Wanadamu wengi wanaokuwa kwenye kazi na kuondoka au wanapofariki huwa wanakumbukwa kwa yale mema waliofanya walipokuwa kwenye ile ofisi au duniani. Kwa mtazamo huo yupo mtu aliyekuwa mhimu kwa mustakabali wa Tanzania huyu si mwingine ni Jaji mstaafu aliyekuwakuwaMwenyekiti wa tume ya uchaguzi Lewis Makame ambaye kwa mujibu wa vyombo vya habari amefikia mwisho wa utumishi wake. Sasa tujiulize Watanzania tunaweza kumkumbuka kwa yapii mema au ni alama gani ameiacha ambayo kwayo atakumbukwa kwayo?