Mwenyekiti wa tawi la CHADEMA- Manga Njombe avuliwa nguo na kuwekwa ndani 24hrs

lutondwe

Senior Member
Dec 20, 2010
150
74
Hali ya kisiasa Njombe imeanza kuharibika baada ya jana mwenyekiti wa tawi la Manga kata ya Mahongole(Njombe kaskazini) kukamatwa na kuwekwa kizuizini bila kuwa na nguo mwilini. Kitendo hicho kilifanywa na mwenyekiti wa CCM kijiji cha Manga. Alipigwa kama mbwa na kuwekwa ndani siku nzima hadi pale viongozi wa CHADEMA wilaya ya Njombe walipofika na kufanya mipango ya kumwokoa.

Sababu ya kuwekwa ndani ilikuwa ni kitendo cha kufanya maandalizi ya mkutano wa CHADEMA ambapo ulipangwa kufanywa tarehe 12.8.2012. Baada ya kuokolewa ndani ya Lupango kwenye ofisi ya kijiji viongozi wa CHADEMA waliamua kumpeleka moja kwa moja hospitalini ambako amelazwa hadi sasa.

Leo CHADEMA tayari kimefungua kesi katika mahakama ya wilaya ya Njombe kwa makosa makubwa mawili ya udhalilishaji (defamation) ambayo ni Kuwekwa ndani kwa muda mrefu bila uwezo wa kisheria kufanya hivyo na kosa la pili ni kosa la udhalilishaji (libel). Katika makosa hayo mshitakiwa anatakiwa kulipa 50 milioni.

Pia chama kimemfungulia kesi mwenyekiti huyo wa CCM kesi jinai (criminal) kutokana na kitendo chake cha kushusha bendera ya CHADEMA na kuzichana kinyume cha sheria. Njombe kaskazini ni moja ya majimbo ambayo yanaongozwa na wanasiasa wa aina yake duniani (majah).
 
Hao Mumiani wa CCM kuna siku watakuja kusaga meno vipi ndio maagizo ya mwenyekiti wa CCM aliyoyatoa nchi hii sijui mauaji yataisha lini
 
Hali ya
kisiasa Njombe imeanza kuharibika baada ya jana mwenyekiti wa tawi la Manga kata ya Mahongole(Njombe kaskazini) kukamatwa na kuwekwa kizuizini bila kuwa na nguo mwilini.........

Nani aliyempiga? mwenyekiti? au?
 
pole zake hii hiyo ndio ccm haina huruma iko radhi hata kuua kwa ajili ya madaraka tu
 
harafu ww lutondwe ni ccm mzuri unakumbuka 2005 ulivyotusaliti na kuvaa magamba.? Ukatuacha wanachadema hatuna kwa kupeleka kula zetu!
 
nani aliyempiga? mwenyekiti? au?

Aaah! Na wewe kookolikoo, yaani unashindwa hata kuandika vizuri? Nani alikufundisha kuwa mara baada ya kiunganishi{mf na, au, n.k.} unaweza kuweka kiulizo?
Bahati yako, nitakupeleka jukwaa la lugha.

Turudi kwenye mada. Si mwenyekiti pekee yake aliyemkamata, kumpiga na kumdharirisha huyo ndugu. Mara wanatumia mgambo na vibaraka wao. Sasa unafanyaje kuwapata wote? Unamkamata kiongozi na kumshitaki, vidagaa utawapata tu.
 
Last edited by a moderator:
Wamelelewa vibaya hawa viongoz ndio maana wanashindwa kwenda na mabadiliko.Mungu awe na uyo jamaa na sheria itende haki
 
Alichofanyiwa Dr. Ulimboka lina tofauti gani na hili? Je, kwa matukio haya watu wanaposema ccm ni chama cha magaidi wanakosea?
 
Hii sasa ni Kali!! Hivi Hawa Mazuzu Hawajui Nchi inatawaliwa kwa siasa ya Vyama Vingi? sasa kwa nini Umdhalilishe Mwenzako? Naomba Peoples Power Tumchangia Huyu Mwenzetu aliyeathirika na Jitihada za Kutafuta Mabadiliko ya kweli!! Eh Mungu Umpe heri na apone Haraka kama Dr!!
 
Hii haikubaliki CHADEMA kwa wakati huu hebu ongezeni vijana na imalisheni kurugenzi ya sheria, maana naona kila kona M4C inapotaka kupita viongozi wanatishiwa. vijana wa sheria wapo wengi sana wakawatoe watu uoga.
 
Back
Top Bottom