Mwenyekiti wa zamani UWT kortini kwa kughushi cheti cha ndoa

UWT ya kina Sophia Simba ilikuwa hatare kweli, ilijaa Minyakanga na Mikungwi ya Mjini mitupu!

Husna Mwilima, Asha Baraka huku Sophia mwenyewe

Anne Kilango alijaribu kusogeza Kwato yake akashindwa

Sasa hivi imebadilika?
 
Mbona mashambulizi kwa uongozi wa awamu ya nne. Sofia Simba anahusikaje na ndoa ya mtu. Sifia Simba ni wa mjini, Jakaya Mrisho Kikwete wa mjini pia na mambo yao ni mjini ulitaka wawe wa shamba na mambo ya kishamba kama kutekana tekana?
Waliongoza kistaarabu, ustarabu ulianzia pwani kwenda bara. Mpaka leo bara ustaarabu haujafika.
Hata Koromije haujafika bado?
 
Mbona mashambulizi kwa uongozi wa awamu ya nne. Sofia Simba anahusikaje na ndoa ya mtu. Sifia Simba ni wa mjini, Jakaya Mrisho Kikwete wa mjini pia na mambo yao ni mjini ulitaka wawe wa shamba na mambo ya kishamba kama kutekana tekana?
Waliongoza kistaarabu, ustarabu ulianzia pwani kwenda bara. Mpaka leo bara ustaarabu haujafika.
Hata Koromije haujafika bado?
 
Kumbe hadi vyeti vya ndoa watu wanafoji.......Kama ni ivyo Mzee magu alianzishe swala la vyeti vya ndoa ili madogo wa mtaani waache kukaa vijiweni
CCM wote ndiyo michezo yao. Halafu wale wakubwa wenye vyeo ndiyo wanalindana. Zoezi la vyeti feki lingefanywa kwa halali kuanzia kwa Raisi mpaka balozi. Ungeshangaa hata Magu naye ni mhusika wa vyeti feki. Hivyo vyeti feki vya ndoa waanzie kwa Raisi mpaka balozi uone madudu yao lakini kutokana na CCM kuweka sheria kandamizi itawapitia wachache.
Tanzania hakuna sheria ya haki bali kuna sheria kandamizi ambazo zinatungwa kwa watu fulani tu. Mwanao na mtoto wa jirani wamefanya kosa lakini anayeadhibiwa ni wa jirani. Mimi huwa naamini kuna watu wapo juu ya sheria.
 
Bongo kwa kufukua makaburi ili tukomoane hatujambo, tokea 95 hadi leo, may be kuna kitu behind the scene.
Shida ya wanasiasa wengi wanapenda kuwazika wenzao wakiwa wazima. Haya ndio yanayojiri baada ya nguvu zao kupotea
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda amedai leo Ijumaa Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Anifa Mwingira kuwa Februari 4, 1995 jijini Dar, es Salaam kwa nia ya kudanganya mshtakiwa huyo alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078.

Amedai kuwa alifanya hivyo kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na Silvanus Mzeru (marehemu) Februari 4, 1995 katika kanisa Katoliki Mburahati wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, amekana na kudai Mzeru ni mumewe.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Mtubika Godfrey na Juma Nyamgaruri waliiomba mahakama kumpatia dhamana mteja wao kwa sababu shtaka linalomkabili kwa mujibu wa sheria linadhaminika.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo namba 365 ya mwaka 2019 hadi Julai 17, 2019 itakapotajwa tena huku mshtakiwa akiachiwa kwa dhamana.
Cheti cha ndoa tu kinakua tabu kiasi hicho !!
Mbona kuna mabosi kwenye idara za Afya wana vyeti vya kughushi na wanakalia ofisi kwa mbwembwe huku wakiendelea kula mishahara na marapurupu ya serikali.??

Basi nadhani awamu hii imedhamiria kabisa kuondoa udanganyifu kwenye jamii hasa masuala ya vyeti.

Naipongeza serikali kwa hilo .
 
Asha Baraka enzi zake alishawahi kuuzingua msafara wa JK wkt wakiwa wanatoka msikitini kuswali,simpatii picha leo audindie msafara wa Magu atakachofanywa mpk twanga pepeta watamuimbia wimbo wa kutoa pole kwa mgonjwa.
Hata mawazo tu ya kufanya hivyo hayampitii😁
 
Cheti cha ndoa tu kinakua tabu kiasi hicho !!
Mbona kuna mabosi kwenye idara za Afya wana vyeti vya kughushi na wanakalia ofisi kwa mbwembwe huku wakiendelea kula mishahara na marapurupu ya serikali.??

Basi nadhani awamu hii imedhamiria kabisa kuondoa udanganyifu kwenye jamii hasa masuala ya vyeti.

Naipongeza serikali kwa hilo .
Makonda vipi vyeti vyake?
 
Makonda vipi vyeti vyake?
Jinai haiishi.
Zamu yake haijafika.
Kila zama na kitabu Chake.

Zamu yake ya kucheka.
Kila jambo na majira yake.
Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna, wakati wa Kuzaliawa na wakati wa Kufa, wakati wa kucheka na wakati wa kulia, Wakati wa kufurahi na wakati wa kuomboleza.
 
Back
Top Bottom