Mwenyekiti wa Tawi (CCM) akamatwa na polisi kwa kuvunja tawi la CHADEMA

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Mwenyekiti serikali ya mtaa wa sanawari Arusha amekamatwa na polisi baada ya kuvunja tawi la chadema.

Awali uongozi wa chadema kata ya Sekei baada ya kupata taarifa ulikwenda kituo cha polisi Sekei kutoa taarifa. OCS wa kituo alisema japo walikuwa wana taarifa kuwa tawi litavunjwa na Godfrey, hawatatoa) ya kumkamata. Ikabidi uongozi wa chadema uende Kituo Kikuu cha Arusha na kuandika maelezo na kupewa RB.
Hata hivyo leo asubuhi kuliibuka taharuki kubwa nyumbani kwa mwenyekiti huyo wa mtaa aliyetokana na ccm, baada ya polisi kushindwa kumkamata jana, vijana wenye hasira walikusanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wakitaka kumchomea nyumba. Vijana walilalamika inakuwaje watumie fedha zao kujenga tawi halafu ccm wanakuja kuvunja bila sababu! Uongozi wa chadema kata ya Sekei ilibidi wawasihi vijana waliokusanyika kwa wingi wasifanye uharibifu wowote, wasubiri polisi wafanye kazi yao. Polisi walifika pale wakiongozwa na Inspector Daudi.
Hivi sasa huyo Mwenyekiti huyo yupo selo akisubiri dhamana
 
wange mmabina tu tupunguze idadi yao hawa vibaka na wezi wa mali za umma!
 
Unaposema 'amevunja tawi' unamaanisha nini? Ofisi? bendera? Amewahamisha wanachama?....??
 
Nnajua police walikuja baada ya kupata taarifa kuwa vijana walikuwa wameizingira nyumba ya mwenyekiti so walienda kumtetea asiuawe ,police acheni siasa fanyeni kazi yenu.Hivi mnafikiri mnaweza kumlinda huyo gamba (mizigo)wa ccm muda wote ?.
 
Hapa ndipo napowafagilia watu wa Mbeya na Mwanza...kwani wange mmabina kungekuwa na shida gani?... stupid Magamba...Bado hawajui kuwa Mashina ya CDM yako mioyoni mwa Raia ?....
 
siku nyingine kama polisi wanaringa kuwakamata wala msiwabembeleze, tumieni nguvu ya umma kumfikisha wenyewe polisi,,,,hongereni sana makamanda
 
Mwenyekiti serikali ya mtaa wa sanawari Arusha amekamatwa na polisi baada ya kuvunja tawi la chadema.

Awali uongozi wa chadema kata ya Sekei baada ya kupata taarifa ulikwenda kituo cha polisi Sekei kutoa taarifa. OCS wa kituo alisema japo walikuwa wana taarifa kuwa tawi litavunjwa na Godfrey, hawatatoa) ya kumkamata. Ikabidi uongozi wa chadema uende Kituo Kikuu cha Arusha na kuandika maelezo na kupewa RB.
Hata hivyo leo asubuhi kuliibuka taharuki kubwa nyumbani kwa mwenyekiti huyo wa mtaa aliyetokana na ccm, baada ya polisi kushindwa kumkamata jana, vijana wenye hasira walikusanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wakitaka kumchomea nyumba. Vijana walilalamika inakuwaje watumie fedha zao kujenga tawi halafu ccm wanakuja kuvunja bila sababu! Uongozi wa chadema kata ya Sekei ilibidi wawasihi vijana waliokusanyika kwa wingi wasifanye uharibifu wowote, wasubiri polisi wafanye kazi yao. Polisi walifika pale wakiongozwa na Inspector Daudi.
Hivi sasa huyo Mwenyekiti huyo yupo selo akisubiri dhamana
Hivi huyu Inspector Daud ni yule mkuu wa mkoa alitudanganya alikuwa anahojiwa kujusu bomu la Soweto??? Changa la macjo jilo,,, Nchimbi kwa mbwembwe katuambia hamna tume itaundwa,,, hahahaaaa sasa yuko uraiani damu za watu wa Arusha zitawaosha wote walio husika
 
Safi sana - mwache kwwnza aende selo, akirudi ajenge alipopaharibu fasta. Shenzi zake kwa kukosa ustaarabu
 
Ni kweli huyu bwana anaitwa GODFREY MOLLEL ni mwenyekiti wa Mtaa ninaoishi lakini huwa ana kiherehere sana.
Nimejipanga kumngoa ktk uchaguzi ujao mwakani endapo CCM watamrudisha kugombea tena.

Huyu jamaa huwa anapenda sana kunyanyasa na kuwatishia watu haswa Makabila,lakini kwangu huwa ananiogopa kuliko hata Kikwete.
Huyu habari yake kwisha.
 
huyu ocs aliesema walikuwa na taarifa kuwa ofisi ya CHADEMA itavunjwa lakini hawataweza kumkamata Godfrey alikuwa na maana gani ? Hebu akamatwe awekwe ndani ahojiwe ni kwa vipi au ni mdogo wake Mwigulu.?
 
Zamaan Mada Kama Hizi Zilikuwa Zikinigusa Sana Sema Tangu Mumpindue ZZK Sina Raha Kwa Kweli!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom