaya Mrisho Kikwete wa mjini pia na mambo yao ni mjini ulitaka wawe wa shamba na mambo ya kishamba kama kutekana tekana?
Waliongoza kistaarabu, ustarabu ulianzia pwani kwenda bara. Mpaka leo bara ustaarabu haujafika.
 
UWT ya kina Sophia Simba ilikuwa hatare kweli, ilijaa Minyakanga na Mikungwi ya Mjini mitupu!

Husna Mwilima, Asha Baraka huku Sophia mwenyewe

Anne Kilango alijaribu kusogeza Kwato yake akashindwa
Asha Baraka enzi zake alishawahi kuuzingua msafara wa JK wkt wakiwa wanatoka msikitini kuswali,simpatii picha leo audindie msafara wa Magu atakachofanywa mpk twanga pepeta watamuimbia wimbo wa kutoa pole kwa mgonjwa.
 
Hivi ccm imeshindwaje kumuokoa huyu mtu wao ?
 
huyu mama kama hakufunga ndoa na Mzeru kayataka maana mtaani tunämtambua kama mke wa marehemu tangu miaka ya 80 na amezaa nae mabintii wawili wakubwa Grace na Flora.ila marehemu alikuwa na mali sana *****
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda amedai leo Ijumaa Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Anifa Mwingira kuwa Februari 4, 1995 jijini Dar, es Salaam kwa nia ya kudanganya mshtakiwa huyo alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078.

Amedai kuwa alifanya hivyo kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na Silvanus Mzeru (marehemu) Februari 4, 1995 katika kanisa Katoliki Mburahati wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, amekana na kudai Mzeru ni mumewe.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Mtubika Godfrey na Juma Nyamgaruri waliiomba mahakama kumpatia dhamana mteja wao kwa sababu shtaka linalomkabili kwa mujibu wa sheria linadhaminika.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo namba 365 ya mwaka 2019 hadi Julai 17, 2019 itakapotajwa tena huku mshtakiwa akiachiwa kwa dhamana.
Sasa si waende kanisani kuthibitisha,mbona rahisi tu
 
Kumbe hadi vyeti vya ndoa watu wanafoji.......Kama ni ivyo Mzee magu alianzishe swala la vyeti vya ndoa ili madogo wa mtaani waache kukaa vijiweni
 
Asha Baraka enzi zake alishawahi kuuzingua msafara wa JK wkt wakiwa wanatoka msikitini kuswali,simpatii picha leo audindie msafara wa Magu atakachofanywa mpk twanga pepeta watamuimbia wimbo wa kutoa pole kwa mgonjwa.
Baba Rizi alikuwa anasimamia kucha nn mkuu?
 
Back
Top Bottom