Mwenyekiti Wa Wazee Wa Mila Wa Kimasai (Malaigwanan) Tanzania, Mzee Isaack Oleksongo Asema Julius Kalanga Atashinda, Amshauri Lowassa Arudi CCM

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Mwenyekiti wa Wazee wa Mila wa Kimasai Tanzania, maarufu kwa jina Malaigwanan, Isaac Oleksongo Neijo amemshauri Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa kufanya uamuzi mgumu kwa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akibainisha kuwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM, julius Kalanga atashinda katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika 16/09/2018.

"Hata Lowassa anaelewa sana uamuzi wetu isipikuwa hana la kufanya, lakini mimi binafsi nimemshauri kurudi CCM, huyu ni rika langu, angetoka tu (Upinzani) na anajua kuna kila dalili ushindi kwa Kalanga" anasema mzee Oleksongo.
"mimi mwenyewe ndiye niliyeomba Kalanga arudishwe kugombea ubunge, niliomba kwenye CCM wamrudushe kwa sababu alikuwa na nidhamu, alinifuata kwenye baraza la malaigwanan kutueleza nia yake ya kutaka kujiuzulu ubunge, akatueleza sababu za ugumu wa kazi, akatueleza hataki kuwa mbunge wa kupokea posho , nataka uongozi wa CCM utambue kuwa Monduli ni CCM, nilifanya makosa 2015 kwa sababu ya matarajio yenu, hilo halipo tena Tumerudi" aliendelea kusema Mzee Ole Kisongo

Source: Raia Mwema leo 10/09/2018

IMG_20180910_104404.jpg
 
Mwenyekiti wa Wazee wa Mila wa Kimasai Tanzania, maarufu kwa jina Malaigwanan, Isaac Oleksongo Neijo amemshauri Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa kufanya uamuzi mgumu kwa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akibainisha kuwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM, julius Kalanga atashinda katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika 16/09/2018.

"Hata Lowassa anaelewa sana uamuzi wetu isipikuwa hana la kufanya, lakini mimi binafsi nimemshauri kurudi CCM, huyu ni rika langu, angetoka tu (Upinzani) na anajua kuna kila dalili ushindi kwa Kalanga" anasema mzee Oleksongo.
"mimi mwenyewe ndiye niliyeomba Kalanga arudishwe kugombea ubunge, niliomba kwenye CCM wamrudushe kwa sababu alikuwa na nidhamu, alinifuata kwenye baraza la malaigwanan kutueleza nia yake ya kutaka kujiuzulu ubunge, akarueleza sababu za ugumu wa kazi, akarueleza hataki kuwa mbunge wa kupokea posho , nataka uongozi wa CCM utambue kuwa Monduli ni CCM, nilifanya makosa 2015 kwa sababu ya matarajio yenu, hilo halipo tena Rumerudi" aliendelea kusema Mzee Ole Kisongo

Source: Raia Mwema leo 10/09/2018

View attachment 861914
Huyu mheshimiwa angewasilkilza tu hawa malaigwani
 
Back
Top Bottom