Mwenyekiti wa wazee CHADEMA kata ya Bomani wilayani Tarime ahamia CCM akidai imebadilika

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema katika kata ya Bomani wilayani Tarime, Morice Matius amehamia CCM akidai kuvutiwa na mabadiliko ya chama hicho.

Akikabidhi kadi ya Chadema, skafu mbili na fulana mbili za chama hicho kwenye mkutano wa halmashauri ya CCM wilayani hapa, Matius ambaye pia ni mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Buhemba alisema ameamua kujiunga na chama hicho kutokana na mabadiliko yanayofanywa na Serikali.

Alisema moja ya ajenda iliyokuwa ikizungumzwa na Chadema kipindi cha nyuma ni kutokuwapo kwa ndege za Serikali, mikataba mibovu ya madini na kero zingine ambazo zimeanza kutatuliwa huku nyingi zikiwa zinapatiwa ufumbuzi.

Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorius Luoga alisema kila mwanachama wa CCM anatakiwa kwenda na kasi ya Serikali iliyopo madarakani.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Tarime, Godfrey Frances alisema moja ya sababu ya upinzani kushinda kwenye chaguzi ni kutokana na baadhi ya viongozi wa CCM kutokuwa tayari katika kutetea masilahi ya wananchi.
 
Mafuriko hayazuiwi kwa mikono. Ufipani kunafuka moshi wa moto na joto kali. Muda utatoa taswira kamili.
 
81ca5dccc2ad6fa502df27807cacf0a8.jpg
 
Kamanda mmoja akifika bei, tunaachana naye - sisi wengine tuliobakia tunachanja bunga!! CDM si jeshi la mtu mmoko.
 
Chadema si chama cha mchezo mchezo, yaani mwenyekiti wa kata tu ndio mnaona kama mwenyekiti wa mkoa?!
 
kitu kimoja ninachofahamu kuhusu albadir ni kuwa ikitumwa (kusomwa) kwa mtu kimakosa basi hurudi kwa hasira kwa msomaji na kumdhuru mwenyewe......hayo ndiyo niliyoyasikia kule kilwa!!!
 
Back
Top Bottom