Mwenyekiti wa Wafanyabiashara akanusha maagizo ya Paul Makonda

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,576
2,000
Namsikiliza hapa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam kupitia BBC, anakanusha kuwepo kwa punguzo la bei kwa bidhaa kwenye maduka ambayo mkuu wa mkoa wa Dar Ndg Makonda ameyataja.

Makonda alitoa maagizo ya kuwepo punguzo ili watu wajipatie bidhaa zikiwemo mavazi kwa ajili ya kusheherekea anakosema Makonda kwamba ni kupungua kwa maambukizi ya Covid-19.

Anasema wao hawana taarifa na hayo maagizo na wala hakuna mazungumzo yaliyofanyika jinsi gani watafidiwa hivyo wataendelea kuuza kwa bei zao za zamani.
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
5,953
2,000
Tupatie jina la Mwenyekiti mbona habari ipo nusunusu asije kuwa yule aliyeenda kumwona Lowassa kipindi Lowassa yupo Chadema
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,177
2,000
Makonda anajitaidi Sana Lakin bahat Hana
Unataka awe na bahati ya namna gani zaidi ya hiyo iliyomfikisha hapo alipo?

Zamani niliviheshimu sana hivi vyeo. Mtu anateuliwa kuwa kiongozi wa mkoa au waziri, niliona kuwa huyo mtu anazo sifa za kipekee katika jamii nzima zilizomfikisha kwenye cheo nafasi kama hiyo.

Uteuzi katika awamu hii, umedhihirisha pasi na shaka yoyote kwamba nafasi hizo hazihitaji mtu awe na sifa inayomtofautisha na raia wengine katika jamii.

Hata jambazi anaweza kuwa kwenye nafasi hiyo, mradi tu anayeteua apende iwe hivyo!
 
Top Bottom