Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete akiwa Arizona!!!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
April 22nd, 2011

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA). Mama Salma Kikwete akizungumza pamoja na kujibu masuali ya wanafunzi wa Thunderbird School of Global Management hawapo pichani..April 20.2011.

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) Rais wa Thunderbird School of Global Management Rais Daktari Angel Cabrera, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mwanaidi Maajar, Rais wa Project C.U.R.E Daktari Douglas Jackson pamoja na mjumbe wa Bodi ya WAMA Zakhia Meghji wakimsikiliza kwa makini mwanafunzi wa Kitanzania anaesona chuoni hapo Niky Choksi( hayupo pichani) akitoa maelezo yake ya masomo ya kozi yake chuoni hapo anayochukua.

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipewa maelezo yamaendeleo ya Thunderbird School of Global Management kutoka kwa Rais wa chuo Daktari Angel Cabrera (kulia) April 20,2011 alipokwenda kuzungumza na wanafunzi.

Mwanafunzi wa Kitanzania anaesoma Thunderbird School of Global Management Arizona Niky Chokshi (mbele) akitoa maelezo ya chuo kwa Mama Mwenyekiti wa WAMA pamoja na ujumbe wake. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
 
ndo maisha yaho, first lady wa kiiafrika huwa lazima watanue, nayeye ndo kapata wacha ale kodi zetu siku tukifunguka macho vizuri tutapunguza matumizi yao maana first lady yeyote ni lazima kodi yetu imhudumie, suala linakuwa je matumizi yote anayofanya ni sawa?? je kumwekee limit ya bajeti yake au iwaendelee kula nchi kwa jinsi anavyojisikia yeye na wale wanaomzunguka.
 
Somesheni wake zenu,kimombo kwa sana msije mkaaibika .Huenda ikawa ndiyo ma future first lady.
 
Sipati picha kiingereza kilichokuwa kinazungumzwa pale, maana kiswahili chenyewe huwa kimepindapinda....
 
ndo maisha yaho, first lady wa kiiafrika huwa lazima watanue, nayeye ndo kapata wacha ale kodi zetu siku tukifunguka macho vizuri tutapunguza matumizi yao maana first lady yeyote ni lazima kodi yetu imhudumie, suala linakuwa je matumizi yote anayofanya ni sawa?? je kumwekee limit ya bajeti yake au iwaendelee kula nchi kwa jinsi anavyojisikia yeye na wale wanaomzunguka.
Hivi Maria nyerere akiwa fl wa-tz walikuwa wamefunguja macho?
 
Ningependa mwanajamii mmoja mwanadada anijuze mwenzenu kama uwepo wa nafasi hiyo "UENYEKITI" wa akinamama una maslahi na wanawake,Na pia aeleze kama amenufaika na Mama Salma kuwa mwenyekiti..tafadhali nisaidiwe kabla sijachangia chochote.
 
FL nimemuona kwenye michuzi anajitahidi ila anasoma A to Z anaongea kama amepanic hivi sijui ndio audience ya wazungu.Mwalimu kamsaidia kuweza kusoma sijui sasa kile cha kupiga story za kawaida anaweza.
 
FL nimemuona kwenye michuzi anajitahidi ila anasoma A to Z anaongea kama amepanic hivi sijui ndio audience ya wazungu.Mwalimu kamsaidia kuweza kusoma sijui sasa kile cha kupiga story za kawaida anaweza.[/QUOTE]

yes, me tanzania there, cool and peace of true, welcum again in our country in africa, we have manyara animals, serengeti,
and big tens animal parks. welcum and plant mount kilimanjaro, the tallest in africa.in our country last year hungry
intered there, even me i felt femine
 
Ningependa mwanajamii mmoja mwanadada anijuze mwenzenu kama uwepo wa nafasi hiyo "UENYEKITI" wa akinamama una maslahi na wanawake,Na pia aeleze kama amenufaika na Mama Salma kuwa mwenyekiti..tafadhali nisaidiwe kabla sijachangia chochote.

Hacheni kuwa kama malmbukeni, someni magazeti muongeze knowledge na sio kusoma mwanaspoti na uwazi tu.
Huyu mama ni m/kiti wa WAMA ambayo ni NGO yake yeye kama 1st lady na sio wanawake wote, ya Mama Mkapa iliitwa Mfuko sawa kwa wote. Na kama umefuatilia hii safari kachangishiwa shs 45 billion, lakini watz reasoning yenu ilivyo potofu mnacrush kila kitu.
 
je inamána hujelewa swali la msingi."JE TAASISI HIZI ZA FAST LADY WETU ZINAMNUFAISHA NANI NA KWA KIASI GANI?.
 
Ningependa mwanajamii mmoja mwanadada anijuze mwenzenu kama uwepo wa nafasi hiyo "UENYEKITI" wa akinamama una maslahi na wanawake,Na pia aeleze kama amenufaika na Mama Salma kuwa mwenyekiti..tafadhali nisaidiwe kabla sijachangia chochote.

Waliofaidika wapo kibao tu, nenda kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji utakuta shule ya kisasa imejengwa hapo zaidi ya bilioni 1.9 zimetumika na aliezitafuta ni yeye m/k wa WAMA Mhe Mama Salma Kikwete. Shule hiyo imechukua wanafunzi wa kike toka mikoa yote Tanzania nzima bara na visiwani ni shule pekee kwa wote. Wanafunzi hao ni wale wa familia duni na yatima. Wanagharimiwa kila kitu kuanzai ada,sare za shule na vyakula n.k wao kazi yao ni kusoma tu.

Wanawake wengine waliofaidika ni toka mikoa yote ya Tanzania kupitia ziara zake za mikoani mama Salma Kikwete alitoa misaada ya vifaa vya uzazi na vya kutolea huduma ya afya vyenye thanmani ya zaidi ya Milioni 300 katika vituo vya Afya 66 Nchi nzima . Na pia alichangia vikundi vya kina mama zaidi ya Milioni 152 . Pesa hizi zote hazikutoka Ikulu zimechangwa na Wasamalia wema wanaovutiwa na jitahada zake nae hazibania amerejesha kwa Wananchi husasan akina mama . Mwenye kutaka data kamili atembelee WAMA atapatiwa taarifa za Fedha na hesabu zilizokaguliwa WAMA inazingatia utawala bora , MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI MAMA SALMA KIKWETE AMETEKELEZA WAJIBU WAKE KAMA MAMA WA TAIFA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom